Friday, October 12, 2012

Baraza la Waislamu nchini Uingereza, Muslim Council of Britain, limesema ikiwa wachezaji wa Kiislamu wasivae jezi za wazamini wapya wa Newcastle sababu wanatoza riba na uislamu hauruhusu riba


Demba Ba
                             Demba ni kati ya wachezaji waislamu katika klabu ya Newcastle
Klabu ya Newcastle siku ya Jumanne ilitangaza kwamba itapata pauni milioni 24 kutoka kwa wadhamini wapya, kupitia kuvaa mavazi yao, kampuni inayotoa mikopo ya Wonga, lakini Baraza la Waislamu nchini Uingereza, Muslim Council of Britain, limesema ikiwa wachezaji wa Kiislamu watavaa mavazi hayo, hilo litakuwa ni kinyume cha sharia kulingana na dini.
Baadhi ya watu wamelalamika kuhusiana na klabu kutia saini mkataba wa muda mfupi na kampuni hiyo ya Wonga, na sasa Baraza la Waislamu nchini Uingereza, MSB, limeingilia kati suala hilo.
Mkataba huo na Wonga ni wa miaka minne.
Wachezaji wanne ambao ni waislamu walishiriki katika mechi dhidi ya wageni Manchester United siku ya Jumapili, mechi ya ligi kuu ya Premier; Demba Ba, Papiss Cisse, Cheick Tiote na Hatem Ben Arfa – na wote wamehimizwa kuelezea msimamo wao.
Sheikh Ibrahim Mogra, naibu wa katibu mkuu wa MCB amesema: "Kuna masuala mawili katika hili. Kuna kanuni za dini katika suala hili, na vile vile kuna uamuzi wa mtu binafsi, na kuzingatia au kutozingatia kanuni hiyo.
"Nia ni kuwalinda wale ambao ni dhaifu na huenda wakakandamizwa na kutumiwa na wenye mamlaka na matajiri.
"Wakati wanapotoa mikopo na kutoza kiasi kikubwa cha riba, hilo linamaanisha maskini hunufaika kwa muda mfupi kutokana na mkopo, lakini matatizo ya baadaye ni ya muda mrefu wanaposhindwa kulipa mikopo, kwa kuwa huwa ni vigumu kuendelea kuwaza kulipa riba hiyo."
Aliongezea: "Mfumo wa Kiislamu huepuka kuzingatia kunfuaika kwa kutoza riba."
Klabu kimekuwa kikijaribu kukwepa shinikizo hizo, na baada ya mkataba huo, kimetangaza kwamba kitabadilisha jina la uwanja wake kutoka Sports Direct Arena, na kulitumia jina la zamani la St James' Park.
Hata hivyo wengi wameendelea kukilaumu klabu kwa kukubali kutia saini mkataba na kampuni ya Wonga, na wamekuwa wakielezea namna wameudhika, hasa kupitia mitandao mbalimbali ya jamii.

No comments:

Post a Comment