Habari zilizotufikia hivi punde kutoka Iringa zimeeleza kwamba vigogo hao wa Polisi na Mahakama walifika Mkoani Iringa mapema leo na Tangu wafike mara moja walianza harakati za Kumuomba Dr.slaa na Timu yake wakutane nao kwa ajili ya kikao cha dharua,
baadhi ya mambo waliozungumza ni pamoja na kifo na mazishi ya mwandishi wa habari aliyefariki jana katika mapigano kati ya polisi na wananchi,
Katika kikao hicho kilichoanza majira ya saa sita na kumalizika saa tis mchana huu pamoja na mambo mengine wamekubaliana kuahirisha shughuli za M4C hadi tarehe 9 ambambo shughuli za sensa zitzkuwa zimemalizika na taratibu za kumzika Marehemu Daudi zitakuwa zimekwisha.
Dr.slaa amesema wamekubaliana hayo na amemteua mjumbe wake mmoja pamoja na MANUMBA DCI,wayaweke makubaliano hayo katika maandishi ili wasijekugeukana baadae.
Kwa habari zaidi ungana nasi baadae....
No comments:
Post a Comment