Saturday, November 17, 2012

Mtangazaji Fred Mtoi afariki dunia,ni Mtanzania

BBC inasikitika kutangaza kifo cha mtangazaji mwenzetu Fred Mtoi ambaye alifariki Ijumaa usiku mjini London.

Fredd Mtoi
Fred alianza kazi ya utangazaji katika Radio Tanzania kabla ya kuja Ulaya kwa mafunzo.
Amekuwa akifanya kazi huku akiendelea na masomo ya shahada ya pili ya masters kwenye digital media katika chuo kikuu kimoja cha London.
Alishiriki katika vipindi muhimu na vilivyopata sifa hasa vya sanaa, utamaduni na jamii kutokana na kuwafahamu wakaazi wengi wa London hasa wenye asili ya Afrika Mashariki.
Alishiriki piya katika matangazo ya kawaida ya habari ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC.
Wenzake katika Idhaa ya Kiswahili ya BBC wanamkumbuka Fred kuwa mtu mwema, mpole, mchangamfu na anayepatana na wote, na ambaye alikuwa mtangazaji tulivu na akishikilia kazi lazima ahakikishe kuwa ameimaliza vema iwezekanavyo.
Matayarisho yanafanywa kusafirisha mwili wake hadi Tanzania.
chanzo-bbc.com

No comments:

Post a Comment