Friday, November 30, 2012

Makaburi zaidi ya 100 yafukuliwa nchini Benin

                    Voodoo nchini Benin
Zaidi ya makaburi 100 yamefukuliwa katika eneo la makaburi karibu na mji mkuu wa Benin, Porto-Novo, polisi wamesema.
Wahalifu hao, waliofanya kitendo hicho, pia walivikata vichwa vya miili hiyo na kuiba baadhi ya viungo vyao vya ndani.
Mwandishi habari wa BBC Vincent Nnanna, aliyeko Benin, alisema inashukiwa kwamba uhalifu huo una uhusiano fulani na itikadi za kichawi zijulikanazo kama Voodoo, zinazotumia viungo vya miili ya wanadamu kama hirizi.
Hii ndiyo mara ya kwanza kwa kisa kama hiki kutokea nchini humo, ambapo Voodoo ni dini rasmi, Nnanna aliendelea kusema.
Kuna zaidi ya Voodoo 100 zinzaowakilisha maswala tofauti. Kwa mfano, Gou huwakilisha vita na masonara, na Sakpata huwakilisha ugonjwa, uponyaji na dunia.
Kuhuzunishwa
Mwandishi wetu anasema makaburi hayo yalipatikana na mwashi aliyekuwa amesahau ala zake za kazi katika eneo hilo la makaburi lililoko Dangbo, karibu na Porto-Novo.
Ndugu za maiti hao wamehuzunishwa sana kwa sababu wanaamini kwamba baada ya kufariki roho ya mtu huweza kuzaliwa tena katika kiumbe kingine. Wanahofia kwamba wapendwa wao watazaliwa upya pasipo na viungo vilivyibwa.
Kasisi mkuu wa Voodoo aliiaambia BBC kwamba visa kama hivyo havikubaliki katika imani hiyo – na akashutumu uhalifu huo.
Wafuasi wa Voodoo – ambao ni asilimia 40 ya idadi ya watu wote nchini Benin – wanaamini kwamba maisha yote huendeshwa na nguvu za pepo ya malihai kama maji, moto, dunia na hewa.

No comments:

Post a Comment