Wednesday, November 28, 2012

MZEE MAJUTO AZIRAI MSIBANI,SHARO ALIKUWA MANAGER WA MZEE MAJUTO

MMOJA wa watu waliokaribu sana na marehemu Sharo Milionea, Mzee Majuto jana alizirai msibani wakati mwili wa marehemu ukiwa njiani kuletwa nyumbani kutoka hospitali tayari kwa mazishi.
Majuto ambaye kwa wakati fulani alionekana kujitahidi kuwa imara, alijikuta akichotwa na hisia kali na kudondoka chini na kisha kupoteza fahamu kwa dakika kadhaa.
Hatimaye baada ya juhudi ningi za kumpepea, Mzee Majuto alizinduka na kupumzishwa kando ili aweze kurejea katika hali ya kawaida.
Akiongea na Saluti5 baadae, Mzee Majuto alisema kifo cha Sharo kimemuumiza sana “Nahisi kama nusu ya mwili wangu umechukuliwa, ni mtoto mdogo lakini alikuwa rafiki yangu sana, alikuwa zaidi ya mwanangu” alisema kwa uchungu mzee Majuto.
Kwa miaka ya hivi karibuni Mzee Majuto na Sharo Milionea wamekuwa ndio wasanii wanao-oana zaidi kikazi kiasi cha kupelekea makampuni kadhaa kuwatumia kwenye matangazo yao ya biashara.

No comments:

Post a Comment