Monday, October 29, 2012

Panya SUA wahudumia hospitali 13

 
UNAPOINGIA katika kitengo cha Apopo kilichopo katika Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA), Morogoro macho yako yatalakiwa na  vizimba vilivyosheheni panya.
Pia utalakiwa na ukanda mwembamba  uliobeba makopo madogo madogo yaliyojazwa makohozi, ambayo baadaye unabaini kuwa ni ya binadamu.
Inaweza kuwa kama wengi wasivyotarajia, kumwona Osama bin Laden akimkumbatia Rais  Barack Obama wa Marekani, kwani kwa mtu anayefika eneo hilo bila kujua kinachoendelea, atachanganyikiwana hata kushindwa kuelewa uhusiano uliopo kati ya panya na makohozi ya binadamu.
Lakini, katika kitengo hicho cha Apopo (SUA), panya wana uhusiano wa karibu na makohozi kwani mnyama huyo  ana kazi kubwa iliyo ya kipekee ambayo ni kuyapima makohozi ya binadamu ili kubaini iwapo yana vijidudu vya Kifua Kikuu (TB) au la.
Panya huyo anadaiwa kuwa na uwezo wa kupima sampuli 140 za makohozi kwa dakika 15 tu, wakati mtaalamu wa maabara aliyebobea huweza kupima wagonjwa 25 kwa siku.
Lakini, ili aweze kuifanya kazi hiyo, panya hutakiwa kwanza kwenda shule.
Kama ambavyo binadamu husoma kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu, vivyo hivyo kwa panya hao. Hupatiwa mafunzo maalumu katika ngazi tofauti ili kufuzu  jinsi ya kubaini  vijidudu vya TB  katika makohozi.
Panya  hao ni wanaopatikana Afrika, ambao  ni wakubwa kisayansi huitwa ‘cricetomy  gambianus’
Kitengo cha Apopo kwa sasa kina aina hiyo ya panya wanaofikia 30, ambao wapo katika mafunzo maalumu kwa kazi hiyo.
Mkuu wa Mafunzo ya Panya Apopo, Peter Luanda anasema kuwa wanyama hao hupewa mafunzo kuanzia wanapokuwa na umri wa kuanzia wiki nne tangu kuzaliwa.
“Nia ya kuwapa mafunzo hayo wakiwa wadogo, ni kuwafanya wakariri kwa urahisi elimu wanayopewa na pia  ujuzi wao utumike kwa muda mrefu,” anasema Luanda.
Anasema kuwa panya hao wanaobaini TB hupatiwa mafunzo katika hatua  zisizozidi tano.
Luanda anaeleza kuwa kama ilivyokuwa kwa panya wa kutegua mabomu, panya wa TB huanza kupewa mafunzo ya kuwazoea wanadamu ‘socialization stage’ na hatua ya pili ni ya chakula na mlio.
Hatua ya chakula na mlio ni ya kuwazoesha panya kujua kuwa, kila wanaposikia mlio fulani hapo wanatakiwa kula.
“Tunawapa mazoezi kila siku asubuhi na mchana, lakini kwa mafunzo ya TB, panya hupewa zaidi tembe za vitamini, wakati wale wa mabomu wakipewa vyakula kama ndizi na karanga,” anasema

No comments:

Post a Comment