Ni baada ya kulipukiwa na bomu la kutupwa kwa
mkono wakati walipokuwa wakichezea Bomu hilo lililookotwa kwenye vyuma
chakavu na kudhani kuwa ni mpira.
Tukio hilo lilitokea Jumatano majira
ya asubuhi huko Wilayani Karagwe mkoani Kagera Magharibi mwa Tanzania
wakati watoto walipokuwa wakichezea kitu mfano wa mpira mdogo ,ambacho
baadaye kilikuja kutambulika kuwa lilikuwa Bomu la kurushwa kwa mkono.
Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC mjini Dar es
Salama, Eric David Nampesya , mkuu wa Wilaya wa Karagwe Bi Darli
Rwegasira amesema kuwa watoto hao walilipukiwa na Bomu hilo ambapo
watatu kati yao walikufa papo hapo huku wawili wakifia hospitalini.
Kwa Mujibu wa Mkuu huyo wa Wilaya, awali mzazi
wa watoto hao amekiri kuwa aliliona bomu nyumbani kwake hapo juzi ambapo
watoto wake walikuja nalo baada ya kuliokota huku wakidhani kuwa ni
mpira.
Naye Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Philipo
Kalangi alisema kuwa utafiti waliofanya umeonyesha kuwa Bomu hilo
lililookotwa na kijana mmoja ambaye alikuwa akikusanya vyuma chakavu kwa
lengo la kuviuza hapo wilayani karagwe.
Bomu hilo lilikuwa mojawapo katika vyuma
alivyokuwa ameokota na baadaye watoto hao walienda kulichezea nyumbani
kwao na hatimaye kusababisha maafa hayo.
Mkuu huyo wa Polisi mkoani Kagera alidokeza kuwa
uchunguzi unaendelea ili kujua kwa undani Bomu hilo lilitokea wapi na
iwapo kama kuna mabomu mengine yanayoweza kuwa yamebaki katika maeneo
mbali mbali hapo Wilayani Karagwe.
Mkuu huyo wa Polisi hakuweza kukiri wala kukana
moja kwa moja kuhusisha Bomu hilo Kama matokeo ya uwepo wa wakimbizi wa
Rwanda waliowahi kuishi Wilayani hapo mwaka 1994 baada ya mauaji ya
kimbari nchini Rwanda ambapo Wilaya ya Karagwe ni moja ya wilaya
zilizopokea wakimbizi wengi kutoka nchini Rwanda.
Uchunguzi zaidi unaendelea huku ukiwahusisha wataalam wa milipuko kutoka Polisi na jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
source bbc.com
No comments:
Post a Comment