Saturday, November 17, 2012

Arsenal yaipepeta Tottenham 5-2

Wachezaji wa Arsenal wakisherehekea  bao lao
Wachezaji wa Arsenal wakisherehekea bao lao
Arsenal leo imeilaza Tottenham kwa magoli 5-2 katika mechi ya kusisimua iliyochezwa katika uwanja wa Emirates.
Arsenal ilitumia fursa ya kuondolewa kwa mchezaji wao wa zamani Emmanuel Adebayor, kuwalemea majirani wao.
Adebayor alipewa kadi nyekundi baada ya kumfanyia madhambi, Santi Carzola muda mfupi tu baada ya kuifungia Tottenham bao lake la Kwanza.
Dakika nne baadaye, Per Mertesacker akaizawazishia Arsenal kabla ya Luka Podolski na Oliver Giroud kuongeza la pili na tatu kabla ya muda wa mapunziko.
Hata hivyo Tottenham ilipata bao lake la kufutia machozi kupitia kwa mchezahi Gareth Bale.
Theo Walcot naye akaifungia Arsenal bao lake la tano.
Ushindi wa leo ni wa kwanza kwa Arsenal tangu tarehe 27 October.
Akizungumza baada ya mechi hiyo kocha wa Tottenham Andre Villas-Boas, amesema mwenyekiti wa klaby hiyo Daniel Levy alikuwa amekariri kuwa ni muhimu wa klbau hoyo kushinda mechi ya leo.
Lakini wito huo ulionekana kutumbukia nyongo tu mara nyota wake Adebayor alipopewa kadi nyekundu.
Arsenal sasa imepanda hadi nafasi ya 6 na alama 19 kwenye msururu wa ligi.
Manchester United bado ingali kileleni na alama 27 ikifuatwa na Manchester City na Chelsea.

No comments:

Post a Comment