ALIYEKUWA Mwasisi wa Chama cha Mageuzi ya Kitaifa
(NCCR-Mageuzi), Emmanuel Petro ole Sirikwa (70), amefariki dunia juzi
kwenye Hospitali ya AICC alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na maradhi ya
kiharusi.
Akizungumza na wandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Mussa Kombo Mussa, alisema wamepoteza mwanamageuzi wa kweli katika ulingo wa siasa nchini.
Akifafanua kuhusu nyadhifa alizoshika ndani ya chama, alisema aliwahi kuwa Kamishna mkoani Arusha na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa pia Mjumbe wa Baraza la Wadhamini.
Alikuwa mmoja wa waanzilishi wa NCCR– Mageuzi akiwa anamiliki kadi namba 03 ya uanachama.
Nafasi nyingine za uongozi alizowahi kushika ni Mwenyekiti wa Mkoa na mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa (kabla ya mabadiliko ya katiba).
“Kutokana na heshima na historia yake ndani ya chama, tumeamua kuenzi uvumilivu na misimamo yake kwa kuuita ukumbi wa mikutano wa chama chetu kuwa Sirikwa,” alisema.
Mussa alisema maziko yanatarajiwa kufanyika kijijini kwake Olijilah- Arumeru mkoani Arusha Jumatano.
Alisema chama kitawakilishwa na viongozi wakuu wakiongozwa na Mwenyekiri wa Taifa, James Mbatia.

No comments:
Post a Comment