Friday, October 5, 2012

Mashujaa wa Mau Mau kuishtaki Uingereza,Nashauri Tanzania iwashitaki Wajerumani Sababu walitutesa.


                                                 Mashujaa wa Mau Mau
Mahakama nchini Uingereza imeamua kuwa mashujaa wa Mau Mau walioishtaki serikali hiyo kwa mateso na dhulma wakati wa vita vya Mau Mau, wanaweza kuendelea na kesi ya kuitaka nchi hiyo kuwalipa fidia.
Jaji Richard McCombe, alisema kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuonyesha mateso yalitokea kwani serikali ya Uingereza wakati huo ilikuwa makini sana katika kuweka rekodi za yaliyotokea.
Serikali ya Uingereza imesema itakata rufaa. Katika taarifa ya wizara ya mambo ya nje nchini humo, watekelezaji wengi wa ukatili huo tayari wamekufa na kwa hivyo hakuna mashahidi wa kueleza kilichotokea.
Uamuzi huu wa kihistoria una maana kuwa watu wengine kama mashujaa hawa walioteswa na serikali za kikoloni wanaweza kudai fidia.
Wakenya hao wanadai waliteswa na kudhulumiwa na serikali ya ukoloni ya Uingereza katika miaka ya 1950, wakati wa harakati za kupigania uhuru wa taifa hilo.
Mnamo mwezi Julai, serikali ya Uingereza ilikiri kwa mara ya kwanza kwamba washukiwa wa vita vya Mau Mau waliteswa na hivyo Uingereza ikaomba radhi.
Mahakama hata hivyo itaamua ikiwa kesi itaendelea au iamrishe walipwe fidia.
Lakini mawakili wa serikali waliteta wanateta wakisema kuwa kesi ya haki haiwezi kutendeka kwa sababu matukio hayo yalitokea miaka ya hamsini.
Mapema mwaka huu, mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Askofu mkuu mstaafu Desmond Tutu, alimtumia ujumbe waziri mkuu David Cameron akimtuhumu kwa kujaribu kukwepa kuwajibika kisheria kwa makosa yaliyofanywa na wakoloni.
Nashauri kama hawa wakifanikiwa basi Tanzania tuwashitaki wajerumani waliowauwa na kuwatesa babu zetu wasio na hatia,na bila kuwasahau wale waarabu waliowachukuwa ndugu zetu katika biashara ya utumwa?

No comments:

Post a Comment