Tuesday, November 20, 2012

Wataka ziara za rais zidhibitiwe,ni maoni a katiba mpya

ZIARA za nje za Rais jana ziligeuka hoja kuu wakati wajumbe wa tume ya maoni ya Katiba walipokutana na wananchi wilayani Karatu ambapo baadhi walipendekeza Katiba mpya ipange idadi ya ziara za Mkuu huyo wa nchi ili kuwabana wenye hulka ya safari zisizo na tija kwa gharama na kodi ya umma.

Phillipo Josephat (40), mkazi wa Rhotia wilayani Karatu aliomba licha ya kupanga idadi maalumu ya ziara za nje ya nchi kwa Rais, pia idadi ya watu anaoambatana nao idhibitiwe kupunguza gharama.

Utakuta Marais wa nchi maskini kama yetu wanafanya ziara nyingi za nje wakiwa na misafara mikubwa kuliko hata wenzao wa nchi zilizoendelea. Na kwa sababu hawabanwi, kila anayeingia madarakani huamua kusafiri atakavyo bila kuangalia faida na hasara za safari zake kwa Taifa,î alisema Josephat.

Arther Gurti yeye alipendekeza Katiba iondoe mamlaka ya uteuzi wa Jaji Mkuu na wajumbe wa Tume ya Taifa ya uchaguzi mikononi mwa Rais, badala yake nafasi hizo ziombwe kwa sifa za kitaaluma na uadilifu wa
waombaji.

Alisema baada ya kuomba na kuchujwa, majina machache yawasilishwe mbele ya kamati maalumu itakayoundwa na bunge ambayo itawahoji na kupendekeza majina machache yatakayowasilishwa kwa Rais kwa uteuzi wa mwisho kabla ya bunge zima kuidhinisha jina la mteule.

Kwa upande wake, Orbano Michael yeye alitaka katiba mpya imnyangíanye madaraka Rais kuteua watu 10 kuingia bungeni badala yake aruhusiwe kuteua watu kushika madaraka ya Uwaziri kutoka nje ya bunge ili kupanua wigo wa uteuzi unaotumika kuteua wabunge.

No comments:

Post a Comment