Friday, October 19, 2012

Sababu za Leo Waislam Kuandamana ni Kama Ifuatavyo-kwa Habari zaidi na Picha za Matukio gonga hapa.








 Siku Ya Jana Maandamano yalikuwa rasmi kwa ajili ya Kupinga kukamatwa kwa Katibu Wa Wanaharakati wa Kiislam Shekhe Ponda Issa Ponda ambapo walikuwa wakishinikiza Kuachiliwa kwa shekhe huyo aliyefikishwa Mahakami siku ya Jana. Leo Waumini hao walishinikiza Serikali kama Mpaka Mchana swala ya Ijumaa itakapokuwa inamalizika kama shekhe huyo hata achiliwa basi wataandamana Jiji zima kushinikiza kuachiliwa kwa shekhe huyo.

Mchana wa leo majira ya saa 6 Mkuu wa Mkoa wa Dar, aliutangazia uma kupitia Radio One kuwa Maandamano hayo hayana baraka za Serikali ni Batili, hivyo watu wasiandamane. Mara baada ya swala ya Ijumaa Waislam wakakaidi amri hiyo kwa kuandamana.

Hii ni wiki ya nne Waislam kuandama kila baada ya Swala ya Ijumaa, wiki iliyopita Waumini wa dini hiyo walichoma Makanisa Kadha wa Kadha kuonesha hasira zao za Kijana mwenye umri wa miaka 12 kukojolea kitabu chao Kitakatifu cha Quran.
Sababu za maandamano ya leo
 1. Quran Kukojolewa
2. Shekhe Ponda Kukamatwa.
3. Shekhe Faridi ajulikani alipo huko Zanzibar.

4. Waislam Kuonewa na Kuteswa kwa sababu ya Mbagala
5. Akina mama Wa Kiislam Kudhalilishwa wakati wa Kichapo Mbagala.
6. Msikiti Umepigwa Bomu la Machozi mbagala.
7. Askari wameingia na Viatu Msikitini.
8. Rais amewapa pole Wakristo.
9. Maaskofu kuwapongeza Polisi Kuwakamata Waislam na kuwaweka ndani.
 
 
 
 
 
 

jwtz wakihakikisha usalama mitaani leo jijini dar
mitaa ya kariakoo vijana wakiingia kazini
Add caption

 waandamanaji wakiwa katika kukabiliana na askari wa kutuliza ghasia 
             


No comments:

Post a Comment