WASHINGTON, Marekani
NCHI ya Marekani imepinga uamuzi wa Israel kujenga nyumba 3,000 za walowezi Mashariki mwa Jerusalem pamoja na Ukingo wa Magharibi kwa madai kuwa unarudisha nyuma jitihada za amani.
Hillary Clinton |
NCHI ya Marekani imepinga uamuzi wa Israel kujenga nyumba 3,000 za walowezi Mashariki mwa Jerusalem pamoja na Ukingo wa Magharibi kwa madai kuwa unarudisha nyuma jitihada za amani.
Kwa mujibu wa Waziri wa nchi hiyo, Hillary Clinton
alisema kuwa hatua hiyo itakuwa ikirudisha nyuma maendeleo ya nchi hiyo
pamoja na jitihada ambazo zinafanywa katika kuleta amani.
"Naomba niseme kwamba utawala huu, ni kama tawala
zilizotangulia na umeweka bayana kwa Israel haiwezi kuendelea na ujenzi
huo kwa kuwa shughuli hizo zinarudisha nyuma jitihada za majadiliano
ya amani," alisema Clinton.
Clinton alisema hayo mbele ya hadhira alipokuwa
akizungumza katika jukwaa lililoandaliwa na kituo cha sera za Mashariki
iliyowajumuisha mawaziri mbalimbali akiwemo Waziri wa Mambo ya Kigeni
wa Israel, Avigdor Lieberman pamoja na Waziri wa Ulinzi, Ehud Barak.
Pia Clinton alisema kuwa suluhisho la kudumu la
mgogoro wa Gaza lingekuwa ni miongoni mwa mipango mizuri ya kuleta
amani kati ya Israel na Wapalestina wote.
Utawala wa Rais Barack Obama ulijaribu kuzuia
shinikizo la Palestina la kutambuliwa na Umoja wa Mataifa, kwa madai
kuwa hatua hiyo imekuwa ni kizingiti kikubwa katika amani na kwamba
taifa la Palestina lingetokana kwa kuwepo na mazungumzo na Israel.
Hata hivyo, Clinton alisema kuwa pande zote mbili
zinapaswa kufanya kazi kwa pamoja ili kutafuta njia ya kusonga mbele
katika mazungumzo ambayo ndiyo yataleta suluhisho la mataifa mawili.
Aliongeza kuwa pande mbili zitakapokuwa tayari
kushiriki katika mazungumzo na Rais Obama pia atakuwa tayari
kushirikiana nao kikamilifu.
Kwa upande wa msemaji wa Bazara la Taifa la
Usalama, Tommy Vietor alisema kuwa vitendo hivyo haviwezi kuleta manufaa
yoyote katika meza ya mazungumzo na kuongeza kuwa Marekani inarejea
upinzani wake wa muda mrefu dhidi ya makazi ya walowezi, pamoja na
ujenzi Mashariki mwa Jerusalem.
"Tunaamini vitendo hivi havileti manufaa yoyote zaidi ya kuhujumu jitihada za kurudi kwenye meza ya mazungumzo," alisema Vietor.
"Tunaamini vitendo hivi havileti manufaa yoyote zaidi ya kuhujumu jitihada za kurudi kwenye meza ya mazungumzo," alisema Vietor.
Taarifa za vyombo vya habari zilisema kuwa baadhi
ya ujenzi wa Israel utafanyika katika eneo linalogombaniwa lililopo
katika Ukingo wa Magharibi maarufu kama E1, ambalo linapita kati ya
upande wa mwisho wa Mashariki ya eneo lililotekwa la Jerusalem
mashariki, na makazi ya Maaleh Adumim.
Vilevile Chama cha Ukombozi wa Palestina (PLO), kimelaani hatua hiyo na kusema ni uvamizi dhidi ya taifa hilo.
Wapalestina wanapinga kwa nguvu zote, mradi wa E1
kwa sababu unaligawanya eneo la Ukingo wa Magharibi katika vipande
viwili - Kaskazini na Kusini, hatua ambayo inafanya uundwaji wa taifa la
Palestina kuwa mgumu.
No comments:
Post a Comment