Uganda imeadhimisha
miaka hamsini ya uhuru wake huku wakuu kadhaa wa mataifa ya Afrika
wakiungana na Rais Yoweri Museveni katika sherehe hizo mjini Kampala.
Wadadisi wanasema kuwa Rais Museveni aliyeingia
madarakani tangu mwaka 1986 ameiongoza nchi hiyo kwa kudumisha amani na
kuleta maenedeleo baada ya miaka mingi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe
na unyanyasaji.Lakini wakosoaji wake wanasema amekandamiza upinzani nchini humo.
Kiongozi wa upinzani Kizza Besigye aliyewekwa kizuizini mara mbili wiki iliyopita anamshutumu Rais Museveni kwa kuiangamiza nchi hiyo iliyojipatia uhuru wake toka kwa Waingereza.
Sherehe za leo zilihuduhuriwa na takriban viongozi 15 wa Afrika wakiwemo marais wa miaka mingi, Robert Mugabe wa Zimbabwe na Yahya Jammeh wa Gambia.
Museveni hajasema ikiwa atawania urais katika uchaguzi mkuu mwaka 2016, ingawa baadhi ya vigogo katika chama chake wanataka astaafu wakisema kuwa anapoendelea kusalia mamlakani, ndivyo chama tawala kinaendelea kupoteza ushawishi.
Kwa wanaharakati wa upinzani ,wasioona cha kusherehekea wanasema kuwa Museveni amekua mamlakani nusu ya miaka ambayo nchi hiyo imejitawala na hivyo wangetaka kutumia fursa hiii ya kusherehekea uhuru kumtaka aondoke mamlakani.
No comments:
Post a Comment