Tuesday, August 27, 2013

Dk Slaa amjia juu Kinana

Katibu mkuu huyo wa Chadema pia alieleza kusikitishwa kwake na mapendekezo yanayotolewa na CCM kuhusu Katiba Mpya na kupingana na maoni ya Tume ya Katiba.
Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa ameelezea kusikitishwa kwake na kauli ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwamba chama hicho tawala kimekusanya maoni ya Katiba kwa Watanzania milioni mbili.
Akizungumza  jana kwenye mkutano wa hadhara wa kukusanya maoni ya Katiba, uliofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Turiani, Magomeni, Dar es Salaam Dk Slaa alisema: “Nimesikitishwa sana na kauli ya Kinana kwamba wamekusanya maoni ya Katiba yanayofikia milioni mbili jambo ambalo si kweli.”
Alisema Chadema wamekuwa wawazi kwa kufanya mikutano yao nchi nzima, lakini hawakuwahi kusikia CCM wamekusanya maoni  jambo ambalo alidai ni la ajabu kwa chama hicho kutaja idadi hiyo.
Akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), Dodoma juzi, Kinana alisema CCM kimekusanya maoni milioni mbili ya wanachama kuhusu Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba, mchakato unaoendelea kupitia mabaraza.
Alidai kuwa Kinana alisema uongo kwa sababu hakuwahi kusikia maoni hayo yakikusanywa kama Chadema kinavyofanya kwa kuzunguka nchi nzima.
“Sisi tunafanya mikutano yetu ya kukusanya maoni ya Katiba kwa uwazi, lakini CCM wanatangaza kwa wanachama wao kwamba wamekusanya maoni milioni mbili bila kueleza njia wanazotumia... “Chadema imefanya mikutano ya kukusanya  maoni nchi nzima na kufanya mikutano 48.”
Katibu mkuu huyo wa Chadema pia alieleza kusikitishwa kwake na mapendekezo yanayotolewa na CCM kuhusu Katiba Mpya na kupingana na maoni ya Tume ya Katiba akisema kinapinga mambo mengi ya msingi.
“Kuna mambo ya msingi ambayo yana masilahi kwa taifa na wananchi kwa jumla, lakini wao (CCM), wanataka yasiwepo kwenye Katiba na wanapingana na Tume,” alisema.
Baadhi ya mambo ambayo Dk Slaa aliyataja ni pamoja na ubaguzi, rushwa, dhuluma, vitisho na unyanyasaji ambayo alisema Rasimu ya Katiba imeyapa umuhimu kwa kuyatambua na kueleza kwamba hayapaswi kufanyika ili kulinda haki za wananchi.
“Ninasikitishwa na CCM kwamba kila jambo ambalo Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba ameona lina umuhimu kuwepo  kwenye Katiba wao wanapingana nalo kitu ambacho ninaona hawana nia  njema na maisha ya Watanzania na taifa kwa jumla,” alisema.
Aidha, Dk Slaa alizungumzia tukio la kukamatwa kwa Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe huko Iringa kwa madai ya kuvunja sheria kwa kuzidisha muda wa kufanya mikutano.

CCM yamvua uanachama kigogo

Dodoma. Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (Nec), jana iliridhia kumvua uanachama, Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki, Mkoa wa Mjini Magharibi, Mansour Yussuf Himid kutokana na kukiuka miiko ya chama hicho.
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma jana kuwa Mansour ambaye hivi karibuni alikuwa waziri katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), amefukuzwa uanachama kutokana na kukiuka mambo matatu.
Aliyataja mambo hayo kuwa ni kushindwa kutimiza malengo ya CCM na kutekeleza malengo ya uanachama, kushindwa kutekeleza wajibu wa uanachama na kukiuka maadili ya uongozi, kuikana na kuisaliti Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015.
Kutokana na uamuzi huo, Nape alisema Mansour hatakuwa na nafasi ya kukata rufani mahali popote kwa kuwa uamuzi uliofikiwa jana ni wa kikao cha juu cha mwisho.
Akizungumza na Mwananchi jana, Mansour alisema kwa sasa hawezi kuzungumza mengi kwani anahitaji muda wa kutafakari kutokana na uzito wa suala lenyewe.
“Ndugu yangu nashukuru sana kwa kunipigia simu. Ila ninahitaji muda wa kutulia kwanza. Nipe kama siku mbili au tatu hivi halafu nitaongea,” alisema Mansour, ambaye amekuwa Mwakilishi wa Kiembe Samaki tangu mwaka 2005.
Nec ilifikia uamuzi huo ikibariki mapendekezo yaliyotolewa na Kamati Kuu ya CCM upande wa Zanzibar iliyomvua uanachama kutokana na misimamo yake ya kisiasa na hasa suala la Muungano.
Mansour aliwahi kushika nyadhifa kadhaa ndani ya CCM ikiwamo ya ujumbe wa Halmashauri Kuu na Mweka Hazina wa chama hicho upande wa Zanzibar.
Kilichomponza
Kwa mara ya kwanza, tuhuma za Mansour zilifikishwa katika kikao cha Kamati ya Maadili ya CCM Zanzibar, kilichoketi Agosti 16, mwaka huu katika Ofisi za CCM Kisiwandui ambacho wajumbe wa kamati hiyo kwa kauli moja walitoka na azimio la kumfuta uanachama.
Suala hilo lilifikishwa Kamati Kuu ya CCM, Zanzibar Agosti 22, mwaka huu kupitia uamuzi huo na iliafiki. Kitendo cha Mansour kuingia kwenye Kamati ya Maridhiano ya Zanzibar inayoongozwa na mwanasiasa mkongwe Hassan Nassor Moyo ambayo imekuwa ikipigania Muungano wa mkataba ilichochea tofauti yake na makada wenzake wa CCM Zanzibar.
Kitendo cha kuungana na Mzee Moyo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharrif Hamad kupigia debe suala la Muungano wa Mkataba kati ya Tanganyika na Zanzibar kuliwakera makada wa CCM waliomchukulia kuwa anapingana na Katiba na Ilani ya CCM vilivyosimamia katika Serikali mbil

Tuesday, August 20, 2013

Butiku: Ningejua CCM itaingilia mchakato wa Katiba nisingeshiriki

Tanga. Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Joseph Butiku amesema asingekubali kushiriki katika Tume hiyo laiti kama angejua CCM ingeingilia mchakato huo.
 
Butiku ambaye alitoa kauli hizo kwa nyakati tofauti, wikiendi iliyopita kwenye Mabaraza ya Katiba ya Halmashauri ya Mji wa Soni, Lushoto na Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, alieleza kutokufurahishwa kwake na kitendo cha CCM kushinikiza maoni yake mbele ya mabaraza hayo.
Alilalamika kuwa kitabu cha mwongozo wa utoaji maoni kilichotolewa na CCM kinatumiwa vibaya kushinikiza maoni kwenye Rasimu ya Katiba Mpya.
“CCM imeandaa kitabu kizuri kweli kusaidia wanachama wake, tuliwaambia (Tume) hatukitaki; ni mwongozo kusaidia wanachama wake namna ya kutoa maoni, lakini kimekuwa kinatumika vibaya. Kinatumika kushinikiza maoni,” alisema Butiku.
Butiku ambaye ni mwanachama wa Tanu tangu mwaka 1958 na CCM kuanzia 1977 alisema: “Ningejua itatokea chama kitafanya hivyo, nisingekula kiapo nilichokula kufanya kazi hii katika Tume ya Marekebisho ya Katiba. Kundi moja lisigeuke Tanzania. Mimi ni mzee nasema kitu kikubwa nataka Mwenyekiti (wa CCM) asikie, Halmashauri Kuu yangu (ya CCM) isikie. Mchakato huu usiingiliwe, madiwani saidieni wananchi wenu kujielewa. Muungano hautaponywa kwa helikopta zinazoruka au vitabu vinavyosambazwa.”
Muungano
Kuhusu Muungano, Butiku aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini alisema: “Mimi ni mzee sasa, sitaki kwenda kaburini bila kuwaambia ukweli. Endeleeni kuujadili, msifanye jambo la kutaka asali bila kujua madhara yake,” alisema.
Kauli hiyo ya Butiku ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mfuko wa Mwalimu Nyerere ilitokana na wajumbe kuonyesha mvutano kuhusu muundo wa Serikali katika Muungano na wengi walionekana kuelemea upande wa Serikali mbili uliopo sasa, baadhi kuunga mkono Rasimu ya Katiba inayopendekeza Serikali tatu, huku wachache wakitaka Serikali moja.
Butiku aliwataka wajumbe wa Mabaraza ya Katiba kutoa maoni yanayolenga kulinda na siyo kuvunja Muungano na kwamba Tume ya Marekebisho ya Katiba imepewa kazi ya kuulinda akisisitiza kwamba haikuwa, wala haina ajenda ya kuvunja.
“Wapo pia viongozi wakubwa ndani ya Baraza la Wawakilishi, wengine wamestaafu, hawautaki Muungano. Tume inawafahamu wanaotaka Tume ya Katiba iwe na ajenda ya kuvunja Muungano. Muungano huu, ulimfukuza Aboud Jumbe madarakani, kiongozi mkubwa tu, mi nawaambia mambo mengine siri. Jumbe alitoka kwenye mkutano wa CCM, kaja pale nje akakuta gari lake lingine siyo la Makamu. Leo, (anamtaja kiongozi huyo) anasema tulifanya makosa kuungana, anajiunga na Jumbe, anaanza kufanana na Uamsho,” alisema Butiku.
Butiku aliifananisha Katiba Mpya nzuri kuwa sawa na asali akieleza kuwa inahitaji umakini wakati wa kuiandaa, akifafanua kuwa unapoandaa asali lazima uwe makini vinginevyo unaweza kuambulia kushambuliwa na nyuki.
“Wajumbe msipokuwa wa kweli, badala yake watu wakaumwa na nyuki, mtatulaumu. Ukweli wanaufahamu wote ili waweze kuamua? Tumekubaliana kwenye Tume tuambiane ukweli ili tupate asali.”

Viongozi wamtuhumu Mwigulu Nchemba kushirikiana na polisi kutisha wananchi.

0
Share

Singida. Polisi wametanda  eneo la mkutano  wa Baraza la Katiba lililoandaliwa na Chadema, Wilaya ya Iramba.
Mkutano huo ulifanyika juzi katika Uwanja wa Soko la Zamani, ambako ni nyumbani kwa Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba. Baada ya kuwasili kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, askari walionekana kutanda kila kona ya uwanja huo.
Baadhi ya askari walikuwa wameshikilia mabomu ya machozi na marungu huku wakiwa wamevalia kofia ngumu,  lakini muda mfupi gari lililosheheni Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU) liliwasili  wanjani hapo na kuegeshwa pembeni mwa mkutano.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mabere Marando,   alikuwa wa kwanza kupanda jukwaani na kukemea kitendo hicho.
“Ndugu zangu polisi mnatumika vibaya jinsi mlivyokaa hapa mkiwa mmevalia kofia zenu na mabomu kama vile mnataka kupambana na wahalifu, ni kitendo kibaya,” alisema Marando na kuongeza:
“Huu mkutano umeruhusiwa  kisheria na Tume na nyie hamna mamlaka ya kuuzuia,  ila nadhani haya ni maagizo kutoka kwa Mbunge Mwigulu Nchemba kama tulivyokuwa tumeelewa kabla ya kufika. “Naye Dk Slaa aliwataadharisha polisi kuacha tabia ya kufanya kazi zao kwa maelekezo ya watu, bila kufuata taaluma zao.
“Kila siku tunawalalamikia polisi kuwa chanzo cha vurugu, huu ni ushahidi tosha mmezunguka jukwaa langu lote huku wananchi ambao ni walengwa mmewasogeza mbali,” alisema Dk Slaa na kuongeza:
“Sikuja hapa kuongea na nyie, nimewafuata wananchi naomba mtoke mkae mbali ili watu wangu wasogee karibu na hiyo ni amri.”
Kitendo ambacho kilipokelewa kwa shangwe na wananchi kwa kushangilia na kuweza kusogea karibu ya jukwaa.

Ponda Dar mpaka Moro kwa Helikopta

Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda alisafirishwa jana kwa helikopta kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro na kupandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa kujibu mashtaka yanayomkabili.
Ponda jana alianza kwa kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu asubuhi na kufutiwa mashtaka ya uchochezi yaliyokuwa yakimkabili baada ya kusomewa mara ya kwanza Agosti 14, mwaka huu akiwa kitandani katika Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Muhimbili, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea kumshtaki.
Alidaiwa kutenda makosa hayo katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano kati ya Juni 2 na Agosti 11 mwaka huu.
Ponda alifikishwa mahakamani hapo saa 12 asubuhi na baadaye alipandishwa kizimbani na kufutiwa kesi hiyo, baada ya Wakili Kweka kuwasilisha hati hiyo ya DPP chini ya Kifungu cha 91 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).
Hata hivyo, baada ya kufutiwa mashtaka hayo, aliendelea kushikiliwa na kisha akachukuliwa na kupelekwa Morogoro ambako pia alisomewa mashtaka ya uchochezi.
Kuwasili Moro
Sheikh Ponda aliwasili kwa helikopta ya polisi na kutua kwenye Uwanja wa Gofu, Morogoro akiwa chini ya ulinzi wa polisi na alipakiwa kwenye gari maalumu ambalo liliongozana na magari mengine matatu ya polisi huku ulinzi ukiwa umeimarishwa katika eneo la Mahakama ukiwajumuisha askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), askari wa upelelezi, Usalama wa Taifa pamoja na mbwa wa polisi na kusababisha shughuli za kazi katika Mahakama hiyo na ofisi za jirani kusimama kwa muda.
Baada ya kufika mahakamani saa tano asubuhi, magari yalisimama kwa takriban dakika 30 kabla ya kumtoa na kumwongoza kwenye Mahakama ya wazi ambayo tayari ilikuwa umejaa watu.
Baada ya kumalizika kusomwa kwa kesi hiyo, msafara uleule ulimrejesha Uwanja wa Gofu saa sita mchana na kupandishwa kwenye helikopta kurejea Dar es Salaam.
Mahakamani Morogoro
Ponda alisafirishwa kwa helikopta ya polisi hadi Morogoro na kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi akiwa chini ya ulinzi mkali.

Vigogo kutoa ushahidi dhidi ya Mbunge Lema

Arusha. Mkuu wa Chuo cha Uhasibu cha Arusha, John Nanyaro na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha, Gillis Mroto, leo wanaanza kutoa ushahidi katika kesi ya tuhuma za uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
Mashahidi wengine katika kesi hiyo ni, Mkaguzi wa Polisi Bernard Nyambanyana na mwenzake aliyetajwa kwa jina moja la Jane.
Hali kadhalika PC Godfrey na Joachim Mahanyu . Wakili wa Serikali, Elinenya Njiro, alitaja mashahidi wengine watakaotoa ushahidi wao mahakamani kuwa Faraji Mnepe, Benjamin Simkanga na Naibu Hamidu, wote kutoka Chuo cha Uhasibu.
Lema anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo, alikwenda katika Chuo cha Uhasibu cha Arusha, mithili ya mtu aliyekwenda kwenye send-off na kwamba hajui chuo hicho kilipo wala mauaji ya mwanafunzi wa chuo hicho.
Wakili Njiro alidai kuwa mbunge huyo alitenda kosa hilo Aprili 24 mwaka huu, akiwa katika eneo la Freedom Square ndani ya Chuo cha Uhasibu na kwamba kitendo hicho kinapingana na kifungu cha 390 sura ya 35 ya sheria ya kanuni ya adhabu.