Wednesday, November 28, 2012

‘SHARO MILIONEA HAKUFA’ ,ndivyo anavyodai msanii mwenzake

PENYE wengi hapokosi mengi, katika mazishi ya msanii nyota, Sharo Milionea yaliyofanyika jana Lusanga, Muheza, zilipenya mbegu mbaya za imani za kishirikina.
Msanii mmoja mkongwe ambaye Saluti5 haioni busara kulitaja jina lake, alithubutu kusema Sharo Milionea hakufariki bali amechukuliwa kama msukule.
“Sina la kufanya kwa kuwa mimi si mwanafamilia lakini ndani ya nafsi yangu naamini Sharo hakufa, yupo hai amechukuliwa msukule” alisema msanii huyo.
Sharo Milionea alifariki Jumatatu usiku kwa ajali mbaya ya gari wakati akielekea kwao Lusanga kumsalimia mama yake mzazi.
chanzo- Saluti5

No comments:

Post a Comment