Friday, November 16, 2012

CHADEMA yazoa wanachama 260

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimezoa wanachama 260 akiwemo aliyekuwa Mbunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Mpwapwa na Kongwa Gideon Senyagwa, pamoja na mwenyekiti na katibu wa chama hicho tawala.
Mbunge huyo aliyepewa Kadi Na. AO CDM 0101716 alihamia chama hicho Novemba 9, mwaka huu, pamoja na Mwenyekiti wa Tawi la Ngh’umbi, Boazi Madukani, katibu wa chama hicho Mbagilwa Festo kutoka Saigodi, na wanachama wengine 36.
Akizungumza katika mkutano uliofanyika Kibaigwa, Senyagwa alisema kuwa hawafurahishwi na vitendo vinavyofanywa na chama tawala ikiwa ni pamoja na kuharibiwa kwa mazao yao kutokana na kupitishwa kwa bomba la maji.
“Ni kweli nimehama chama hicho na kujiunga na CHADEMA kutokana na kuwepo kwa mmomonyoko wa maadili kutoka kwa baadhi ya viongozi huku wakipuuza kero za wananchi na kuwabeza waliotangulia.” alisema Senyagwa.
Alibeza uteuzi wa katibu mkuu wa chama hicho Philip Mangula ambaye amekumbukwa wakati chama hicho kimeshapoteza dira jambo linaloweza kumpa wakati mgumu

No comments:

Post a Comment