Kutokana na kuenea kwa taarifa
kwamba katika baadhi ya Misikiti jijini Dar es salaam kumehifadhiwa
silaha mbalimbali zinazotarajiwa kutumika kwenye maandamano ya waumini
wa dini ya kiislamu watakaoandamana ijumaa novemba 2, Mkuu wa mkoa wa
Dar es salaam Said Meck Sadick amesema Jeshi la polisi linazo taarifa na
limejipanga.
Namkariri mkuu wa mkoa akisema
“ninawataka wala siwaombi, waache utaratibu wao huo kama ni kweli hayo
yanayoelezwa lakini nasema sisi kwa utaratibu wa kiserekali hatujapata
hilo tishio lakini kama kuna mtu yeyote mwenye nia hiyo ya kuhamasisha
watu waende na mapanga, anachezea moto… serikali kupitia vyombo vyake
vya ulinzi na usalama vitakabiliana na hali yoyote na mtu yeyote
atakaekuja na kitisho cha aina yoyote”
Mkuu huyo amesema maandamano
hayo ambayo yanahamasishwa kupitia vipeperushi ambavyo vimetolewa na
jumuiya na Taasisi za kiislam nchini ni batili hivyo polisi wamejipanga
kwa atakaejitokeza.
Sadick amesema pia kwamba
sababu zote zilizotolewa na jumuiya na taasisi hizo zimefanyiwa kazi
ikiwemo ile ya kumchukulia hatua kijana anaedaiwa kudhalilisha kitabu
cha dini hiyo pamoja na kukamatwa kwa watu wote waliohusika na vurugu
zilizotokea katika baadhi ya maeneo Dar es salaam.
Maandamano ya sasa yamepangwa
kufanyika ijumaa hii baada ya swala ya ijumaa Dar es salaam ambapo
yamepangwa kuelekea kwenye ofisi ya Waziri mkuu na mikoani ni kwenye ofisi za Wakuu wa mikoa.
No comments:
Post a Comment