MEYA wa Manispaa ya Ilemela ambaye pia ni diwani wa Kata ya
Kitagiri aliyevulia uanachama wa Chadema, Henry Matata amechaguliwa kwa
mara nyingine kuwa Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa
(Alat) Mkoa wa Mwanza.
Uchaguzi huo umekuja kufuatia mabadiliko yanayotokana na Serikali kuanzisha wilaya na mikoa mipya.
Katika uchaguzi huo,Matata ambaye ni diwani wa Kata ya Kitangiri,alipita bila kupingwa hatua ambayo wajumbe wa Alat walilazimika kumpigia kura za ndiyo na hapana ambapo meya huyo alishinda kwa kupata kura 20 za ndiyo kati ya kura 21 zilizopigwa. Matata alifukuzwa uanachama wa Chadema na kamati kuu ya chama hicho,kisha kufungua kesi mahakamani kupinga kuvulia uanachama na hukumu ya kesi hiyo bado haijatolewa mahakamani.
Licha ya kuvuliwa uanachama hivi karibuni diwani huyo alichaguliwa kuwa Meya wa Manispaa ya Ilemela baada ya madiwani sita wa Chadema kususia uchaguzi wa Meya kati ya madiwani 14 wa manispaa hiyo.
Baada ya kuchaguliwa alisema yeye ni diwani wa Chadema na kwamba hakubaliani na uamuzi wa watu wachache ya kumvua uanachama wasiojali uamuzi wa wengi waliomchagua kwa zaidi ya kura 200,000.
No comments:
Post a Comment