ILI kuwaongezea wateja wake uwanja mpana wa kutumia mawasiliano ya simu,
Kampuni ya simu za Mkononi ya Tigo, imezindua kifaa maalum cha kuchaji
simu kinachotumia nishati ya jua.
Kifaa hicho kitawafanya
wananchi hasa wanaoishi vijijini ambako hakuna nishati ya umeme kuweza
kuchaji simu zao, hivyo kuongeza idadi ya watumiaji wa mawasiliano ya
simu nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam
jana, Ofisa Masoko wa Kampuni hiyo, Jaqulini Nnunuma alisema Tanzania
ina idadi kubwa ya watu ambao wanatumia simu za mikononi na asilimia 50
ni wateja wa tigo, hivyo wameamua kuanzisha vifaa vya nishati ya jua
vyenye uwezo wa kuchaji simu kwa lengo la kurahisisha huduma zao.
‘’Tanzania
ina idadi kubwa ya watu ambao hawana njia ya moja kwa moja ya kupata
umeme, hivyo leo tumeamua kuzindua rasmi kifaa maalum cha nishati ya jua
kwa ajili ya kuchaji simu za mikononi’’alisema Nnunduma.
Pia
aliongeza kuwa pamoja na kuwapa wateja nishati rafiki na endelevu kwa
matumizi ya kila siku, watakaonufaika na mradi huu ni wale wanaoendesha
maisha na biashara zao katika maeneo yasiyo na umeme .
‘’Kwa
kuwapa wateja wetu nishati rafiki na endelevu kwa matumizi ya kila siku
watakaonufaika na mradi huu ni wale wale wanaoishi na kuendesha
biashara zao katika maeneo yasiyo na umeme tu’’ aliongeza Nnunduma.
Naye
Meneja Miradi , Yaya Ndoje alisema kuwa watakaonufaika na huduma hiyo
endelevu kwa ajili ya kutoa huduma hiyo ya kusambaza vifaa hivyo ni
wale walio mawakala wa tigo tu, pamoja na wauzaji wa bidhaa za tigo kama
simu na chaji pekee katika mikoa yote nchini Tanzania Bara na Visiwani.
Aidha
aliongeza kuwa kwa kupitia vifaa vya nishati ya jua huduma hii bunifu
itarahisisha na kufanya na upatikanaji wa huduma ya tigo iwe rahisi
pamoja na kuongeza kipato ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma kwa
kipindi kwa wateja wetu.
No comments:
Post a Comment