Wachezaji
wa Kilimanjaro Stars wakisalimiana na wachezaji wa Somalia kabla ya
kuanza mchezo wa michuano ya Cecafa Challenge uliofanyika katika Uwanja
wa Lugogo nchini Uganda ambapo Tanzania ilishinda 7 – 0 Mrisho Ngasa
akifunga magoli matano na John Bocco mawili.
Mrisho
Ngasa wa Kilimanjaro Stars mwenye mpira akijaribu kuwatoka mabeki wa
timu ya Somalia wakati wa mchezo wa michuano ya Cecafa Challenge
uliochezwa katika Uwanja wa Lugogo nchini Uganda.
Beki
wa Kilimanjaro Stars, Erasto Nyoni akiambaa na mpira wakati wa mchezo
wa Cecafa Challenge dhidi ya timu ya Somalia uliochezwa katika Uwanja wa
Lugogo nchini Uganda.
Mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars Mrisho Ngassa akiambaa na mpira uliozaa goli la kwanza sekunde ya 48
Mrisho
Ngassa akishangilia moja ya goli kati ya matano aliyofunga wakati wa
mchezo na Somalia uliochezwa katika Uwanja wa Lugogo nchini Uganda
No comments:
Post a Comment