Wednesday, October 31, 2012

Yanga yaikamata Simba

WAKATI mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba waking’ang’aniwa kwa sare ya 1-1 na Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, watani zao Yanga walichanua Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya kuichapa Mgambo JKT kwa mabao 3-0 na kukabana kileleni zikipishana kwa tofauti ya mabao.
Simba iliyokuwa ikiongoza kwa pointi 22, ilijikuta ikianza kufungwa dakika ya 33, mfungaji akiwa Mokili Rambo ikiwa ni dakika tano tu tangu aingie kuchukua nafasi ya John Bosco, baada ya kuwatoka mabeki wa Simba. Matokeo hayo yalidumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili, Simba ilijitahidi kucharuka na kufanikiwa kuchomoa bao dakika ya 57, likifungwa na Amri Kiemba akiitendea haki kona ya Emmanuel Okwi. Hadi mpira unamalizika Simba na Polisi Moro ambao wanaburuza mkia katika msimamo wa ligi, walitoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1.
Akizungumza baada ya mchezo, Kocha wa Simba, Mserbia Milovan Cirkovic, alilia na refa kutotenda haki, huku akidai licha ya wachezaji wake kupata nafasi nyingi za kufunga, alionekana wazi kuibeba Polisi.
Kocha msaidizi wa Polisi, Ally Jangalu alisema mechi ilikuwa nzuri na vijana wake wameongeza kiwango, kwani walikuwa wakisumbuliwa na ufungaji, lakini tangu walipocheza na Ruvu Shooting wamebadilika.
Simba: Juma Kaseja, Nassoro Masoud ‘Cholo’, Amir Maftah, Paschal Ochieng, Shomari Kapombe, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi, Mrisho Ngasa.
Polisi Moro: Aghaton Mkwando, Nahodha Bakari, John Bosco, Noel Msakwa, Hamis Mamiwa, Abdallah Mfuko, Bantu Adimini, Maige Paschal, Ally Shomari, Malimi Busungu, Nocolaus Kabipe.
Kwenye dimba la Taifa, Yanga ililianza pambano kwa uchu na dakika ya 2 tu, Nadir Haroub ‘Canavaro’ alitumbukiza kitu kambani kwa kichwa, akimalizia krosi safi ya Athumani Idd ‘Chuji’.
Yanga ilizidi kuliandama lango la Mgambo na dakika ya 39, Mrundi Didier Kavumbagu alikandamiza la pili akimalizia krosi murua ya Hamis Kiiza. Hadi dakika 45 zinamalizika, Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-0.
Kipindi cha pili, Yanga ilizidi kucharuka na kuwapelekesha puta Mgambo hao wa JKT, ambako mtokea benchi, Jerry Tegete aliyepishwa na Kavumbagu, alipiga bao la tatu akiitumia vema kona ya Oscar Joshua dakika ya 79.
Dakika ya 86, Mgambo ilipata pigo baada ya mchezaji wake Salum Mlima kulimwa kadi nyekundu na mwamuzi Martin Saanya wa Morogoro kwa kumchezea vibaya Mbuyu Twite. Hadi mpira unamalizika Yanga 3, Mgambo 0.
Kwa matokeo hayo, Yanga na Simba zina pointi 23 kila moja, lakini Watoto wa Msimbazi wakifanikiwa kubaki kileleni kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Yanga: Ally Mustapha 'Barthez', Shadrack Nsajigwa, Oscar Joshua, Nadir Haroub 'Cannavaro', Mbuyu Twite, Athuman Idd 'Chuji', Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima.
Mgambo JKT: Godson Mmasa, Salum Mlima, Yasin Awadh, Salum Kipanga, Bakari Mtama, Ramadhani Malima, Chande Magoja, Musa Ngunda, Issa Kandulu, Fully Maganga, Juma Mwinyimvua.
Matokeo mengine, huko jijini Arusha, Mtibwa Sugar ilizinduka na kuwalaza maafande wa JKT Oljoro kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, huku huko Mwanza, mechi kati ya Toto na Kagera ilishindwa kuchezwa baada ya mvua kubwa kunyesha, hivyo itapigwa leo.

My playlist of today

sikiliza nyimbo mbalimbali mpya kila siku katika blog hii inayokujali

Maoni ya katiba mpya ‘Ijumaa iwe siku ya mapumziko’

MKAZI wa Kijiji cha Kikwe wilayani Siha, Halima Munisi ametaka katiba ijayo iitambue siku ya Ijumaa kuwa ni siku ya mapumziko kama zilivyo siku za Jumamosi na Jumapili.
 Munisi alitoa pendekezo hilo juzi wakati akitoa maoni yake mbele ya kamati ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa ikiongozwa na Profesa Mwesiga Baregu.
 Kwa mujibu wa mwananchi huyo, Ijumaa kutokuwa ni siku ya mapumziko hasa kwa kuwa ndio siku ya kumuabudu Mola kwa Waislam si sahihi na kutaka siku hiyo iwe ya mapumziko.
 Mkazi wa Kitongoji cha Nasai, Stanslaus Mallya alitaka katiba ijayo iweke kifungu ili Mawaziri watakaoteuliwa katika Baraza la Mawaziri wasiwe wabunge wa kuchaguliwa wala kuteuliwa.
 Mallya alisema kitendo cha Mawaziri kushika kofia mbili ya Uwaziri na Ubunge, kinawafanya wasitekeleze majukumu yao ipasavyo hasa pale inapofikia mahali pa kuibana Serikali.
 Kwa upande wake mkazi wa Ndoroso, Solomon Mmari alitaka Spika wa Bunge asiwe Mbunge na wala kuwa mfuasi wa chama chochote cha siasa ili aweze kutenda wajibu wake kwa haki.
 Hoja hiyo iliungwa mkono na Radegunda Nyabu, mkazi wa Magadini Bomang’ombe ambaye alisema endapo Spika anatokana na chama cha siasa, kuna kila sababu ya kutoa upendeleo.
 “Mbunge wa chama cha upinzani anatoa mchango wake anaambiwa kaa chini hata kama ana mchango mzuri kiasi gani… Spika akiwa kwenye chama fulani inaleta mpasuko”alisema.
 Pia alitaka Katiba Mpya iweke kifungu kitakachoilazimisha Tume ya Uchaguzi (NEC), kutopanga siku ya uchaguzi kwa siku zile ambazo zinatumika kumwabudu Mungu.
 Kwa mujibu wa Nyabu, siku hizo ni Ijumaa kwa waumini wa Kiislam na Jumamosi na Jumapili kwa waumini wa Kikristo ili kila mmoja aweze kumwabudu na kumtukuza mola wake.

Mzee wa Upako ‘awapaka’ viongozi wa dini wanaojali dini zao kuliko za wengine

KIONGOZI wa Kanisa la Maombezi la GRC na Ubungo, Dar es Salaam, Mchungaji Antony Lusekelo amewataka viongozi wa dini na Watanzania kwa jumla, kutambua kuwa Tanzania ni bora kuliko dini zao.

Mchungaji Lusekelo pia aliwataka viongozi wa dini kuendeleza vita dhidi ya rushwa huku akisema watoa rushwa na wapokeaji, wamejificha makanisani na kwenye misikiti.
Alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  ambapo alisema viongozi wa dini lazima lazima washiriki katika mapambano ya rushwa bila woga.
Katika mazungumzo hayo, mchungaji huyo pia alisema  Serikali inapaswa kuwajibika kwa kutumia nguvu zake za kisheria katika kulinda amani, huku akinyoshea kidole tukio la hivi karibuni lililoashira kuvunja kwa amani, huku Serikali ikiwa haijachukua hatua.
Alisema hilo ni tatizo kubwa na kwamba  ni watu wengi wakiwamo viongozi wa dini kushindwa kusema ukweli kwa kuogopa maisha yao kuwa mafupi.
“Ni muhimu kila mwananchi kutambua kuwa  Tanzania ni bora kuliko Ukristo na Uislamu. Watu wengi wanaogopa kusema ukweli. Hata viongozi wa dini kwani watoa rushwa wamejificha misikitini na makanisani, tuendeleze mapambano dhidi ya rushwa ipo siku tutashinda,” alisema.
Kuhusu vurugu nchini, alisema chanzo ni viongozi wa dini  kuhubiri siasa za chuki misikitini  na makanisani.
“Vurugu siyo asili ya binadamu inatengenezwa, Serikali ina wajibu wa kutumia nguvu yake kisheria kuilinda amani na amani haishuki kutoka mbinguni au kwa maombi, inatengenezwa pia. Tatizo cheche za kidini zilipoanza hazikudhibitiwa. Serikali ilikuwepo, aidha kwa makusudi au bahati mbaya imelea cheche hizo,” alisema Lusekelo.
Lusekelo maarufu kama mzee wa Upako alisema  watu o wanataka nchi isikae kwa amani na kuandaa mazingira ya watu kukosea.

Hotuba ya Mbunge wa Chadema yamkuna Rais Kikwete (JK)

HOTUBA ya Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) akisifu utendaji kazi wa Rais Jakaya Kikwete na kwamba wananchi wa Rombo wana imani naye kubwa jana ilimkuna Rais Kikwete.
Katika hotuba yake katika sherehe za uzinduzi wa Barabara ya Mkuu-Tarakea, Selasini alisema wapo wanasiasa ambao hakuwataja wenye desturi ya kupanda kwenye migongo ya mafanikio ya wenzao.
Alisema kama angekuwa na uwezo angeipa barabara hiyo jina la “barabara ya JK” kwa sababu ndiye aliyetoa fedha za ujenzi wa barabara hiyo na kuhakikisha ndoto ya wananchi wa Rombo inatimia.

“Nina kila sababu ya kukushukuru na kukupongeza kwa sababu wapo wanasiasa wamekuwa na desturi ya kupanda kwenye migongo ya wengine wamekuwa wakisema wamejenga hii barabara”alisema.

Alisema barabara hiyo imekuwa katika makabrasha tangu enzi za ukoloni. lakini ni Rais Kikwete ambaye ametimiza ndoto ya Warombo ya kuungana tena na wenzao kwa shughuli za kibiashara.

Selasini alisema Wananchi wa Rombo walikuwa kama wametengwa na wananzi wenzao wa wilaya nyingine kwa vile walikuwa wakitumia siku zaidi ya saba kutoka Tarakea hadi Moshi mjini.

Mbunge huyo alimuomba Rais Kikwete asaidie kujenga malambo mawili kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji na pia kikosi cha kudhibiti tembo kutoka Kenya kipatiwe gari la doria.
Alisema Rais Kikwete ndiye aliyetoa ahadi ya kuijenga barabara hiyo ambayo huko nyuma iliwahi kutolewa ahadi nyingi za kujengwa lakini hazikuweza kutekelezwa hadi Rais Kikwete alipoivalia njuga.
Kwa mujibu wa Selasini,wananchi wake wana imani kubwa na utendaji wa Rais Kikwete katika kipindi cha miaka mitatu iliyobaki na akasema kwa ujenzi wa barabara hiyo kamwe hawatamsahau maishani.

Katika hotuba yake, Rais Kikwete alisema Selasini ni mfano mwema wa siasa na akasema anaposemea mahitaji ya Wananchi wa Rombo anaiambia Serikali na kuahidi kutekeleza ombi lake la malambo.
“Nakushukuru kwa maneno yako mazuri wewe ni mfano mwema wa siasa za vyama vingi, hakuna neno zuri bali kuna wanaotawala na wako wanaopika utawala”,alisema Rais Kikwete bila kufafanua.

Alisema haitakuwa na maana kwamba kila kizuri kinachofanywa na Serikali basi viongozi wa upinzani wakibeze akisema angeshangaa kama wapinzani watakataa hajajenga barabara hiyo

Rais Kikwete alisema kuzinduliwa kwa barabara hiyo iliyojengwa kwa usimamizi wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), kutafungua fursa za kiuchumi kwa wananchi wa Rombo na nchi jirani.

KAULI YA MKUU WA MKOA DAR KUHUSU SILAHA ZINAZODAIWA KUFICHWA MISIKITINI.

                                       Maandamano ya oktoba 19/ 2012.
Kutokana na kuenea kwa taarifa kwamba katika baadhi ya Misikiti jijini Dar es salaam kumehifadhiwa silaha mbalimbali zinazotarajiwa kutumika kwenye maandamano ya waumini wa dini ya kiislamu watakaoandamana ijumaa novemba 2, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick amesema Jeshi la polisi linazo taarifa na limejipanga.
Namkariri mkuu wa mkoa akisema “ninawataka wala siwaombi, waache utaratibu wao huo kama ni kweli hayo yanayoelezwa lakini nasema sisi kwa utaratibu wa kiserekali hatujapata hilo tishio lakini kama kuna mtu yeyote mwenye nia hiyo ya kuhamasisha watu waende na mapanga, anachezea moto… serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama vitakabiliana na hali yoyote na mtu yeyote atakaekuja na kitisho cha aina yoyote”
Mkuu huyo amesema maandamano hayo ambayo yanahamasishwa kupitia vipeperushi ambavyo vimetolewa na jumuiya na Taasisi za kiislam nchini ni batili hivyo polisi wamejipanga kwa atakaejitokeza.
Sadick amesema pia kwamba sababu zote zilizotolewa na jumuiya na taasisi hizo zimefanyiwa kazi ikiwemo ile ya kumchukulia hatua kijana anaedaiwa kudhalilisha kitabu cha dini hiyo pamoja na kukamatwa kwa watu wote waliohusika na vurugu zilizotokea katika baadhi ya maeneo Dar es salaam.
Maandamano ya sasa yamepangwa kufanyika ijumaa hii baada ya swala ya ijumaa Dar es salaam ambapo yamepangwa kuelekea kwenye ofisi ya Waziri mkuu na mikoani ni kwenye ofisi za Wakuu wa mikoa.

WANASIASA 10 WA AFRIKA MAARUFU KWENYE TWITTER, MTANZANIA MMOJA.

Hii ni ripoti ya gazeti la The Gurdian la Uingereza.
.
.
.
.

Serikali yanyanyua mikono Fao lakujitoa.Sasa ni ruksa wafanyakazi kuchukua mafao yao muda wowote.

SERIKALI jana iliwasilisha tamko bungeni kurejesha kwa fao la kujitoa katika mifuko ya jamii, ambalo liliondolewa na Mamlaka ya Kusimamia na Kudhibiti Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Agosti mwaka huu.
Akiwasilisha tamko hilo bungeni jana, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka alisema kwa kuzingatia mchakato ulioanza wa kuangalia upya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii, SSRA imeliondoa agizo la kuzuia mifuko kutoa fao la kujitoa.

Alisema kufuatia hatua hiyo , mifuko yote itaendelea kutoa fao hilo kama ilivyokuwa kabla ya zuio hilo na kwa vigezo vilevile kwa wanachama wanaostahili kupata fao hilo.

Waziri huyo alisema Serikali inaandaa muswada wa sheria wa kufanyia marekebisho sheria ya mifuko ya jamii sambamba na kuondoa katika muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali sehemu inayohusu fao la kujitoa.

Alisema kabla ya kuandaa muswada huo, Serikali itafanya majadiliano na wadau wote wakiwamo wabunge, vyama vya wafanyakazi, waajiri na wananchi.

Juzi SSRA ilitoa taarifa ya kufuta tamko lake la kuzuia fao la kujitoa kwa wanachama wa mifuko ya jamii nchini.

  “Mamlaka ya Usimamazi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), inapenda kuufahamisha umma kufutwa kwa tangazo lililotolewa na mamlaka Agosti 2012 kwenye vyombo mbalimbali vya habari lililohusu kusitishwa kwa fao la kujitoa,” ilisema sehemu ya taarifa ya SSRA.

Pamoja na maelezo hayo, taarifa hiyo pia ilieleza kuwa uamuzi huo unaendana sambamba na hatua za Serikali za kuendelea na utekelezaji wa azimio la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kikao cha nane kilichoazimia pamoja na mambo mengine kuirejesha sheria ya hifadhi ya jamii.

J.K kuutubia Arusha siku chache baadaa ccm kunyang'anywa kata ya daraja mbili,na ni mara ya kwanza toka wapoteze jiji hilo kwa CHADEMA 2010.

RAIS Jakaya Kikwete leo atahutubia mkutano wake wa kwanza wa hadhara jijini Arusha tangu kumalizika kwa uchaguzi Mkuu mwaka 2010, ulioshuhudia iliyokuwa ngome ya CCM, ikiangukia mikononi mwa Chadema.
Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, atahutubia mkutano huo katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid, zikiwa ni siku nne tangu CCM kinyang’anywe kiti cha Udiwani Kata ya Daraja II, kilichonyakuliwa na Chadema.
Daraja II ni kati ya kata 29 zilizofanya uchaguzi mdogo Jumapili iliyopita, huku CCM ikifanikiwa kutetea kata zake 24 na kushuhudia tatu zikiangukia mikononi mwa Chadema iliyoshinda tano.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo alisema licha ya Rais Kikwete kuhutubia mkutano wa hadhara, atazindua miradi ya miundombinu na elimu katika Jiji la Arusha na Wilaya ya Monduli.
“Kabla ya kuhutubia wakazi wa Arusha na vitongoji vyake, Rais Kikwete atazindua hospitali ya Ortumer na baadaye kuwa mgeni rasmi sherehe za uzinduzi rasmi wa Arusha kupanda hadhi kutoka manispaa kuwa jiji,”  alisema Mulongo.
Alisema Novemba 2, Rais Kikwete atakizindua rasmi Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Nelson Mandela kilichopo eneo la Tengeru wilayani Arumeru, baadaye atatembelea kiwanda cha A to Z kinachotengeneza vyandarua vyenye viuwatilifu vya kuua mbu.
Pia, ratiba hiyo inaonyesha Novemba 3, atatembelea Wilaya ya Monduli ambako atazindua Sule ya Msingi Sokoine kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa upanuzi wa barabara ya Arusha Minjingu.

Habari zilizopatikana mjini hapa juzi usiku zinasema, Zungu alikamatwa saa 4.30 katika moja ya vituo vya mafuta akidaiwa kujaribu kutoa rushwa ya Sh100,000 kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM.

Waandishi Wetu, Dodoma
MMOJA wa Wenyeviti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu pamoja na makada wengine wa CCM, juzi usiku walikamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Dodoma kwa tuhuma za rushwa.

Habari zilizopatikana mjini hapa juzi usiku zinasema, Zungu alikamatwa saa 4.30 katika moja ya vituo vya mafuta akidaiwa kujaribu kutoa rushwa ya Sh100,000 kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM.

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Eunice Mmari, jana alikiri kuwakamata baadhi ya watu wakijihusisha na vitendo vya rushwa akiwamo Zungu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mmari alidai kuwa vijana wake walimtia nguvuni Zungu juzi saa tatu usiku katika Hoteli ya Golden Crown akiwa na wapambe wake wakiendelea kugawa fedha kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wazazi.
Alisema taarifa za Zungu kudaiwa kugawa fedha hizo walizipata juzi mchana na kuanza kufuatilia nyendo zake ambazo zilionyesha kuwa na dalili zote za rushwa.
“Tuliweka mitego yetu kila mahali ndipo tukabahatika kukutana naye katika eneo la hoteli hiyo akiwa na magari mawili, moja ikiwa ni teksi ya kawaida na nyingine ikiwa ni Prado ambayo ndiyo ilisadikiwa kubeba pesa,” alisema Mmari.
Kamanda huyo alidai kuwa kiasi cha fedha kilichokuwa kikitolewa na Zungu kilikuwa Sh100,000 kwa kila mjumbe ili kumshawishi ampigie kura.
Hata hivyo, alisema hawakuweza kumkamata moja kwa moja akitoa na hata fedha hizo hawakuzikamata kwani maofisa wa Takukuru walizingira gari dogo wakati fedha hizo zinasadikiwa zilikuwa katika Prado ambalo baada ya vurugu hizo lilitokomea kusikojulikana.
Akizungumzia madai hayo Zungu alisema: “Kwanza niseme kuwa si kweli kwamba nimekamatwa nikitoa rushwa, nilikuwa katika kituo kimoja cha mafuta wakaja watu ambao walisema wana shaka na gari langu.”
Aliendelea: “Samahani, halikuwa gari langu, bali ilikuwa ni teksi, mimi nikawaruhusu, wakaingia wakafanya ukaguzi na waliporidhika wakaniachia nikaondoka.”

Taarifa za awali

Zungu alikuwa mmoja wa wagombea wa nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec) kupitia Wazazi katika uchaguzi uliofanyika jana mjini Dodoma.
Habari zilizopatikana mapema jana zilisema baada ya kukamatwa, Zungu alipelekwa Ofisi ya Takukuru Mkoa wa Dodoma ambako alihojiwa hadi saa nane usiku alipoachiwa baada ya kuwekewa dhamana na Mbunge wa Bukene (CCM), Selemani Zedi.
Habari hizo zinaeleza kuwa baada ya kukamatwa, gari alilokuwamo lilifanyiwa upekuzi kabla ya kupelekwa Ofisi za Takukuru, pamoja na makada wengine wa CCM ambao walikamatwa kwa tuhuma hizohizo.
Kamanda Mmari pia alithibitisha kukamatwa kwa makada wengine watano ambao aliwataja kuwa ni Yahaya Danga, Busuro Pazi na Frank Mang’ati ambao alidai kwamba walikuwa wakimsaidia Zungu katika mpango wake huo.
Mbali na watu hao, Takukuru ilimtia mbaroni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Mbeya, Fatuma Kasenga ambaye anadaiwa kukamatwa akitoa rushwa ya chakula kwa wajumbe.
Alisema alikamatwa katika Hoteli ya Kitoli, Barabara ya Iringa saa tisa usiku.
Alisema kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja waliachiwa kwa dhamana na kwamba uchunguzi unaendelea.
Katika hatua nyingine, Mmari alisema kuwa taarifa walizokuwa nazo ni kuwa mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya hiyo, Abdallah Bulembo alikuwa akitoa rushwa zaidi.
“Tatizo ni kwamba wanazungumza lakini hawatoi ushirikiano, maana kama wangetoa ushirikiano tungeweza kuwakamata kwa urahisi,” alisema Mmari.

Bunge hawajui

Akizungumzia kukamatwa kwa mbunge huyo, Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel alisema Ofisi ya Bunge haikuwa na taarifa zozote kuhusu kukamatwa kwa mbunge huyo.
“Ndugu yangu, ndiyo nasikia kutoka kwako, sisi hatuna taarifa hiyo. Ni vigumu kuzungumzia jambo ambalo sijalisikia. Hata hivyo, nakushukuru sana kwa taarifa,” alisema Joel.
chanzo mwananchi.

magazeti ya leo yapo hapa 1/11/2012

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Watoto watano ,watatu wakiwa wa familia moja wamekufa Wilayani Karagwe mkoani Kagera Magharibi mwa Tanzania.

Ni baada ya kulipukiwa na bomu la kutupwa kwa mkono wakati walipokuwa wakichezea Bomu hilo lililookotwa kwenye vyuma chakavu na kudhani kuwa ni mpira.
Tukio hilo lilitokea Jumatano majira ya asubuhi huko Wilayani Karagwe mkoani Kagera Magharibi mwa Tanzania wakati watoto walipokuwa wakichezea kitu mfano wa mpira mdogo ,ambacho baadaye kilikuja kutambulika kuwa lilikuwa Bomu la kurushwa kwa mkono.
Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC mjini Dar es Salama, Eric David Nampesya , mkuu wa Wilaya wa Karagwe Bi Darli Rwegasira amesema kuwa watoto hao walilipukiwa na Bomu hilo ambapo watatu kati yao walikufa papo hapo huku wawili wakifia hospitalini.
Kwa Mujibu wa Mkuu huyo wa Wilaya, awali mzazi wa watoto hao amekiri kuwa aliliona bomu nyumbani kwake hapo juzi ambapo watoto wake walikuja nalo baada ya kuliokota huku wakidhani kuwa ni mpira.
Naye Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Philipo Kalangi alisema kuwa utafiti waliofanya umeonyesha kuwa Bomu hilo lililookotwa na kijana mmoja ambaye alikuwa akikusanya vyuma chakavu kwa lengo la kuviuza hapo wilayani karagwe.
Bomu hilo lilikuwa mojawapo katika vyuma alivyokuwa ameokota na baadaye watoto hao walienda kulichezea nyumbani kwao na hatimaye kusababisha maafa hayo.
Mkuu huyo wa Polisi mkoani Kagera alidokeza kuwa uchunguzi unaendelea ili kujua kwa undani Bomu hilo lilitokea wapi na iwapo kama kuna mabomu mengine yanayoweza kuwa yamebaki katika maeneo mbali mbali hapo Wilayani Karagwe.
Mkuu huyo wa Polisi hakuweza kukiri wala kukana moja kwa moja kuhusisha Bomu hilo Kama matokeo ya uwepo wa wakimbizi wa Rwanda waliowahi kuishi Wilayani hapo mwaka 1994 baada ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda ambapo Wilaya ya Karagwe ni moja ya wilaya zilizopokea wakimbizi wengi kutoka nchini Rwanda.
Uchunguzi zaidi unaendelea huku ukiwahusisha wataalam wa milipuko kutoka Polisi na jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
source bbc.com

Why Hurricane Sandy might cost Obama the popular vote—but not the presidency

This year’s black swan arrived on a rush of wind.
Once again, a highly unlikely, unanticipated event has roiled the waters—literally—late in the campaign cycle. Twelve years ago, it was the revelation of George W. Bush’s long-ago drunk driving arrest that likely cost him the popular vote and almost cost him the White House. Four years ago, the September collapse of Lehman Brothers and the near-collapse of the global financial universe turned a likely Obama victory into a certain one.
And this year, the impact of Hurricane Sandy makes it more likely that we’ll see a presidential election where the winner winds up winning fewer votes than the loser.
Even before Sandy struck the East Coast Monday, an observation was gaining hurricane force: What if Sandy had struck a week later? What if, on Election Day, tens of millions were without power, with mass transit shut, roads flooded, polling stations shut or inaccessible? Would states or the federal government postpone the voting?
Well, we don’t have to turn to “what-if” questions (much as I enjoy them). The storm will likely have a measurable impact on next Tuesday’s voting.
In the past, we’ve seen less powerful storms knock out power for well over a week. Flooding has already taken place on a massive scale, meaning that property owners across the East, and hundreds of miles inland, will be coping with water in their cellars, living rooms, stores and offices. There are schools that may still be closed. This means there’s a very good chance that voters—maybe hundreds of thousands of them—will be coping with urgent, personal affairs, and the trip to the polls may simply be one burden too many.
Now consider where these voters are: overwhelmingly, they’re in states where Obama is all but certain to win, and with huge pluralities. (The latest poll out of New York gives the President a 61-35 advantage over Mitt Romney, which translates to a 2-million-vote plurality.)
This enormous lead, combined with the post-storm burdens, suggests that there’s markedly less incentive than usual for Obama voters in deep-blue states to vote.
The likely result? An increased chance that Obama will lose the national popular vote to Romney, and thus an increased chance that we’ll see, as we did in 2000, a split between the popular vote and the Electoral College tally that in fact decides the presidency.
Should Obama win the election this way, it would be historic: We’ve never had an incumbent president returned to office while losing the popular vote. (Gerald Ford came close; despite losing the popular vote by 1.7 million votes, a shift of barely 11,000 votes in Ohio and Hawaii would have kept him in the White House).
More significant, it would rekindle the argument over the Electoral College that arose—briefly—in 2000: Is this 200-year old mechanism, with an overtly anti-democratic tilt (small states have disproportionately more clout than big states), the right way to choose a president?
After immersing myself in the mysteries of the Electoral College for a novel I wrote in the ’90s, I came away believing that the case for scrapping it is less obvious than I originally thought.
For one thing, losing the popular vote is not necessarily a sign of what “the people” really wanted. Candidates structure their campaigns around the Electoral College; had 2000 been a popular vote election, George W. Bush would have spent more time running up the vote in Texas and California’s inland empire, while Al Gore would have been campaigning in Dallas and Atlanta.
For another, the chaos that enveloped Florida back in 2000 might extend to every state if the popular vote was as close as it was in 1960, 1968, and 2000 (and as it may well be this time). Instead of lawyers and operatives descending on Florida, they might be loaded onto C-130s and parachuted into every state where disputes arose.
I grant you, this inquiry is speculative. It still may be that in the last week of the election, there will be a decisive shift in the electorate that turns a nail-biter into a clear victory. It may be that Sandy is not the Black Swan that will shape the outcome.
source-yahoo news

Kimbunga Sandy chapunguza kasi ,chaitia hasara marekani cha mamilioni ya dollar

        Baadhi ya athari za kimbunga Sandy nchini Marekani
Biashara na huduma nyinginezo zinatarajiwa kurejea katika hali ya kaiwaida hii leo baada ya siku mbili za kufungwa kufuatia kimbunga kilichopiga Kaskazini Mashariki mwa Marekani.
Baadhi ya viwanja vya ndege, majengo ya serikali, shule na hata soko la hisa la New York, zilifunga shughuli zao
Maelfu ya watu katika eneo la kaskazini mashrikiwamo katika kumbi za shule tofauti kwa usiku wa pili na katika hifadhi nyengine za dharura baada ya makaazi yao kuathirika na mafuriko kutokana na kimbunga kibaya kuwahi kutokea katika eneo hilo kwa miongo kadhaa.
Kimbunga hicho kimesababisha vifo vya zaidi ya watu arobaini, miongoni mwao watu kumi na nane kutoka jimbo la New York.
Zaidi ya nyumba milioni nane na maeneo ya kibiashara katika majimbo kumi na saba yamo gizani kwa kukosa huduma ya nguvu za umeme.
Usafiri umetatizika pakubwa na usafiri wa chini ya ardhi wa treni mjini New York huenda usifunguliwe kwa siku kadhaa zijazo.
Rais Obama anatarajiwa kuzuru majimbo yalioathirika zaidi kama vile New Jersey,baadaye hii leo. Kimbunga hicho kimepungua kasi lakini wataalmau wanaonya kuwa shughuli ya kusafisha miji huendna ikachukua muda.
chanzo bbc.com

Mkutano unafanyika leo mjini London kujadili mkakati mpya wa utakaotumika baada ya ule wa malengo ya milenia.

mtoto wa kiafrika ,ambapo bado njaa ni tishio kwa bara la Africa
 Malengo hayo yaliwekwa mwaka elfu mbili kuimarisha maisha ya watu katika nchi maskini na walitumai kuwa yangefikiwa mwishoni mwa mwaka 2015.
Aidha malengo hayo yananuia kukabiliana na maswala kama viwango vya umaskini, magonjwa , njaa na ukosefu wa elimu lakini mafanikio yamekuwa kidogo sana ikilinganishwa na matumaini ambayo watu walikuwa nayo.
Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, anafanya mazungumzo na Rais Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia na Rais Susilo Bambang Yudhoyono wa Indonesia, wenyekiti watatu wa jopo la umoja wa mataifa litakalopewa jukumu la kuweka mkakati mwingine mwaka 2015 kwa sababu ya malengo ya milenia.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa wale wanaohudhuria mkutano wa London watahitaji kutafakari ikiwa swala la malengo ya kupata misaada ni wazo la kizamani liliopitwa na wakti.

Kilimo cha bangi chaongezeka Burma,je takwimu za Tanzania zinajulikana?

                                                              Shamba la bangi nchini Burma
Umoja wa mataifa unasema kilimo cha bangi nchini Burma kimeongezeka kwa mwaka wa sita mtawalia.
Ripoti iliyotolewa na ofisi ya Umoja huo inayoshughulikia masuala ya madawa ya kulevya na uhalifu inasemas sehemu ya ardhi ambayo bangi hiyo imepandwa imeongezeka kwa asilimia kumi na saba.
Umoja huo umelaumu ongezeka la ukuwaji huo wa bangi kutokana na ukosefu wa utulivu na mzozo katika majimbo ya Shan na kachin ambako ndiko kuna mashamba mingi ya bangi.
Inasemekana wakulima hawakuwa na mazao mbadala ya kukuza kando na bangi hiyo ambayo hutumika kama kilewesha kwa kuwa ni zao lenye faida kubwa kifedha.
Burma ni nchi ya pili duniani inayokuza kwa wingi bangi baada ya Afghanistan.
Mwandishi wa BBC anasema hakuna jitihada kamili za kumaliza ukuwaji wa bangi kwa kuwa jeshi nchini humo na makundi ya wanamgambo yananufaika kutokana na biashara hiyo.
swali la kujiuliza je kwa nnchi za africa kama Tanzania na kenya je kunazo takwimu za kilimo cha bangi?tupe maoni yako.
chanzo-bbc.com

Tuesday, October 30, 2012

Mwanaume aliyewafanyia vitendo vya kishirikina au ''Juju'' wasichana ambao alikuwa anawalangua kutoka nchini Nigeria hadi barani Ulaya amehukumiwa jela miaka 20 nchini Uingereza.

Osezua Osolase raia wa Nigeria na mwenye umri wa miaka 42,kutoka mtaa wa Gravesend, Kent aliwatumia wasichana maskini kwa kuwahadaa kuwa wangepata maisha mazuri baada ya kufika alikokuwa anawapeleka.
Jaji Adele Williams wa mahakama ya Canterbury Crown alisikia katika ushahidi uliotolewa mahakamani dhidi ya mshtakiwa na kumwambia kuwa alikosa utu kwa kufanya vitendo kama vile.
Osolase alipatikana na hatia ya makosa matano ikiwemo ubakaji na kumfanyia dhulma za kingono mtoto mdogo.
Jopo la majaji lilisikia katika kesi hii iliyoisha siku ya Ijumaa kuwa vitendo vya kishirikina pia vilitumiwa kuwatia hofu waathiriwa watatu wa vitendo vya Osolase.
Jaji alisema kuwa Osolase ambaye ni mwathiriwa wa HIV, aliwatia hofu waathiriwa wake ili kuwalazimisha kumtii na kukaa kimya.
"umetenda dhulma na kuwafanyia unyama waathiriwa vitendo vyako'' jaji alimwambia bwana Osolase.
"wewe sio mwaminifu hata kidogo. Una kiburi na ukatili, hauna ubinadamu wala huruma kwa waathiriwa wako.'' aliongeza jaji
Aidha jaji Williams alisema kuwa bwana Osolase aliwaharibu wasichana hao wakati alijua kuwa ana virusi vya HIV na hata kumbaka msichana mmoja wakati akijua alifanya kitendo kibaya sana .
Osolase aliwapeleka wasichana hao kwake nyumbani kabla ya kuwapeleka barani Ulaya kufanya kazi ya ukahaba.
Mahakama ilisema kuwa mwanaume huyo arejeshwa nyumbani Nigeria atakapomaliza kuhudumia kifungo chake.
Mmoja wa wasichana alielezea yaliyomkuba wakati akifanyiwa vitendo vya kishirikina, alisema alitolewa damu mwilini , kisha akakatwa nywele zake za kichwani na sehemu zake za siri.Baada ya hapo alilishwa kiapo kutosema chochote.
Osolase alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Stansted mwezi Aprili alipojaribu kupanda ndege mwaka jana.

KUFUATIA CHAGUZI NDOGO ZA UDIWANI -CHADEMA Tumeshinda,Wasema Nape anapiga vuvuzela bila tathmini

WAKATI Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akitambia ushindi mkubwa walioupata katika kata 22 kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Jumapili, CHADEMA wamemtaka aache kuwa kama vuvuzela, wakidai wao ndio washindi.
Chama hicho kimesema kutokana na idadi kubwa ya kura walizopata katika kata zote hata zile ambazo hawakushinda ni dhahiri kuwa ngome yao inazidi kuimarika maeneo mengi nchini kiasi cha kuweza kuwanyang’anya CCM kata.
Kauli ya CHADEMA ilitolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa (Bavicha), John Heche, wakati akijibu tambo za Nape na kudai kuwa kada huyo ni sawa na vuvuzela, kwani kama angekuwa anafanya tathmini angeweza kubaini ni kwanini wananchi wanazidi kuikataa CCM.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi ndogo za chama hicho zilizopo Mtaa wa Lumumba, Nape alisema kuwa idadi kubwa hiyo ya madiwani waliyopata ni ishara kwamba CCM bado kinakubalika kwa wananchi na kitaendelea kushinda katika chaguzi zijazo.
Kauli ya Nape inakuja ikiwa ni siku moja tangu kumalizika kwa uchaguzi huo mdogo kwenye kata 29, ambapo CCM iliweza kurejesha kata zake 22 na kupoteza tatu zilizochukuliwa na CHADEMA iliyoshinda kata tano na CUF ikipata kata moja.
Nape alisema ushindi huo umetokana na chama hicho kuhubiri amani mara kwa mara katika mikutano yake, tofauti na vyama vingine ambavyo sera zao ni za kumwaga damu, kitendo ambacho wananchi hawakikubali.
“Ushindi huu unadhihirisha kuwa hata katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 chama chetu kitawashinda wapinzani,” alijigamba.
Nape aliponda opereshini ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) inayoendeshwa na CHADEMA nchi mzima, akidai inaandamana na vurugu na kwamba haitakisaidia chama hicho.
Alisema operesheni hizo zimekuwa zikisababisha vurugu na vifo katika maeneo mbambali kilipopita chama hicho.
“Juhudi zote walizofanya Katibu Mkuu, Dk. Slaa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, hazikuzaa matunda, hiyo inatokana na siasa chafu za vurugu, hivyo wananchi wameamua kukinyima ushindi,” alisema.
Nape pia alisema kuwa CCM inalaani vurugu zilizotokea katika baadhi ya maeneo kulikofanyika uchaguzi huo kwamba huo si utamaduni wa Watanzania.
Alisema kuwa uchaguzi ulifanyika katika kata 29 na kati ya hizo 27 zilikuwa za CCM na mbili za CHADEMA, hivyo wao waliweza kuzirejesha kata zao na kutwaa nyingine tatu.
“Nape aache kupiga kelele kama vuvuzela bali wakae chini na kujifanyia tathmini, wajiulize ni kwanini watu wanazidi kuwakataa. Sisi kwanza tumeweka historia tangu mfumo wa vyama vingi uanze kwa kusimamisha wagombea kwenye kata zote, tumeweza kutetea kata zetu mbili na kuchukua za CCM tatu,” alisema.
Katika kujibu hoja hizo, Heche alisema kuwa wanachokifanya CCM sasa ni sawa na kufiwa na watoto halafu ukajipongeza kwa wale waliobaki, huku akibainisha kuwa uchaguzi huo umewawezesha CHADEMA kufika katika vijiji 116 na kusimika matawi.
Kuhusu madai ya Nape kwamba Operesheni ya M4C haikufua dafu katika uchaguzi huo kwa vile inachochea vurugu, alisema kuwa taarifa za magazeti mengi ya jana zilieleza bayana kuwa vitendo vya vurugu kwenye uchaguzi vilisababishwa na CCM kwa kuwashambulia wafuasi wa CHADEMA.
“CCM ni chama cha rushwa na wamechaguana kwa rushwa hata Mwenyekiti wao Jakaya Kikwete amekemea hilo kwenye mikutano ya UVCCM na UWT, sasa kwa mantiki hiyo Nape apime mwenyewe nani kapoteza na kama anafikiri tunafanya mzaha, basi angoje mwaka 2015,” alisema.

JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha, limemsafisha Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari

JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha, limemsafisha Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (CHADEMA), kuwa hakuhusika katika tukio la kufyatua risasi hewani kama ilivyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari jana.
Badala yake, Kamanda wa Polisi Mkoa, Liberatus Sabas, alisema kuwa wanamhoji mjumbe wa mkutano Muu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Wilaya ya Arusha, Godfrey Mwalusamba, kuhusiana na tukio hilo.
Kufuatia hatua hiyo, Nassari ametoa siku 14 kwa magazeti ya Uhuru na Habari Leo kukanusha taarifa walizoandika wakimhusisha na tukio hilo kwenye Kata ya Daraja Mbili siku ya Jumapili, vinginevyo atayashitaki Baraza la Habari nchini (MCT).
Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Kamanda Sabas alisema kuwa Mwalusamba alifyatua risasi hewani kwa lengo la kumuokoa mwanamke mmoja ambaye jina lake hakulitaja, ambaye alikuwa akishambuliwa na kundi la vijana wakimtuhumu kuwa alikuwa akigawa fedha kwa wapiga kura.
Alisema kuwa kwenye tukio hilo, Musa Khamisi, alijeruhiwa kwa kukatwa na panga ambapo jumla ya watu wanane walikamatwa na tayari walifikishwa mahakamani jana kujibu mashitaka ya kujeruhi na shambulio la aibu.
Naye Nassari, aliwaambia waandishi wa habari kuwa amefikia uamuzi wa kuyataka magazeti hayo kukanusha habari hizo kwa uzito uleule waliotumia kuzitangaza baada ya kutafakari na kujiridhisha kuwa habari hizo ziliandikwa kwa hila, zikiwa na lengo la kumchafua.
“Magazeti hayo yameandika kuwa nilifyatua risasi saa saba mchana Kata ya Daraja Mbili wakati muda huo nilikuwa Kata ya Bangata nikiwa wakala mkuu wa uchaguzi, siku hiyo nilipita Kata ya Daraja Mbili saa mbili asubuhi kwa ajili ya kushusha mawakala kisha nikaondoka,” alisema.
Alisema kuwa habari hiyo iliyoandikwa na gazeti la CCM na lile la Serikali iliandikwa kimkakati kwa lengo la kumchafua yeye binafsi na chama chake huku akiweka bayana kuwa huo ni mwendelezo wa hila anazofanyiwa tangu anyakue ushindi wa jimbo hilo.
source-tanzania daima

Monday, October 29, 2012

Kova kuanza kusaka mtandao wa vipeperushi vya maandamano ya Waislamu

POLISI nchini wamepanga kusambaratisha mtandao unaodhamini na kuchapisha vipeperushi vinavyohamasisha kufanyika kwa maandamano, kutaka kutolewa kwa Katibu wa Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda  Issa Ponda na wenzake.
Hatua hiyo imekuja baada ya waumini hao kupanga kufanya maandamano  Novemba Mosi, ambayo yatahamasisha mahakama hiyo kutoa dhamana kwa kiongozi wa taasisi hiyo na wenzake.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Suleiman Kova alisema wataanza kufanya msako wa wote wanaohamasisha, wanaochapisha na wanaotoa vipeperushi ili kuwakamata.
“Tunafuatilia wadhamini na wachapishaji wa vipeperushi kwani ni chanzo cha uchochezi na upotevu wa amani nchini,” alisema Kova.
Kova alisema maandamano hayo ambayo yamepangwa na waumini hao yanatishia amani , wananchi watashindwa kwenda kazini na kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.
“Hatuna mazungumzo tena kwa suala lolote litakalotishia uvunjifu wa amani hasa kwa yeyote atakayefanya maandamano bila kibali, hatutangalia anatoka dini gani au chama gani hivyo polisi itafanya kazi yake na kuwachukulia hatua kali,” alisema Kova na kuongeza:
“Kisheria kumtishia mtu siyo lazima utumie bomu, bali unaweza ukatumia kauli au vipeperushi kama hivyo vya maandamano.”
Alisema wazazi watakaoruhusu watoto wa shule kufanya maandamano watachukuliwa hatua za kisheria na kufikishwa mahakamani, ikiwezekana  kufungwa mwaka mmoja jela.
“Nimesikia wanataka kuwahusisha watoto wasiende shule, ili wafanye maandamano ambayo yanazuiwa na sheria ya mtoto kutofanya maandamano,” alisema Kova na kuongeza:
“Sisi tutahakikisha sheria inachukua mkondo wake, kama kuna mtu amefikishwa mahakamani kuna taratibu zake za kupata dhamana, siyo kufanya maandamano haramu.”
Pia, aliwaomba wananchi wasishiriki maandamano hayo kwani yataleta madhara makubwa kwa familia zao kwa wale watakaokamatwa.
“Hii inajidhihirisha pale utakapotembelea familia za wale waliokamatwa katika maandamano yaliyopita, watoto wanashindwa hata kwenda shule kutokana na kukamatwa kwa wazazi wao na wanakosa nauli na chakula,” alisema Kamanda Kova.

Panya SUA wahudumia hospitali 13

UNAPOINGIA katika kitengo cha Apopo kilichopo katika Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA), Morogoro macho yako yatalakiwa na  vizimba vilivyosheheni panya.
Pia utalakiwa na ukanda mwembamba  uliobeba makopo madogo madogo yaliyojazwa makohozi, ambayo baadaye unabaini kuwa ni ya binadamu.
Inaweza kuwa kama wengi wasivyotarajia, kumwona Osama bin Laden akimkumbatia Rais  Barack Obama wa Marekani, kwani kwa mtu anayefika eneo hilo bila kujua kinachoendelea, atachanganyikiwana hata kushindwa kuelewa uhusiano uliopo kati ya panya na makohozi ya binadamu.
Lakini, katika kitengo hicho cha Apopo (SUA), panya wana uhusiano wa karibu na makohozi kwani mnyama huyo  ana kazi kubwa iliyo ya kipekee ambayo ni kuyapima makohozi ya binadamu ili kubaini iwapo yana vijidudu vya Kifua Kikuu (TB) au la.
Panya huyo anadaiwa kuwa na uwezo wa kupima sampuli 140 za makohozi kwa dakika 15 tu, wakati mtaalamu wa maabara aliyebobea huweza kupima wagonjwa 25 kwa siku.
Lakini, ili aweze kuifanya kazi hiyo, panya hutakiwa kwanza kwenda shule.
Kama ambavyo binadamu husoma kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu, vivyo hivyo kwa panya hao. Hupatiwa mafunzo maalumu katika ngazi tofauti ili kufuzu  jinsi ya kubaini  vijidudu vya TB  katika makohozi.
Panya  hao ni wanaopatikana Afrika, ambao  ni wakubwa kisayansi huitwa ‘cricetomy  gambianus’
Kitengo cha Apopo kwa sasa kina aina hiyo ya panya wanaofikia 30, ambao wapo katika mafunzo maalumu kwa kazi hiyo.
Mkuu wa Mafunzo ya Panya Apopo, Peter Luanda anasema kuwa wanyama hao hupewa mafunzo kuanzia wanapokuwa na umri wa kuanzia wiki nne tangu kuzaliwa.
“Nia ya kuwapa mafunzo hayo wakiwa wadogo, ni kuwafanya wakariri kwa urahisi elimu wanayopewa na pia  ujuzi wao utumike kwa muda mrefu,” anasema Luanda.
Anasema kuwa panya hao wanaobaini TB hupatiwa mafunzo katika hatua  zisizozidi tano.
Luanda anaeleza kuwa kama ilivyokuwa kwa panya wa kutegua mabomu, panya wa TB huanza kupewa mafunzo ya kuwazoea wanadamu ‘socialization stage’ na hatua ya pili ni ya chakula na mlio.
Hatua ya chakula na mlio ni ya kuwazoesha panya kujua kuwa, kila wanaposikia mlio fulani hapo wanatakiwa kula.
“Tunawapa mazoezi kila siku asubuhi na mchana, lakini kwa mafunzo ya TB, panya hupewa zaidi tembe za vitamini, wakati wale wa mabomu wakipewa vyakula kama ndizi na karanga,” anasema

Saturday, October 27, 2012

Zifuatazo ni timu 16 zitakazoshiriki fainali hizo-na historia zao kwa undani

JO'BURG, Afrika Kusini
RATIBA ya Fainali za Afrika 2013 inatarajiwa kupangwa keshokutwa mjini Durban, Afrika Kusini, ambapo fainali hizo zitaanza Januari 19 mpaka Februari 10 na zitafanyika kwenye viwanja vya Soccer City, Mbombela, Nelson Mandela Bay, Royal Bafokeng na Moses Mabhida.

Mechi ya ufunguzi na fainali zitachezwa kwenye Uwanja wa Soccer City jijini Johannesburg.

Zifuatazo ni timu 16 zitakazoshiriki fainali hizo:

AFRIKA KUSINI
Imeshiriki fainali hizo mara 7 ambazo ni  mwaka (1996, 1998, 2000, 2002, 2004, 2006, 2008).
Afrika Kusini ndiyo wenyeji wa Fainali za Afrika 2013. Mara ya mwisho Afrika Kusini imeshiriki fainali hizo ni 2008, ambapo tayari kocha wa Afrika Kusini, Gordon Igesund ametakiwa kuhakikisha timu hiyo inafika nusu fainali. Afrika Kusini imetwaa ubingwa wa Afrika mara 1 (1996).

GHANA
Ghana imeshiriki fainali za Afrika mara 18 ambazo ni mwaka (1963, 1965, 1968, 1970, 1978, 1980, 1982, 1984, 1992, 1994, 1996, 1998, 2000, 2002, 2006, 2008, 2010, 2012).

Mara ya mwisho Ghana imetwaa ubingwa wa Afrika ni mwaka 1982, lakini Ghana imetwaa ubingwa wa Afrika mara 4 (1963, 1965, 1978, 1982).

MALI
Mali imeshiriki fainali za Afrika mara 7 ambazo ni mwaka (1972, 1994, 2002, 2004, 2008, 2010, 2012).
Katika fainali za Afrika zilizofanyika mwanzoni mwa mwaka huu, Mali ilishika nafasi ya tatu. Haijatwaa Kombe la Afrika.

ZAMBIA
Mabingwa watetezi Zambia wameshiriki fainali za Afrika mara 15 ambazo ni mwaka (1974, 1978, 1982, 1986, 1990, 1992, 1994, 1996, 1998, 2000, 2002, 2006, 2008, 2010, 2012).

Zambia wana jukumu la kuonyesha hawakubahatisha kutwaa ubingwa wa Afrika mwanzoni mwa mwaka huu. Zambia imetwaa ubingwa wa Afrika mara 1(2012).

NIGERIA   
Nigeria wameshiriki fainali za Afrika mara 16 ambazo ni mwaka (1963, 1976, 1978, 1980, 1982, 1984, 1988, 1990, 1992, 1994, 2000, 2002, 2004, 2006, 2008, 2010).
Katika miaka ya hivi karibuni Nigeria ilikuwa imepoteza nguvu katika soka la Afrika. Nigeria imetwaa ubingwa wa Afrika mara     2 (1980, 1994).

TUNISIA    
Tunisia wameshiriki fainali za Afrika mara 15 ambazo ni mwaka (1962, 1963, 1965, 1978, 1982, 1994, 1996, 1998, 2000, 2002, 2004, 2006, 2008, 2010, 2012).

Hivi sasa kikosi cha Tunisia kinaundwa na vijana wengi bila wachezaji nyota kikitarajiwa kutoa ushindani wa hali ya juu. Tunisia imetwaa ubingwa wa Afrika mara 1 (2004).

IVORY COAST
Ivory Coast wameshiriki fainali za Afrika mara 19 ambazo ni mwaka (1965, 1968, 1970, 1974, 1980, 1984, 1986, 1988, 1990, 1992, 1994, 1996, 1998, 2000, 2002, 2006, 2008, 2010, 2012).
Hii ni nafasi ya mwisho kwa kizazi bora cha soka nchini Ivory Coast kujaribu bahati yao ya kutwaa ubingwa wa Afrika. Ivory Coast imetwaa ubingwa wa Afrika mara 1 (1992).

MOROCCO
Morocco wameshiriki fainali za Afrika mara 14 ambazo ni mwaka (1972, 1976, 1978, 1980, 1986, 1988, 1992, 1998, 2000, 2002, 2004, 2006, 2008, 2012).

Morocco hawakufanya vizuri katika fainali za mwaka huu, ila wanatarajiwa kutoa ushindani katika fainali za 2013. Morocco imetwaa ubingwa wa Afrika mara 1 (1976).

ETHIOPIA
Ethiopia wameshiriki fainali za Afrika mara 9 ambazo ni mwaka(1957, 1959, 1962, 1963, 1965, 1968, 1970, 1976, 1982).
Mara ya mwisho kwa Ethiopia kushiriki fainali za Afrika ilikuwa mwaka 1982. Hii ni kati ya timu za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati itakayoshiriki fainali za 2013. Ethiopia imetwaa ubingwa wa Afrika mara 1 (1962).

CAPE VERDE
Timu ya Cape Verde haijawahi kushiriki fainali za Afrika. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Cape Verde kushiriki fainali hizo za Afrika 2013. Vape Verde inaingia katika fainali hizo ikiwa imeitoa timu ngumu ya Cameroon. Haijatwa Kombe la Afrika.

ANGOLA   
Angola wameshiriki fainali za Afrika mara 6 ambazo ni mwaka  (1996, 1998, 2006, 2008, 2010, 2012). Katika miaka yote iliyoshiriki, mara nne imefika hatua ya nne bora, lakini imeshindwa kufika fainali au kutwaa ubingwa wa Afrika. Haijatwa Kombe la Afrika.

NIGER
Niger wameshiriki fainali za Afrika mara 1 ambayo ni mwaka (2012).
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Niger kushiriki fainali hizo za Afrika. Ni timu ambayo katika hatua ya kufuzu inafanya vizuri katika mechi zake zote za nyumbani. Haijatwa Kombe la Afrika.

TOGO
Togo wameshiriki fainali za Afrika mara 6 ambazo ni mwaka  (1972, 1984, 1998, 2000, 2002, 2006).Togo baada ya kushambuliwa na waasi katika fainali za Afrika zilizofanyika huko Angola walijitoa katika fainali za 2010, lakini hivi sasa wamerudi tena na wanatarajiwa kutoa ushindani mkubwa. Haijatwa Kombe la Afrika.

DR CONGO
DR Congo wameshiriki fainali za Afrika mara 15 ambazo ni mwaka (1965, 1968, 1970, 1972, 1974, 1976, 1988, 1992, 1994, 1996, 1998, 2000, 2002, 2004, 2006).

DR Congo ilishindwa kushiriki fainali hizo kwa muda wa miaka saba, lakini hivi sasa wameingia katika fainali hizo na wanatarajiwa kutoa upinzani mkubwa. DR Congo imetwaa ubingwa wa Afrika mara 2 (1968, 1974).

BURKINA FASO
Burkina Faso wameshiriki fainali za Afrika mara 8 ambazo ni mwaka (1978, 1996, 1998, 2000, 2002, 2004, 2010, 2012).

Burkina Faso imekuwa ikishiriki fainali za Afrika, lakini haijawahi kufika hatua ya robo fainali. Haijatwa Kombe la Afrika.

ALGERIA  
Algeria wameshiriki fainali za Afrika mara 14 ambazo ni mwaka (1968, 1980, 1982, 1984, 1986, 1988, 1990, 1992, 1996, 1998, 2000, 2002, 2004, 2010).

Kila mara Algeria imekuwa na kikosi bora, lakini ni mara moja tu katika fainali za Afrika imefika hatua ya nusu fainali. Algeria imetwaa ubingwa wa Afrika mara 1 (1990).

MTU anayeshukiwa kuhusika kumpiga risasi na kumuua aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow (53), amekamatwa na polisi mkoani Mwanza

MTU mmoja anayeshukiwa kuwa ndiye aliyehusika kumpiga risasi na kumuua aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow (53), amekamatwa na polisi mkoani Mwanza.Kamanda Barlow aliuawa kwa kupigwa risasi shingoni usiku wa manane wakati akimsindikiza mwanamke mmoja baada ya kuhudhuria kikao cha harusi ya ndugu yake.
 Mtuhumiwa huyo anaaminika kuwa ndiye aliyehusika na kumpiga risasi, na inadaiwa kuwa ana rekodi ya kuhusika na matukio mbalimbali ya uhalifu.
Ilielezwa kuwa mtuhumiwa huyo kabla ya kuhusika na mauaji hayo, alitoka jela miezi minne iliyopita.
 Habari za uhakika kutoka ndani ya jeshi hilo pamoja na timu ya makachero wanaohusika na uchunguzi wa mauaji hayo chini ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, zimeeleza kwamba, kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kumetegua kitendawili cha chanzo cha mauaji hayo na kubainisha kuwa hayahusiani na mapenzi.
 “Jana (juzi) ilikuwa ni siku muhimu kwa Jeshi la Polisi, mtu muhimu sana katika sakata la mauaji hayo alikamatwa, huyu kwa mujibu wa rekodi zetu anaonekana kuhusika na matukio kadhaa ya ujambazi na kabla ya ya mauaji ya kamanda wetu alikuwa jela,” kilieleza chanzo chetu.
 Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo,  kunafanya waliokamatwa hadi sasa kufikia sita akiwamo Mwalimu Dorothy Moses.
 Imeelezwa kwamba kupatikana kwa mtuhumiwa huyo, maelezo ya awali ambayo yalitolewa na Mwalimu Dorothy Moses pia yamebadilika kutokana na kuonekana ni mmoja wa watu wa karibu na mtuhumiwa huyo na kwamba zipo dalili za kuhusika katika njama hizo za mauaji.
 Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Lili Matola alikiri kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, lakini hakutaka kuingia ndani kwa madai ya kwamba hiyo ilikuwa ni kazi ya DCI Manumba anayehusika na upelelezi huo.
 “Naomba muwe na subira, mambo ni mazuri, kwani hatua za upelelezi wa mauaji ya Kamanda Barlow umefikia hatua nzuri, hayo mnayosema baadhi ni sahihi, lakini mengine nami nayasikia, ila tu la muhimu tuvute subira kwani ukweli wote utatangazwa,”alieleza.
 Kutokana na uchunguzi huo kuingia katika hatua muhimu, ilielezwa kwamba DCI Manumba aliwasiliana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, (IGP) Said Mwema ambaye aliwasili jana jijini Mwanza.

Baadaye Mwema  aliiwasilisha ripoti ya kukamatwa kwa mtuhumiwa katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama cha Mkoa wa Mwanza chini ya Mkuu wa Mkoa Mhandisi Evarist Ndikilo.
chanzo -mwananchi

Friday, October 26, 2012

AIRTEL WAZIDI KUPAGAWISHA WATEJA WAKE

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, imezindua ofa ya kuongea bure mara tano ya wastani wa matumizi ya kupiga simu kwa siku nzima, kwa wateja wake nchini
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Sam Elangalloor, alisema wametoa ofa hiyo kwa wateja wao kwa wastani wa kiwango cha fedha watakayotumia kila siku.
Alisema wateja watatumia bonasi hiyo ya muda wa maongezi,kupiga simu kwenda mtandao wowote  kwa siku hiyo.
”Tumefanya hivi ili kuendelea kuboresha huduma zetu na pia kuendelea kudhibitisha dhamira yetu ya kuwapatia wateja wetu nchini nzima, uhuru wa kuongea,” alisema Elangalloor.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Beatrice Singano, alisema mteja anayetumia mtandao huo ameshaunganishwa katika bonasi hiyo na kwamba kinachotakiwa ni kupiga simu ili apate salio la bure mara tano kwa wastani wa matumizi yake.
“Kadri mteja anavyotumia simu yake kwa kupiga simu, ndivyo atakavyojipatia  nafasi  zaidi ya kuzawadiwa asilimia 500 ya bonasi ya muda wa maongezi bure,”alisema.

 “Mfano mteja anaweka vocha ya Sh 500 kwa siku nzima, hivyo akatumia na kuisha saa 6:00 mchana muda huo atapewa bonasi ya maongezi ya bure ambayo itakuwa mara tano ambapo ataongezewa salio la Sh2,500 litakalotumika siku hiyo kabla ya saa 6 usiku”alisema Singano

Thursday, October 25, 2012

SASA ni dhahiri kwamba matokeo ya uchaguzi wa UVCCM, yameigawa jumuiya hiyo,Kifo alichotabiri J.K chanukia.

ZAIDI YA 300 WASAINI KUPINGA MATOKEO,MAKONDA ANENA, AAPA KUTORUDI NYUMA
SASA ni dhahiri kwamba matokeo ya uchaguzi wa Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), yameigawa jumuiya hiyo na huenda ikajikuta kwenye mgogoro mkubwa wa kiuongozi ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa.
Hali hiyo inatazamwa na baadhi ya wachunguzi wa mambo kwamba ni kutimia kwa utabiri wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete ambao aliutoa wakati akifungua mkutano huo kwamba lazima viongozi watakaochaguliwa wachukue hatua za kuondoa nyufa zitakazotokana na uchaguzi huo.
Kadhalika, Rais Kikwete aliwaambia UVCCM kwamba watajuta ikiwa watachagua viongozi wasio na uwezo kutokana na kushawishiwa na rushwa, kauli ambayo hata hivyo, vijana hao waliipuuza kwani uchaguzi huo ulidaiwa kugubikwa na vitendo hivyo hali iliyozua malalamiko kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa mkutano.
Wasiwasi wa kupasuka kwa UVCCM unatokana na wanaodaiwa kuwa wanachama wa jumuiya hiyo 379 wengi wakiwa wajumbe wa mkutano mkuu, kusaini tamko la kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi wa nafasi ya mwenyekiti, Mbunge wa Donge, Sadifa Juma Khamisi na Makamu wake Mboni Mhita.
Kadhalika, hofu ya kukua kwa ufa huo, inatokana na ukimya wa aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Paul Makonda juu ya nafasi ya kuteuliwa kwake na Sadifa kuwa mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM.
Tofauti na mgombea mwenzake, Rashid Simai Msaraka aliyekubali uteuzi uliofanywa na Sadifa kumpa ujumbe wa baraza, Makonda hadi sasa hajaukubali wala kuukataa, ukimya unaotafsiriwa kuwa unaweza kuwa na ajenda kubwa ndani yake.
Hata hivyo, Makonda alipozungumza na Mwananchi jana alisema atatoa uamuzi wake baadaye pale atakapozungumza na vyombo vya habari kuhusu yaliyojiri katika uchaguzi wa UVCCM.
“Kwa sasa siwezi kusema nimekubali uteuzi huu au hapana, ninafanya hivi kwa sababu kama ulinisikia jana (juzi) nilisema uongozi tuliouchagua ni aina ya jumuiya tunayoitaka, sasa ni aina gani hiyo, nitazungumza na baada ya hapo nitatoa sababu za kukubali au kukataa uteuzi wa Sadifa,”alisema Makonda na kuongeza:
“Leo hii nikisema nakubali uteuzi huo, basi wapo watakaosema nimehongwa au nimerubuniwa, lakini pia nikisema naukataa wapo watakaosema nina uchungu wa kukosa uongozi, sasa subiri tu siku nikisema nakubali au nakataa nitatoa sababu”.
Gazeti hili jana lilipomtaka Makonda atoe ufafanuzi wa kauli yake aliyoitoa juzi alisema: “Unawezaje kujivuna kwamba wewe ni mshindi wakati dhamiri yako ikijua kwamba ulitumia hila, fedha na ulaghai, huwezi kuwa na confidence (kujiamini) hata kidogo, sasa mtu asiyejiamini hiyo ni fedheha.”

Kwa upande mwingine, kundi la vijana wanaoongoza harakati za kutaka matokeo hayo yatenguliwe, jana liliwasilisha Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, baadhi ya vielelezo kuhusu kuwapo kwa vitendo vya rushwa katika uchaguzi huo.
Taarifa zinasema  kundi hilo linaanda barua na kiambatanisho cha majina na saini za wanachama wa UVCCM 379 ambao mpaka sasa wamesaini tamko la kupinga matokeo ya uchaguzi huo kupeleka kwa uongozi wa CCM.
Mmoja wa maofisa wa CCM makao makuu mjini Dodoma ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe aliliambia gazeti hili kuwa: “Ni kweli wale vijana wameleta sehemu ya ushahidi wao na tumeupokea, ila tumewaelekeza kwamba lazima waandike barua ya malalamiko na iwe imefika sehemu husika katika muda wa siku 14 tangu kutangazwa kwa matokeo”.
chanzo -gazeti la mwananchi

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Bafana Bafana, Gordon Igesund, amesema timu yake tayari imefikia asilimia 75 katika maandalizi yake kupambana katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

Bafana Bafana
Kocha wa Bafana Gordon Igelsund anasema timu hadi sasa imefikia asilimia 75 ya uwezo wake kamili
Afrika Kusini ni wenyeji wa mashindano hayo ambayo yatafanyika mwezi Januari mwaka 2013.
Bafana Bafana waliendelea kuonyesha uwezo wao, walipoishinda Kenya siku ya Jumanne, magoli 2-1, katika mechi ya kirafiki.
"Cha kunifurahisha hasa sio ushindi huo, bali ni kuhusiana na juhudi, namna walivyocheza, na mtizamo wa timu," alielezea Igesund.
"Bado hatujafika, kwani tunahitaji kucheza kwa pamoja - lakini vijana walionyesha uwezo wao."
Afrika Kusini ilitangulia katika mechi ya Nairobi kupitia Tokelo Rantie baada ya dakika 20, lakini Dennis Oliech aliweza kusawazisha kupitia penalti, na zikiwa zimesalia dakika 18 tu mechi kumalizika, kufuatia Bongani Khumalo kuunawa mpira.
Dakika nne baadaye, Bernard Parker ambaye awali alisaidia kutumbukiza wavuni bao la kwanza, alisaidiwa na Christopher Wekesa ambaye mpira ulipomgonga ulibadilisha mwendo na kuelekea wavuni na kuiwezesha Afrika Kusini kushinda.
Bao hilo la kujifunga wenyewe dakika ya mwisho linamaanisha kocha mpya wa Kenya, Henri Michel, ameanza kazi yake mpya kwa kushindwa.
"Ilikuwa ni ushindi uliopatikana kwa shida, na uwanja ulikuwa hauchezeki, lakini ni matatizo kama hayo ambayo yatatusaidia kimawazo," alieleza Igesund.
"Tulicheza kwa kuzingatia asilimia, na wala sio mchezo maridadi, katika kuwasukuma hadi wafanye makosa.
"Ninasikitishwa tu na bao ambalo tulifungwa, hatupaswi kuruhusu timu kutufunga magoli kama hayo. Lakini kwa jumla ilikuwa ni mazoezi mazuri, tukifikiria tulikusudia kufanya nini.
"Kwa sasa tumefikia asilimia 75 ya yale tunaweza kuyafanya."
Mwezi Januari, kwa mara ya kwanza, tangu fainali za mwaka 2008, itashiriki tena katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, baada ya kutokuwepo katika mashindano ya mwaka 2010 na 2012.
chanzo bbc.com

Muungano wa Afrika umeiruhusu tena Mali kuwa mwanachama baada ya kusimamisha kwa muda uanachama wake mwezi Machi kufuatia mapinduzi ya kijeshi.

Mali yarejea kwenye Muungano wa Afrika

                                                 Waasi Kaskazini mwa Mali
Muungano wa Afrika umeiruhusu tena Mali kuwa mwanachama baada ya kusimamisha kwa muda uanachama wake mwezi Machi kufuatia mapinduzi ya kijeshi.
Muungano huo pia umeidhinisha mpango wa Mali kuitisha uchaguzi mkuu na kuirejesha nchi katika hali ya utulivu , kwa mujibu wa msemaji wa AU.
Maafisa wa Muungano huo pia wamekuwa wakijadili mipango ya kutuma vikosi vya jeshi kusaidia wanajeshi wa Mali kudhibiti maeneo yaliyotwaliwa na wapiganaji wa kiisilamu Kaskazini mwa nchi.
Eneo hilo lilitwaliwa na waasi baada ya vurugu zilizotokea katika mji mkuu, Bamako mwezi Machi.
''Baraza la usalama na ulinzi la Umoja wa Afrika, uliamua kuirejesha Mali kwenye uwanachama wake na kwa hivyo nchi hiyo inakaribishwa kushiriki kikamilifu.'' alisema Ramtane Lamamra, msemaji wa baraza hilo .
AU pia inakamilisha mipango yake ya kutuma vikosi vya wanajeshi wa Afrika nchini Mali kulingana na mwenyekiti wa tume ya AU Nkosazana Dlamini-Zuma.
''Hata hivyo, serikali itatoa fursa kwa wapiganaji ambao wanataka kufanya mazungumzo nayo.'' aliongeza Bi Zuma.
Mapinduzi ya mwezi Machi, yalifanywa na wanajeshi waliopindua serikali ya Rais Amadou Toumani Toure, wakidai kuwa serikali yake ilikosa kukabiliana vilivyo na waasi wa Tauareg.
Baada ya mapinduzi , wapiganaji wa kiisilamu walidhibiti miji ya Kaskazini mwa Mali wakishirikiana na waasi wa Tuareg, lakini ushirkiano wao ulivunjika.
Mapema mwezi huu, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, lilipitisha azimio la kuruhusu jeshi kuingilia hali nchini Mali na kuyataka mashirika ya Afrika kubuni mkakati wa jeshi la pamoja katika muda wa siku arobaini na tano.

NSSF yazitaka Man U, Chelsea, Madrid KUWEKEZA HAPA NCHINI KATIKA MICHEZO

SHIRIKA la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limeanzisha mchakato wa kujenga kituo cha kuibua vipaji vya soka nchini kwa kutumia jina la klabu mojawapo kubwa ya barani Ulaya.
Mkurungenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau, aliiambia Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), jana kwamba, kwa sasa wapo katika mazungumzo na timu kubwa za Real Madrid ya Hispania, Manchester United, Liverpool na Chelsea za England.
Dk. Dau alisema katika mazungumzo na timu hizo, itakayokubali kuingia ubia, wataialika kuja nchini kuangalia eneo zuri la uwekezaji huo.
Alisema ubia huo utahusu namna ya kusaidia kufundisha jinsi ya kuwekeza katika mchezo wa soka na hatimaye vipaji viweze kuibuka na kuunda timu hapa nchini, itakayotumia jina la NSSF na timu watakayokuwa wameafikiana nao.
Dk. Dau alisema baada ya kuanzisha kituo hicho na kupatikana kwa timu hiyo, itakuwa ikipata faida ya kufunguliwa mafao yote ambayo yanatolewa na NSSF.
Na katika hatua nyingine, Dk. Dau alisema watafikiria kuwapa uanachama katika fao la bima ya afya, timu ya taifa ya soka Tanzania, Taifa Stars ili iweze kufanya vizuri zaidi.
Kauli hiyo aliitoa baada ya Mwenyekiti wa POAC, Zitto Kabwe, kuuliza kama Taifa Stars inapata fao hilo na kama haipati, je kuna uwezekano?

MADIWANI wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika Manispaa ya Moshi, Kilimanjaro juzi walitwangana makonde,Mwenyekiti Chadema achomwa mkuki

MADIWANI wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika Manispaa ya Moshi, Kilimanjaro juzi walitwangana makonde huku kiini kikitajwa kuwa ni gari la Mstahiki Meya.
Tukio hilo linadaiwa kutokea juzi katika moja ya kumbi za mikutano ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakati madiwani hao wakiwa katika kikao cha ndani cha maandalizi ya mkutano wa baraza la madiwani.
Hata hivyo, licha ya taarifa za tukio hilo kuzagaa haraka, wahusika wameifanya siri ili kulinda heshima ya chama hicho.
Inadaiwa kuwa kisa cha kupigana ni ubishi juu ya nani anastahili kupanda gari hilo la Meya na baada ya kurushiana maneno, madiwani hao walivaana na kuanza kupigana kabla ya kuamuliwa na wenzao.
Habari zinadai kuwa madiwani watatu wamekuwa wakilitumia gari la Meya kila wanapolihitaji bila kikwazo jambo ambalo limekuwa likiwakera baadhi yao.
Mwenyekiti wa Madiwani wa CCM katika Baraza hilo, Michael Mwita amekiri kuarifiwa juu ya tukio hilo lakini hakulishuhudia akisema alikuwa katika ukumbi mwingine.
Meya wa Manispaa ya Moshi, Jaffar Michael hakupatikana kuzungumzia tukio hilo kwani tangu juzi, simu yake imekuwa ikiita bila kupokewa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Bernadette Kinabo alisema amesikia kutokea kwa tukio hilo.
Alisema tukio hilo limemsikitisha na kuwataka madiwani kuhimili jambo hata kama ni kutukanwa... “Nimearifiwa juu ya jambo hilo japo si kwa undani sana. Ila kwa kweli madiwani wanapaswa kujiheshimu ili na wengine wajifunze kutoka kwao. Haipendezi madiwani kutumia lugha ya kuudhi zaidi yao na anayetolewa lugha hiyo naye lazima azuie jazba.”

Mwenyekiti Chadema achomwa mkuki

Mwenyekiti wa Chadema, Tawi la Mwawaza, Shinyanga, Bundala Katunge amechomwa mkuki baada ya kuvamiwa na
kushambuliwa na kundi la watu zaidi ya 30.
Tukio hilo lilitokea juzi katika Kijiji cha Mwawaza saa tano usiku akiwa amelala nyumbani kwake.
Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa Katunge alijeruhiwa baada ya kutoka nje ya nyumba yake mara baada ya kusikia bendera ya Chadema ikishushwa kwenye mlingoti.
Ilidaiwa kuwa alijaribu kuwazuia lakini walimzidi nguvu na kuanza kumshambulia. Aliwaponyoka na kuanza kukimbia ndipo mmojawao alipomrushia mkuki na kumchoma sehemu za mbavu upande wa kushoto. Baada ya tukio hilo  kundi hilo lilitoweka.
Katibu wa Chadema Wilaya ya Shinyanga, Nyangaki Shilungushela alisema Katunge alikimbilia kwa majirani ambao walimpeleka katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga ambako alifanyiwa upasuaji na kulazwa akisema hali yake ni mbaya.
Mganga Mfawidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Frederick Mlekwa alikiri kuwapo kwa mgonjwa huyo na kusema anaendelea kupatiwa matibabu.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangala alisema hana taarifa ya tukio hilo.
Hata hivyo, wananchi wa eneo hilo walisema jana kwamba tangu tukio hilo lilipotokea, hawajaona polisi aliyefuatilia licha ya kutoa taarifa na kupewa fomu namba tatu iliyowezesha matibabu ya kiongozi huyo wa Chadema.
“Tunashangaa ni kwa nini polisi hawajatoa ushirikiano na huku taarifa wameshazipata,” alisema mmoja wa wakazi wa kijiji hicho ambaye hakutaka jina lake litajwe.
CHANZO GAZETI  LA MWANANCHI

Wednesday, October 24, 2012

Matokeo ya uchaguzi wa uvccm yalikuwa hivi na jua watuhumiwa walichokisema

Lukuvi alimtangaza Mbunge wa Donge, Sadifa Juma Khamisi kuwa Mwenyekiti wa UVCCM baada ya kupata kura 483.
Sadifa alimshinda Rashid Simai Msaraka aliyepata kura 263, wakati mgombea mwingine Lulu Msham Abdallah licha ya kujitoa katika kinyang’anyiro hicho muda mfupi kabla ya kura kupigwa, alipata kura nane.
Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti Mboni Muhita alishinda katika duru ya pili baada ya kupata kura 489 na kumshinda, Paul Makonda aliyepata kura 241.
Katika duru ya kwanza, Mboni alikuwa amepata kura 361 na Makonda kura 206, huku mgombea mwingine Ally Salum Hapi akipata kura 179. Uchaguzi huo ulirudiwa baada ya wagombea wote kutofikisha nusu ya kura kama kanuni zinavyotaka.
“Sheria kushindwa kwa heshima kuliko kushinda kwa fedheha.”
Makonda aliyekuwa akizungumza kwa hisia jukwaani alisema ikiwa UVCCM wanataka kujenga taasisi yenye nguvu na inayoaminika, lazima wahakikishe wanajiepusha na vitendo vya rushwa ambavyo vinaua demokrasia.
“Uchaguzi tulioufanya hatukumchagua Sadifa wala Mboni, bali tumechagua uongozi wa aina ya jumuiya tunayoitaka, sasa tutarajie jumuiya hiyo…. kama sikueleweka historia itakuja kutuambia maana ya maneno haya,” alisema Makonda na kuongeza:
“Kama kuna mtoto wa maskini, mtoto wa mkulima kama mimi amechagua au kupiga kura yake kwa sababu ya rushwa, basi ajue amepanda mbegu maishani mwake.”
Baada ya Makonda kutoa kauli hizo alishuka jukwaani na kwenda moja kwa moja nje ya ukumbi ambako baadhi ya wapambe wake walimfuata na kuanza kulia machozi.
Baadhi yao walisikika wakisema kwamba UVCCM wameisaliti demokrasia kutokana na nguvu ya fedha. Hata hivyo, Makonda alikuwa akiwafariji kwa kuwaambia wasife moyo.
  WATUHUMIWA WAJITETEA HIVII
Kwa nyakati tofauti, wakijibu tuhuma hizo watuhumiwa wote walikanusha kuhusika kutoa rushwa na kuwataka wanaolalamika kupeleka ushahidi wao Takukuru na kufikisha malalamiko hayo katika vikao vya ulinzi na maadili vya CCM.
Shigela kwa upande wake, akizungumza na waandishi wa habari alisema kinachotokea sasa kuhusu tuhuma hizo kilitarajiwa kwani ni kawaida watu wanaposhindwa katika uchaguzi kutoa malalamiko hata kama hawana ushahidi wa tuhuma husika.
Shigela alikanusha yeye na Malisa kutoa fedha kwa viongozi wa mikoa akisema kwa nafasi yake asingeweza kupata fursa ya kufanya hivyo kwani alikuwa mratibu mkuu wa uchaguzi kuhakikisha kila jambo linakwenda sawa.
“Kama kuna watu hawakuridhika kuna taratibu za chama inabidi zifuatwe, kwa mujibu wa taratibu zetu kuna siku 14 za malalamiko na hizo mtu anaweza kuzitumia kuandika malalamiko yake na yapelekwe kwa viongozi wahusika ili wachuke hatua,” alisema Shigela na kuongeza:
“Vinginevyo taratibu za chama haziruhusu kutoa au kupokea rushwa kwa namna yeyote, kwa hiyo kama mtu anadhani ana uwezo aitumikie jumuiya popote pale alipo kwa sababu wote hatuwezi kuwa viongozi kwa pamoja.”
Kwa upande wake, Malisa alisema: “Nimefanya kazi yangu na kutekeleza wajibu wangu kwa ukamilifu, kama kuna jambo lolote ambalo linahusu UVCCM, basi kamuulizeni mwenyekiti wa jumuiya maana yupo.”
Bashe alikanusha kuhusika na vitendo vya rushwa na kuwataka wanaotoa madai hayo, kama wana ushahidi waupeleke Takukuru au kufikisha suala hilo katika vikao vya chama hicho.
“Waambieni kwamba wasilete siasa za shule za sekondari UVCCM, maana kama wangeshinda ni dhahiri kwamba wasingelalamika. Ninawapa ushauri wa bure, kwanza kama wana ushahidi wa madai hayo kwamba mimi Hussein nimetoa rushwa, basi wapeleke ushahidi wao Takukuru lakini pia ndani ya chama tunayo Kamati ya Maadili na Usalama wapeleke malalamiko yao huko ili yafanyiwe kazi.”
Alisema hawezi kujihusisha na rushwa kwani hata Rais Kikwete katika hotuba ya ufunguzi alikemea vitendo hivyo.
Fredy akizungumza kwa simu alisema: “Tuhuma hizo siyo za kweli kwani mimi licha ya kwamba nilipata barua ya mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo sikuenda Dodoma kutokana na kubanwa na kazi.
“Kwanza mimi si mjumbe wa mkutano mkuu japokuwa ni Katibu wa Uhamasishaji wa Mkoa wa Arusha. Nilipata mwaliko lakini sikuweza kufika huko (Dodoma) nimetingwa na kazi nyingi,” alisema.

Yaliyojiri dodoma katika uvccm na wasemavyo vijana katika mitangao ya kijamii,facebook,twitter etc

Uchaguzi Wa Uvccm Taifa Uliofanyika Jana Uligubikwa Kwa Rushwa yaani Viongozi waliochaguliwa hawana Uwezo Na Sifa,Neno Langu La Mwisho CCm Inaelekea Kubaya Katika Hali Mbaya Huo Ndyo Ukweli Kamili.Bila Uvccm Imara,CCM itayumba na Nchi Pia....Namnukuu Hayat Baba wa Taifa Katika Mkutano Mkuu wa CCM mwaka 1995 Watanzania wanahitaji mabadiliko,wasipoyaona Ndani Ya CCm watayatafuta Nje Ya CCM,Pia watanzania wanaichukia sana Rushwa na Viongozi wanaochaguliwa kwa Rushwa
Like · ·
  • Masudi Kuseka mie hapa mpaka kichwa kinauma.mambo ya ukambi
  • Grace Shindika Vp mtu wako ulompigia bede kashindwa???jipe moyo tuondoe hayo na tuendeleze chama,,,coz acekubal kushindw c mshindani
  • Mathew Mfinanga James tulikuambia unania njema na kundi lako ila ndani ya ccm watu wema hawapenyi,lazima uwe mchawi au uwe na pesa ya kununua watu,
    cjaamini hadi sasa paul makonda kupigwa chini.
  • James Rock Mwakibinga Hatuwezi kuvumilia tatizo la rushwa likiendelea madaraka yamekuwa yakinunuliwa hali hii itaisha lini@Irene,kwa hili usiingilie kabsa yaani usinikasirishe unajua mm simwogop mtu ,bala nawaheshimue tu haya yote yanayofanywa kisa Lowassa mwizi anayumbisha ccm na Jumuiya zake....Wewe ngoja tu Watanzania si wa jinga tena,wana ccm labda ndyo wakunuliwa hili watu wapate madaraka,Tumechoka tunahitaji mabadiliko ya watoto wa kimasikin nao kupata nafasi kuongoza
  • Albert Alex Ibrahim Niliwahi kukuambia kaka kamwe huwezi kuiongelea Rushwa ukiwa umevaa Green.,!.,Sasa umedhihirisha mwenyewe Rushwa ndio sera ya CCM.,Na ina baraka zoote.,Kiukweli Vijana Tumekwisha no way...!
  • Amoni Geofrey Kitundu mm nahic mtu ameiba pasword ya james ndo akapost hii status mana huyu siye jems ninayemfahamu.Kama ni yeye basi Naomba Mungu azidi kumfunulia zaid na zaid kama sisi alivyotufunuliaga mapema tukahama ccm,Naamn nafasi bado ipo ya james kuchukua maamuz sahihi
  • Balozi Jacob JaJu mi kwasasa siwezi kuwalaumu waliochaguliwa bali NTAKUFA NA WAJUMBE,KWANI WAO WALIFUMBWA AKILI,HUU NI UJINGA WA MWISHO KULIKO MAUJINGA YOTE,UNAPIGA KURA KWA MTU KWA VILE KAKUPA FEDHA,MIMI NINGECHUKUA FEDHA NA KURA NINGEELEKEZA KWENGINE ILIMRADI TU NISICHAGUE KIONGOZI ZUZU
  • Sophie Kessy na huo ndio ukweli nakwambia wasipo yaona ndani ya CCm watayatafuta nje ya CCM na wanaona wanasikia na wanajua wanacho kitaka
  • Albert Alex Ibrahim Kaka tumechoshwa na Ushenzi wa Kiburushwa na Vibaraka wa Lowassa....!,Nakuinbox nn tufanye vijana ndani na nje ya CCM,kabla ya 2015
  • Masudi Kuseka we mwenyewe ulimsikia RAIS alivyokuwa analalamika kwamba uchaguzi wa UWT TAIFA uligubikwa na rushwa wakati kabla ya huo uchaguzi wa UWT TAIFA, TAKUKURU walisema wamedhitibi RUSHWA na hakukuwa na Rushwa,sasa huyo RAIS wetu kaambiwa na nani kama kulikuwa na Rushwa katika uchaguzi wa UWT TAIFA.sasa nani muongo KATI YA TAKUKURU NA RAIS?
  • Loma Kivuyo Hv kwel huyu james rock nnayemfaham au n m2 anatumia acount yake? Ktk post zake nyng nazsomaga 2 na kutochangia chochote ila cku 1 alnkera sana kwa kuifagilia ccm na kuponda CHADEMA ila ya leo kal cc w M4C tulyaona hayo mapema ndo mana tukaseba kimiakimia
  • Irene Msellem hakuna anaekutisha wote walikuwa na vigezo vilivyowawezesha kufikia hatua ya fainali. sasa wewe ulitaka nani ashindwe wote ni ccm wenzio tumkubali alieshinds. uvccm haiwezi kufa kwa makonda kushindwa. ajipange upya miaka minne sio mingi@James
  • Elijah Samson Mwakilindi James Rock mwakibinga, uyaonayo sasa tuliyaona mapema, fanya maamuzi magumu kaka.
  • Ayoub Yusuph-Mwanaharakati Wajumbe ndio wenye matatizo tena makubwa ndio maana jana nilisema mfumo wa uchaguzi ubadilike badala ya wajumbe wachache kwenda kuchagua viongozi ni bora kila mwanachama apate nafasi ya kuchagua mtu anayempenda na anaeona anafaa.Vijana wote wa UVCCM ndio walitakiwa kuwachagua viongozi wao na si kundi la wachache
  • Masudi Kuseka Lowassa is our next Prezidaaa.mkatae au mkubali, KIDUMU CHAMA TAWALA CCM.KIDUMU CHA MAPINDUZI CCM.
  • Balozi Jacob JaJu Irene,hata mimi namuunga mkono james kwasababu moja,wote walikuwa na nafasi ya kushinda,hofu na tatizo letu limetokana na namna ushindi wa huyu mwenzetu ulivopatikana,yani kama ni mahakamani ni kwamba watu walifanya maamuzi wakiwa hawana akili timamu,yaani wakifurahia fedha badala ya kumfurahia kiongozi
  • Mtela Mwampamba Nani kashinda ndugu zangu?
  • Jestina George It's about time watu wakaongea ukweli asante sana James Rock Mwakibinga na Mungu akulinde kwa hili. Inatia aibu na kusikitisha sana
  • Sule Junior Hahahahahaha! Hyo ndio ccm mdgo wangu James!
  • John W. Jacob Kuna cku nilimwambia James Kuwa "TIME WILL TELL" Thats what i meant. Sasa rushwa na umakundi ndani ya ccm are INSEPERABLE COMPANIONS. Viva M4C Viva.
  • Florah Nkondola Amon No comment ila mwakibinga ulijiamin c kawaida,mwacheni mwanamke afanye kazi m2 hajaanza kazi mnaanza kulalamika wanawake wanaweza banaha me ila cna chama zaidi ya chakabila ye2 wanyasa bhaaaaass
  • Agustino Chacha Dawa si kukimbia tatizo bali ni kukabiliana nalo kilichopo mbele ye2 ni kuhakikisha 2napinga kwa dhati rushwa ndani ya chama kama 2taendelea kuweka viongozi ambao hata kujitambulisha wao wenyewe ni tatizo basi Mungu ibariki CCM@James.
  • Salome Steeve Nilikuwa nasubiri post ya namna hii kutoka kwako mpigadebe mashuhuri,kama kulikuwa na rushwa si mngezuia uchaguzi usifanyike, kwi kwi kwi hahahahahahahahahahaaaa bonyeza kizenji wahenga walisemaaaaaa asiyekubali kushindwa si mshindani
  • Waridy Peter James .james james. Mwakibinga
  • Witness Peter i like ur post James!
  • Hamis Pembe Ushauri wangu achana na siasa ndugu yangu maana hata ukienda huko kwingine mambo ni hayo hayo ndo mfumo wa siasa katika nchi ulioasisiwa na chama hiko hiko unachokipenda ndio ulivo kama huna kitu uctegemee chotechote.

  • Florian Sospeter Muchunguzi Pole kwani ulikuwa ujui au baada ya kushindwa ndo rushwa inaibuka
  • Florian Sospeter Muchunguzi CCM NI PESA TU BILA PESA IMEKULA KWAKO(chukua chako mapema-CCM)
  • Florah Nkondola Amon Bwana wee safari hi walikuwa wanataka M/m uvccm mwanamke kama ilivyokuwa kwa spika mwa 2010,kwi kwi kwi kwi me thithemi
  • Getrude Kokwenda Ndibalema Nimezid kukupenda james kwa kuongea ukweli juu ya hata pale unapopapenda..
  • Simba Roine acha kulalamia kaka....! kushindwa wewe ndo ushindi wa wenzio
  • Gabriel Gregory Ishole kwa sababu Makonda hajachaguliwa?.Tukubali matokeo dogo na hiyo ndiyo siasa
  • Said Noyi Polen sn bt hyo ndo siasa ndgu yangu we jipange 2.
  • Isaac Kitogo James Rock Mwakibinga, take time kutafakari kwanza, kumbuka hao waliopitishwa ngazi zote za vikao vya chama ziliona wanafaa na wanauwezo wa kuwa viongozi ndiyo maana wakapewa nafasi ya kushindana. labda kwanza uhoji vikao vyote vya uteuzi ndani ya cham...See More
  • Mathew Mfinanga Kueleza isia zako za ndani kwa uliyoyaona cyo udhaifu,sumaye alieleza anayoeleza james na pia jk akifungua mkutano alieleza hayo hayo je,nao ni wadhaifu hawajakubaliana na matokeo?
    Tusidanganyane ndani ya ccm hakuna haki hata kidogo.White hair amewanunua.
  • Jofrey Kamwava pole kaka umeangukia pua nini? mbona maneno mengi sana................