Wednesday, October 31, 2012

Kimbunga Sandy chapunguza kasi ,chaitia hasara marekani cha mamilioni ya dollar



        Baadhi ya athari za kimbunga Sandy nchini Marekani
Biashara na huduma nyinginezo zinatarajiwa kurejea katika hali ya kaiwaida hii leo baada ya siku mbili za kufungwa kufuatia kimbunga kilichopiga Kaskazini Mashariki mwa Marekani.
Baadhi ya viwanja vya ndege, majengo ya serikali, shule na hata soko la hisa la New York, zilifunga shughuli zao
Maelfu ya watu katika eneo la kaskazini mashrikiwamo katika kumbi za shule tofauti kwa usiku wa pili na katika hifadhi nyengine za dharura baada ya makaazi yao kuathirika na mafuriko kutokana na kimbunga kibaya kuwahi kutokea katika eneo hilo kwa miongo kadhaa.
Kimbunga hicho kimesababisha vifo vya zaidi ya watu arobaini, miongoni mwao watu kumi na nane kutoka jimbo la New York.
Zaidi ya nyumba milioni nane na maeneo ya kibiashara katika majimbo kumi na saba yamo gizani kwa kukosa huduma ya nguvu za umeme.
Usafiri umetatizika pakubwa na usafiri wa chini ya ardhi wa treni mjini New York huenda usifunguliwe kwa siku kadhaa zijazo.
Rais Obama anatarajiwa kuzuru majimbo yalioathirika zaidi kama vile New Jersey,baadaye hii leo. Kimbunga hicho kimepungua kasi lakini wataalmau wanaonya kuwa shughuli ya kusafisha miji huendna ikachukua muda.
chanzo bbc.com

No comments:

Post a Comment