Friday, November 16, 2012

Airtel, Unesco kuzindua redio ya jamii

WAZIRI wa Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzundizi wa radio ya jamii katika kijiji cha Ololosokwani, kilichoko tarafa ya Loliondo, wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha.
Uzinduzi wa redio hiyo unafanyika kwa ushirikiano kati ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel na Shirika la Umoja wa Mataifa la UNESCO.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, alisema Airtel na Unesco inatimiza dhamira iliyojiwekea ya kuwafikia na kuzisaidia jamii zilizoko pembezoni hasa kinamama.
“Mradi huu utasaidia kupigana na kutokomeza changamoto za mila zilizopitwa na wakati zikiwemo ukeketwaji wa wanawake, elimu duni, imani za kishirikina, umaskini, unyanyasaji wa kijinsia, kukua kwa kasi kwa ugonjwa wa ukimwi na matatizo mengine,” alisema.
Akifafanua kuhusu ufungwaji wa mitambo hiyo ya radio, Ofisa Mradi wa Habari na Mawasiliano UNESCO, Yusuph Al Amin, alisema mradu huo umekamilika na kuishukuru Airtel na wananchi wote kwa ushirikiano.
Sehemu nyingine zitakazonufaika na mradi huo wa radio jamii ni Sengerema (Mwanza), Karagwe (Kagera), Chakechake (Pemba), Makunduchi (Unguja), Pangani (Tanga), Kyela (Mbeya) na Kahama (Shinyanga).

No comments:

Post a Comment