Thursday, December 6, 2012

Jeshi lawatimua waandamanaji Misri

Jeshi latumia vifaru kuwafurusha waandamanaji kutoka Tahrir
Wanajeshi nchini Misri wameanza kuwaondoa watu kutoka katika eneo la ikulu ya rais mjini Cairo ambako kumekuwa na makabliano makali kati ya wafuasi na wapinzani wa rais Mohammed Morsi
Limetuma vifaru na magari mengine yaliyo hamiwa kwa silaha nje ya kasri la rais baada ya mapigano ya usiku kucha kati ya wafuasi na wapinzani wa rais Mohammed Morsi.
Walioshuhudia matukio wanasema kuwa waandamanaji wameanza kuondoka kutoka eneo hilo.
Makabiliano yamesababisha vifo vya watu watano na wengine zaidi ya mia sita wakijeruhiwa.
Taarifa za televisheini ya taifa zinasema kuwa rais Morsi atatoa hutuba kwa taifa baadaye leo.
Mamlaka kuu ya waisilamu, Al-Azhar,imemtaka rais kufutilia mbali mamlaka aliyojilimbikizia.
Viongozi wa upinzani wameitisha maandamano zaidi hii leo kupinga hatua ya rais kujipa mamlaka zaidi pamoja na kuipinga rasimu ya katiba mpya inayotarajiwa kupigiwa kura tarehe 15 mwezi huu.
Pande hizo mbili zilitumia mawe, na mabomu ya petroli kushambuliana baada ya wafuasi wa rais kujaribu kulitawanya kundi la upinzani lililokuwa likiandamana nje ya kasri la rais.
Upinzani umeshutumu chama cha Muslim Brotherhood kupanga mashambulio hilo Vurugu hizo zilisambaa katika maeneo mengine ya nchi hiyo huku ofisi za Muslim Brotherhood zikishambulia katika miji ya Ismailia na Suez.
Washauri wanne wa rais Morsi wamejiuzulu.
Upinzani unasema upo tayari kwa mazungumzo iwapo Morsi atasitisha agizo linalompa mamlaka mpaya ya zaidi na iwapo ataahirisha kura ya maoni ya kielelezo cha katiba
chanzo-bbc.com.

No comments:

Post a Comment