Waipa siku saba serikali kuwaachia watuhumiwa,waliochoma makanisa
JUMUIYA na Taasisi za Kiislamu nchini, zimeipa serikali siku saba
kuwapa dhamana watuhumiwa wa Kiislamu wanaoshikiliwa kutokana na vurugu
zilizotokea hivi karibuni maeneo ya Mbagala, jijini Dar es Salaam, na
kusababisha makanisa kuchomwa moto na kuharibu mali nyingine kadhaa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika hoteli ya Lamada,
Katibu wa Jumiya hiyo, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema Waislam hao
wanapaswa kupewa dhamana kwa kuwa ni haki yao kisheria.
Ponda alisema endapo siku hizo zitaisha bila kupewa haki hiyo watatangaza nini watakifanya ili kuondoa ukandamizaji huo.
Alisema katika vurugu zile waliokamatwa wengi ni Waislamu huku hoja
ya kuwanyima dhamana ikiwa ni suala la kuharibiwa makanisa ambayo
imechukuliwa kuwa ni ya kitaifa.
Tabia hiyo ya viongozi wa serikali kuyafanya mambo ya kanisa kuwa ya
kitaifa na kudharau Waislamu na haki zao, Sheikh Ponda alisema ndiko
kunakochangia kuligawa taifa katika misingi ya udini.
Sambamba na hilo pia waliitaka serikali kutoa tamko rasmi la kulaani
kukojolea Kuran na kuongeza kwamba lile alilolitoa Rais Jakaya Kikwete
katika kilele cha mbio za Mwenge hawalitambui na wala halitoshi kutokana
na ukubwa wa tukio lenyewe.
Wasikitishwa JK kutotembelea misikiti
Jumuiya hiyo pia imesikitishwa na kitendo cha Rais kwenda kutembelea
makanisa tu wakati vurugu hizo pia zilisababisha baadhi ya misikiti
kuchomewa makapeti kwa mabomu yaliyokuwa yanarushwa na Jeshi la Polisi
na watu kujeruhiwa.
“Rais alipofanya ziara katika kanisa la Zakiem alipita mita tatu
jirani na msikiti wa Hijra ambapo makapeti yake mpaka tunakwenda
mitamboni yameloa damu kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na polisi
waliokuwa wakilinda doria katika kanisa hilo, alisema.
Waislamu hawajahusika na uvunjaji wa makanisa
Katika hatua nyingine Sheikh Ponda alisema Waislam hawajahusika na
uvunjwaji wala uchomaji wa makanisa na kueleza vurugu zilitokea siku
ambayo Waislam walikusanyika kwa wingi katika msikiti maalum kwa ajili
ya ibada ya sala ya Ijumaa.
Alisema polisi walikuwa na upande katika tukio hilo kwani misikiti ya
Ijumaa ilianza kuzingirwa mapema kuanzia majira ya saa 4:00 asubuhi na
ilipofika majira ya saa 6:00 mchana baadhi ya misikiti ikiwemo ile
iliyoko umbali wa kilometa mbili kutoka kituo cha polisi Maturubai,
ilianza kushambuliwa kwa mabomu.
Wakati wa mashambulizi hayo, Ponda anadai makanisa yalionekana kupewa
ulinzi wa amani huku misikiti ikipelekewa vikosi vya kushambuliwa.
Hata hivyo ilipotimu majira ya saa 9:00 alasiri alidai alifika mmoja
wa maafisa kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ambaye aliwahoji
masheikh waliokuwepo eneo la Maturabai na kutaka kujua ni kwa nini
hawashiriki katika kusaidia kutuliza vurugu zinazoendelea kati ya
polisi na Waislamu.
Baada ya kuwepo kwa mvutano wa muda mrefu kati ya Kamanda wa Polisi wa
Temeke, Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Maturubai, masheikh hao na
Waislamu waliofika kituo cha polisi cha Maturabai ili kushinikiza
kufikishwa mahakamani kwa mtuhumiwa aliyekojelea Kuran, muafaka ulikuwa
ni masheikh kwenda viwanja vya Zakiem kwa lengo la kuwatuliza waumini
wao.
Huku pendekezo la pili likiwa ni la Waislam wote waliokamatwa watolewe
mahabusu na la tatu ni polisi kutoa gari na vipaza sauti kwa masheikh
ambapo hilo la kuzungumza na waumini lilikamilika kwa msaada wa Kituo
cha Sheria na Haki za Binadamu ambao walitoa msaada wa gari kwa
masheikh.
“Kilichotokea baada ya masheikh kuondoka na waumini walijikuta
wakishikiliwa na polisi kwa tuhuma za kufanya vurugu ambapo polisi
walimwagwa mitaani na kuwakamata watu wasiokuwa na hatia, ukamataji
uliohusisha kuhojiwa watu majina, kuandamwa kwa mbio mtu aliyevaa kanzu,
kofia na kuachwa aliyevaa msalaba akikatiza katikati ya askari na
hatimaye matumizi ya nguvu kubwa kwa aliyekamatwa.
“Hatua hii ndiyo iliyopelekea kukamatwa kwa watuhumiwa wengi waliokuwa
mikononi mwa polisi mpaka leo na ndiyo iliyochochea vurugu
zilizosambaa mitaani,” alisema Sheikh Ponda.
No comments:
Post a Comment