Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, imezindua ofa ya kuongea bure mara
tano ya wastani wa matumizi ya kupiga simu kwa siku nzima, kwa wateja
wake nchini
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa
Kampuni hiyo, Sam Elangalloor, alisema wametoa ofa hiyo kwa wateja wao
kwa wastani wa kiwango cha fedha watakayotumia kila siku.
Alisema wateja watatumia bonasi hiyo ya muda wa maongezi,kupiga simu kwenda mtandao wowote kwa siku hiyo.
”Tumefanya
hivi ili kuendelea kuboresha huduma zetu na pia kuendelea kudhibitisha
dhamira yetu ya kuwapatia wateja wetu nchini nzima, uhuru wa kuongea,”
alisema Elangalloor.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni hiyo,
Beatrice Singano, alisema mteja anayetumia mtandao huo ameshaunganishwa
katika bonasi hiyo na kwamba kinachotakiwa ni kupiga simu ili apate
salio la bure mara tano kwa wastani wa matumizi yake.
“Kadri mteja
anavyotumia simu yake kwa kupiga simu, ndivyo atakavyojipatia nafasi
zaidi ya kuzawadiwa asilimia 500 ya bonasi ya muda wa maongezi
bure,”alisema.
“Mfano mteja anaweka vocha ya Sh 500 kwa siku
nzima, hivyo akatumia na kuisha saa 6:00 mchana muda huo atapewa bonasi
ya maongezi ya bure ambayo itakuwa mara tano ambapo ataongezewa salio la
Sh2,500 litakalotumika siku hiyo kabla ya saa 6 usiku”alisema Singano
No comments:
Post a Comment