Wednesday, November 28, 2012

MAZISHI YA MSANII SHARO MILIONEA NI MAZISHI YA KIHISTORIA TANGA

INAAMINIKA kuwa mazishi ya Mchekeshaji na mwanamuziki, Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ hayajawahi kutokea mkoani Tanga.
Mzee Rajabu (mwenye kofia pichani juu) ni mmoja wa watu wanaomini hivyo, anasema tangu azaliwe hadi kufikia utu uzima alionao, hajawahi kushuhudia mazishi makubwa namna ile.
“Nashukru nimeishi miaka mingi na nimetembea sehemu kadhaa za nchi hii, lakini sijawahi kuhudhuria msiba wenye watu wengi kama waliojitokeza kuja kumzika kijana wetu”
“ Amezikwa na watu wengi sana tena wa kila aina inaonyesha kuwa ni mtu aliyeishi na watu vizuri alikuwa ni kijana mwema sana aliyependa wenzake,”anasema Babu huyo mkazi wa Lusanga, wilayani Muheza.
Sharo amepumzishwa jana kwenye nyumba yake ya milele katika makaburi ya familia yao kijijini Jibandeni, Lusanga. Umati mkubwa ulihudhuria mazishi yake na inakadiriwa zaidi ya nusu ya waliohudhuria, walitoka Dar es Salaam.
Kitu pekee ambacho unaweza kujifunza kwenye msiba huu ni kwamba WASANII ni watu wakubwa sana, labda hawajijui tu, ni watu wakubwa na mashuhuri pengine kuliko hata wanasiasa wakubwa.
CHANZO-SALUTI5

No comments:

Post a Comment