Mpango huo ulitangazwa katika mkutano wa nchi za
Jumuiya ya Ulaya mjini Brussels, huku chombo hicho cha usimamizi
kikitarajiwa kuanza kazi rasmi mwaka ujao.
Inaonekana ni makubaliano kati ya Ufaransa na Ujerumani ambazo awali zilipingana juu ya muda na idadi ya benki chombo hicho kimoja kitachozisimamia.
Akizungumza katika mkutano huo rais wa Ufaransa, Francois Hollande, amesema ni jambo muhimu kuwa wameafikiana tarehe maalum kuhakikisha mfumo wa sheria unawekwa kwa ajili ya mpango huo.
Bwana Hollande pia amesema kazi zaidi inahitajika kufanyika kabla chombo cha usimamizi hakijaanza kutoa msaada kwa mabenki hapo mwaka kesho.
habari zaidi kuhusu umoja huu zitakujia baadae

No comments:
Post a Comment