

Mwenyekiti
wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh Freeman Mbowe
akihutubia wananchi wa Kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha jana
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh Freeman
Mbowe akihutubia wananchi wa Kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha jana
katika muendelezo wa kampeni za chama chake kuwania nafasi ya uwakilishi
katika Halmashauri ya Jiji kupitia Kata hiyo. Mkutano huo nusura
usifanyike hiyo jana baada ya kilichoelezwa kuwa chama hicho kilikosa
eneo la kufanyia mkutano na hivyo kulazimiaka kufanyia nje ya ofisi za
chama hicho Kata ya Daraja Mbili, ofisi ambazo ziko jirani na za
mahasimu wao kisiasa, CCM.
Aidha, ujio wa Mbowe haukujulikana mapema kiasi cha wananchi kushangaa
kumuona jukwaani ghafla tu. Pia, Mh Mbowe hakuweza kumnadi mgombea wa
chama hicho kwa kuelezwa kwamba alikuwa anashikiliwa na Polisi
alikolazwa hospitali ya Mt Meru na hivyo kushindwa kuhudhuria mkutano
huo.
Godbless Lema nae akizungumza mkutanoni hapo.
Sehemu
ya umati wa watu uliojitokeza kusikiliza hotuba za viongozi wa Chadema.
Katika mkutano huo, zaidi ya sh laki 3 zilichangwa na wananchi hao
kusaidia kampeni zaidi za chama hicho katika Kata hiyo.
No comments:
Post a Comment