Wednesday, October 3, 2012

Kigoda, Sendeka, Karamagi washinda Nec

Vigogo kadhaa wameibuka na ushindi katika uchaguzi unaoendelea katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya wilaya.
Mkoani Kagera, Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, ameshinda kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) kupitia Wilaya ya Bukoba Vijijini.katika serikali ya awamu ya nne, Nazir Karamgi,jana alifanikiwa kurudishwa kwa wapiga kura wa wilaya ya bukoba Vijijini kwa kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM (NEC)akiwakilisha wilaya ya Bukoba Vijijini.
Karamagi alipata kura 779 huku akiwaacha wapinzani wake ambao ni Murshid Ngeze aliyambulia kura 252 na Joyce Justinian kura 37.
Kwa upande wa nafasi ya Mwekekiti wa CCM wa wilaya hiyo, Novatus Nkwama alichukua nafasi hiyo kwa kushinda jumla ya kura 645 na kumshinda  Sadru Nyangasha aliyekuwa anatetea nafasi yake kwa kupata kura 385.
Waziri wa viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda, amechaguliwa kuwa mjumbe wa Nec, baada ya kupata jumla ya kura 942, akiwabwaga, Juma Nkondo kura 75, Augastino Mwengele 61 na Hadija Masudi 27.Nafasi ya Uenyekiti ilikwenda kwa Athumani Malunda aliyepata kura 534.
Katika Wilaya ya Simanjiro, Mbunge wa jimbo hilo, Christopher Ole Sendeka, ameibuka na ushindi wa ujumbe wa Nec baada yakumshinda mpinzani wake, Justine Nyari. Sendeka alipata kura 471 na Nyari 126.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa wilaya, mshindi ni Broun Methius Ole Suye ambaye alipata kura 423 na dhidi ya mpinzani wake, Lengai Ole Makooo aliyepata kura 198.
 

No comments:

Post a Comment