SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limemteua mshambuliaji wa TP Mazembe na
Tanzania, Mbwana Samata kuwa miongoni mwa nyota 32 watakaowania tuzo ya
mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani ya Afrika.Hii
ni mara ya kwanza kwa mchezaji wa Tanzania kuingia kwenye orodha hiyo ya
wachezaji wanaowania tuzo ya Afrika kwa wachezaji wa ndani.Katika
taarifa iliyotolewa mwishoni mwa wiki na CAF, ilivitaja vigezo
vilivyotumika kumjumuisha Samata kwenye orodha yake kuwa ni mchezaji
kijana aliyeibuka na kuwa nyota katika kikosi cha TP Mazembe tangu
alipojiunga nayo mwaka 2011
Pia, lilimtaja Samata kama miongoni
mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha TP Mazembe akiwa ameifungia
mabao sita katika mechi mbalimbali za michuano ya kimataifa.
Hivi
karibuni Samata aliingia kwenye orodha ya wafungaji bora 71, duniani
sambamba na Lionel Messi, Neymar na Cristiano Ronaldo.Mbali ya
Samata, TP Mazembe imefanikiwa kuingiza jumla ya wanandinga watano
kwenye kinyang'anyiro hicho cha kumsaka mwanasoka bora wa Afrika kwa
wachezaji wa ndani.Wengine ni mshambuliaji raia wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC), Tresor Mputu, beki Stoppila Sunzu, kiungo
Rainford Kalaba na mshambuliaji Given Singuluma wote raia wa Zambia.
Orodha
kamili ya nyota 32 wanaowania tuzo hiyo na klabu zao na nchi wanazotoka
ni Mbwana Samata (TP Mazembe, Tanzania), Abdelmoumen Djabou (Club
Africain, Algeria), Ahmed El-basha(Al-Merreikh, Sudan), Ahmed Zuway (CA
Bibertin, Lybia), Abdoulrazak Fiston (Lydia Adacademic, Burundi), Alou
Bagayok (Djoliba, Mali), Moxolisi Mthethwa (Royal Leopard, Swaziland) na
Oboaboa Godfrey (Sunshine Stars, Nigeria).Pia yupo Alula Girma
(St George, Ethiopia), Azuka Boko Izu (Sunshine Stars, Nigeria),
Boubacar Bangolula (Djoliba, Mali), Edward Sadomba (Al Hilal,
Zimbambwe), Essam El Hadary (El Merreikh, Misri), Emmanuel Clottey
(Esperance, Ghana), Given Singuluma (TP Mazembe, Zambia), Omar Mohamed
Bakheet(Al Hilal, Sudan), Rainford Kalaba (TP Mazembe, Zambia) na Razak
Yakubu (Al Ahly Shandy, Ghana).Wengine ni Amouda Ahmed Elbashir
(Al Ahly Shandy,Sudan), Arrison Affur (Esperance,Ghana), Ismailia Diara
(Cercle Olympique de Bamako,Mali), Joao Hernani (Interclub,Angola),
Mohamed Aboutreika (Al-Ahly,Misri), Mongezi Bobe (Black Leopards,Afrika
Kusini), Mudather El-Taieb (Al Hilal, Sudan) na Solomon Asante (Berekum
Chelsea, Ghana).Orodha hiyo inakamilishwa na Stopila Sunzu (TP
Mazembe, Zambia), Taboko Eric Nyemba (AC Leopard Dolisite, DRC Congo),
Tresor Mtupu (TP Mazembe, DRC Congo), Walid Hicheri (Esperance,
Tunisia), Yannick N'Djeng (Esperance,Cameroon) na Youssef Msakni
(Esperance, Tunisia).
No comments:
Post a Comment