RATIBA ya Fainali za Afrika 2013 inatarajiwa kupangwa keshokutwa mjini Durban, Afrika Kusini, ambapo fainali hizo zitaanza Januari 19 mpaka Februari 10 na zitafanyika kwenye viwanja vya Soccer City, Mbombela, Nelson Mandela Bay, Royal Bafokeng na Moses Mabhida.
Mechi ya ufunguzi na fainali zitachezwa kwenye Uwanja wa Soccer City jijini Johannesburg.
Zifuatazo ni timu 16 zitakazoshiriki fainali hizo:
AFRIKA KUSINI
Imeshiriki fainali hizo mara 7 ambazo ni mwaka (1996, 1998, 2000, 2002, 2004, 2006, 2008).
Afrika Kusini ndiyo wenyeji wa Fainali za Afrika 2013. Mara ya mwisho Afrika Kusini imeshiriki fainali hizo ni 2008, ambapo tayari kocha wa Afrika Kusini, Gordon Igesund ametakiwa kuhakikisha timu hiyo inafika nusu fainali. Afrika Kusini imetwaa ubingwa wa Afrika mara 1 (1996).
GHANA
Ghana imeshiriki fainali za Afrika mara 18 ambazo ni mwaka (1963, 1965, 1968, 1970, 1978, 1980, 1982, 1984, 1992, 1994, 1996, 1998, 2000, 2002, 2006, 2008, 2010, 2012).
Mara ya mwisho Ghana imetwaa ubingwa wa Afrika ni mwaka 1982, lakini Ghana imetwaa ubingwa wa Afrika mara 4 (1963, 1965, 1978, 1982).
MALI
Mali imeshiriki fainali za Afrika mara 7 ambazo ni mwaka (1972, 1994, 2002, 2004, 2008, 2010, 2012).
Katika fainali za Afrika zilizofanyika mwanzoni mwa mwaka huu, Mali ilishika nafasi ya tatu. Haijatwaa Kombe la Afrika.
ZAMBIA
Mabingwa watetezi Zambia wameshiriki fainali za Afrika mara 15 ambazo ni mwaka (1974, 1978, 1982, 1986, 1990, 1992, 1994, 1996, 1998, 2000, 2002, 2006, 2008, 2010, 2012).
Zambia wana jukumu la kuonyesha hawakubahatisha kutwaa ubingwa wa Afrika mwanzoni mwa mwaka huu. Zambia imetwaa ubingwa wa Afrika mara 1(2012).
NIGERIA
Nigeria wameshiriki fainali za Afrika mara 16 ambazo ni mwaka (1963, 1976, 1978, 1980, 1982, 1984, 1988, 1990, 1992, 1994, 2000, 2002, 2004, 2006, 2008, 2010).
Katika miaka ya hivi karibuni Nigeria ilikuwa imepoteza nguvu katika soka la Afrika. Nigeria imetwaa ubingwa wa Afrika mara 2 (1980, 1994).
TUNISIA
Tunisia wameshiriki fainali za Afrika mara 15 ambazo ni mwaka (1962, 1963, 1965, 1978, 1982, 1994, 1996, 1998, 2000, 2002, 2004, 2006, 2008, 2010, 2012).
Hivi sasa kikosi cha Tunisia kinaundwa na vijana wengi bila wachezaji nyota kikitarajiwa kutoa ushindani wa hali ya juu. Tunisia imetwaa ubingwa wa Afrika mara 1 (2004).
IVORY COAST
Ivory Coast wameshiriki fainali za Afrika mara 19 ambazo ni mwaka (1965, 1968, 1970, 1974, 1980, 1984, 1986, 1988, 1990, 1992, 1994, 1996, 1998, 2000, 2002, 2006, 2008, 2010, 2012).
Hii ni nafasi ya mwisho kwa kizazi bora cha soka nchini Ivory Coast kujaribu bahati yao ya kutwaa ubingwa wa Afrika. Ivory Coast imetwaa ubingwa wa Afrika mara 1 (1992).
MOROCCO
Morocco wameshiriki fainali za Afrika mara 14 ambazo ni mwaka (1972, 1976, 1978, 1980, 1986, 1988, 1992, 1998, 2000, 2002, 2004, 2006, 2008, 2012).
Morocco hawakufanya vizuri katika fainali za mwaka huu, ila wanatarajiwa kutoa ushindani katika fainali za 2013. Morocco imetwaa ubingwa wa Afrika mara 1 (1976).
ETHIOPIA
Ethiopia wameshiriki fainali za Afrika mara 9 ambazo ni mwaka(1957, 1959, 1962, 1963, 1965, 1968, 1970, 1976, 1982).
Mara ya mwisho kwa Ethiopia kushiriki fainali za Afrika ilikuwa mwaka 1982. Hii ni kati ya timu za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati itakayoshiriki fainali za 2013. Ethiopia imetwaa ubingwa wa Afrika mara 1 (1962).
CAPE VERDE
Timu ya Cape Verde haijawahi kushiriki fainali za Afrika. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Cape Verde kushiriki fainali hizo za Afrika 2013. Vape Verde inaingia katika fainali hizo ikiwa imeitoa timu ngumu ya Cameroon. Haijatwa Kombe la Afrika.
ANGOLA
Angola wameshiriki fainali za Afrika mara 6 ambazo ni mwaka (1996, 1998, 2006, 2008, 2010, 2012). Katika miaka yote iliyoshiriki, mara nne imefika hatua ya nne bora, lakini imeshindwa kufika fainali au kutwaa ubingwa wa Afrika. Haijatwa Kombe la Afrika.
NIGER
Niger wameshiriki fainali za Afrika mara 1 ambayo ni mwaka (2012).
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Niger kushiriki fainali hizo za Afrika. Ni timu ambayo katika hatua ya kufuzu inafanya vizuri katika mechi zake zote za nyumbani. Haijatwa Kombe la Afrika.
TOGO
Togo wameshiriki fainali za Afrika mara 6 ambazo ni mwaka (1972, 1984, 1998, 2000, 2002, 2006).Togo baada ya kushambuliwa na waasi katika fainali za Afrika zilizofanyika huko Angola walijitoa katika fainali za 2010, lakini hivi sasa wamerudi tena na wanatarajiwa kutoa ushindani mkubwa. Haijatwa Kombe la Afrika.
DR CONGO
DR Congo wameshiriki fainali za Afrika mara 15 ambazo ni mwaka (1965, 1968, 1970, 1972, 1974, 1976, 1988, 1992, 1994, 1996, 1998, 2000, 2002, 2004, 2006).
DR Congo ilishindwa kushiriki fainali hizo kwa muda wa miaka saba, lakini hivi sasa wameingia katika fainali hizo na wanatarajiwa kutoa upinzani mkubwa. DR Congo imetwaa ubingwa wa Afrika mara 2 (1968, 1974).
BURKINA FASO
Burkina Faso wameshiriki fainali za Afrika mara 8 ambazo ni mwaka (1978, 1996, 1998, 2000, 2002, 2004, 2010, 2012).
Burkina Faso imekuwa ikishiriki fainali za Afrika, lakini haijawahi kufika hatua ya robo fainali. Haijatwa Kombe la Afrika.
ALGERIA
Algeria wameshiriki fainali za Afrika mara 14 ambazo ni mwaka (1968, 1980, 1982, 1984, 1986, 1988, 1990, 1992, 1996, 1998, 2000, 2002, 2004, 2010).
Kila mara Algeria imekuwa na kikosi bora, lakini ni mara moja tu katika fainali za Afrika imefika hatua ya nusu fainali. Algeria imetwaa ubingwa wa Afrika mara 1 (1990).
No comments:
Post a Comment