Mechi ya kufuzu kwa kombe la
mataifa bingwa barani Afrika kati ya Senegal an ivory Coast ilisitishwa
baada ya mashabiki wa sokar kuzua ghasia wakati wa mechi hiyo mjini
Dakar.
Mashabiki hao wa Senegal, waliwasha moto na
kuanza kurusha mawe uwanjani wakati Ivory Coast, ilikuwa ikiongoza kwa
mabao mawili kwa bila, matokeo ambayo yangeliondoa timu hiyo kwa fainali
hizo zitakazo anadaliwa nchiniu Afrika Kusini.Mashabiki wa Ivory coast, walilazimika kuingia uwanjani ili kukwepa ghasia hizo.
Wachezaji na mashabiki hao wa Ivory Coast walizindikizwa na maafisa wa polisi wa kupambana na ghasia ambao walirusha vitoa machozi ili kuwatawanya mashabiki wa Senegal.
Ripoti zinasema watu kumi akiwemo waziri wa michezo wa Senegal, Hadhi Malick Gakou, walijeruhiwa kwenye rapsha hizo zilizotokea katika uwanja wa Stade Leopold Sedar Senghor.
Ghasia hizo zilianza wakati mshambulizi nyota wa Ivory Coast, Didier Drogba, alipofunga bao lake la pili kupitia mkwaju wa penalti huku dakika kumi na tano pekee zikiwa zimesalia kabla ya mechi hiyo kumalizika.
Shirikisho la mchezo wa Soka Barani Afrika CAF halijatoa taarifa yoyote kuhusiana na tukio hilo, lakini maafisa wa shirikisho la mchezo wa soka nchini humo, wamesema, timu hiyo ya Senegal huenda ikaadhibiwa vikali na CAF.
No comments:
Post a Comment