KIONGOZI wa Kanisa la Maombezi la GRC na Ubungo, Dar es Salaam, Mchungaji Antony Lusekelo amewataka viongozi wa dini na Watanzania kwa jumla, kutambua kuwa Tanzania ni bora kuliko dini zao.
Mchungaji Lusekelo pia aliwataka viongozi wa dini
kuendeleza vita dhidi ya rushwa huku akisema watoa rushwa na wapokeaji,
wamejificha makanisani na kwenye misikiti.
Alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam,
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema viongozi wa
dini lazima lazima washiriki katika mapambano ya rushwa bila woga.
Katika mazungumzo hayo, mchungaji huyo pia
alisema Serikali inapaswa kuwajibika kwa kutumia nguvu zake za kisheria
katika kulinda amani, huku akinyoshea kidole tukio la hivi karibuni
lililoashira kuvunja kwa amani, huku Serikali ikiwa haijachukua hatua.
Alisema hilo ni tatizo kubwa na kwamba ni watu wengi wakiwamo viongozi wa dini kushindwa kusema ukweli kwa kuogopa maisha yao kuwa mafupi.
Alisema hilo ni tatizo kubwa na kwamba ni watu wengi wakiwamo viongozi wa dini kushindwa kusema ukweli kwa kuogopa maisha yao kuwa mafupi.
“Ni muhimu kila mwananchi kutambua kuwa Tanzania
ni bora kuliko Ukristo na Uislamu. Watu wengi wanaogopa kusema ukweli.
Hata viongozi wa dini kwani watoa rushwa wamejificha misikitini na
makanisani, tuendeleze mapambano dhidi ya rushwa ipo siku tutashinda,”
alisema.
Kuhusu vurugu nchini, alisema chanzo ni viongozi wa dini kuhubiri siasa za chuki misikitini na makanisani.
“Vurugu siyo asili ya binadamu inatengenezwa,
Serikali ina wajibu wa kutumia nguvu yake kisheria kuilinda amani na
amani haishuki kutoka mbinguni au kwa maombi, inatengenezwa pia. Tatizo
cheche za kidini zilipoanza hazikudhibitiwa. Serikali ilikuwepo, aidha
kwa makusudi au bahati mbaya imelea cheche hizo,” alisema Lusekelo.
Lusekelo maarufu kama mzee wa Upako alisema watu o wanataka nchi isikae kwa amani na kuandaa mazingira ya watu kukosea.
No comments:
Post a Comment