Thursday, November 22, 2012

you must read!!Makala: Uwongo na Ufisadi ni Kansa-Zitto na Demokrasia

Katika kitabu chake kiitwacho Africa – Altered States, Ordinary Miracles mwandishi Richard Dowden anaelezea viongozi wa kiafrika kwa mfano wa Mwanafunzi aliyemfundisha nchini Uganda Willy Kiyingi. Willy alikuwa ni kijana mwenye akili nyingi sana shuleni. Alikuwa anashika nafasi ya kwanza kila siku darasani. Siku moja akaiba pesa za mwalimu wake, akaenda dukani kujinunulia suti na viatu. Kisha akapanda taxi kurudi kijijini na kushuka katikati ya soko la kijiji, watu wakamwona na kumshangilia. Siku ya pili akafukuzwa shule kwa kosa la wizi. Hivyo ndivyo Willy allivyokatisha maisha yake: kwa suti, viatu na taxi. Ufahari wa siku moja tu ukamaliza ndoto zote za maisha yake. Hii ni sura ya ufisadi katika mataifa mengi ya Afrika. Tanzania inao kina Willy wengi sana.
Mkutano uliopita wa Bunge ulidhihirisha namna ambavyo tabia za uwongo zinaweza kuhatarisha Taifa. Katika mkutano wa kabla ya mkutano wa Tisa wa Bunge, Mkutano wa Nane wa Bunge la Kumi, kulikuwa na tuhuma kadhaa dhidi ya Wabunge. Baadhi ya tuhuma zimegundulika kuwa ni za uwongo. Tuhuma zingine zimefunikwa tu bila kuzitolea maamuzi ya Kibunge. Lakini Mbunge yeyote makini alijua kuwa tuhuma zile zilitungwa kwa sababu maalumu – kupitisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini. Lakini Bajeti ile haikuwa na tishio lolote la kupitishwa. Waziri na Manaibu wake walikuwa wanaungwa mkono na wabunge wengi sana na hivyo hata kama Kamati ya Nishati na Madini ingetaka kuzuia Bajeti, Bunge linegipitisha. Badala yake Wizara ikaingia kwenye kutunga uwongo, kupata ushujaa wa siku chache na kisha kuaibika kwa kuonekana wanasema uwongo.
Wabunge na wananchi nao waliingia mtegoni. Wabunge waliitwa kwenye Ofisi za Wizara na kutajiwa wala rushwa. Wabunge wakawaka moto ndani ya Bunge. Ukisoma kumbukumbu za Bunge za tarehe 27 na 28 Julai utaona namna wabunge walicharuka. Walipoitwa kutoa ushahidi kwa yale waliyoyasema, wakabaki wanatoa macho kama mjusi aliyebanwa na mlango. Spika alipowasomea kuwa walikurupuka tu (walitumwa) wakabaki wanalalamika kuwa ‘kesi ya nyani anahukumu ngedere’ na kusahau kuwa duniani kote Mabunge hujiwekea taratibu za kujidhibiti. Wabunge wengine ni watu jasiri na wenye uzalendo usio na mashaka. Lakini umaarufu wa siku moja ukawaingiza kwenye historia ya kuwa watu wanaotumika.
Jambo ambalo wananchi hawalijui ni kwamba, siku ya uwasilishaji wa hotuba ya Wizara ya Nishati na Madini ndio siku ambayo Wabunge waliongezewa mishahara yao kimya kimya wakati Walimu na Madaktari wanalia. Suala hili halikuingia kabisa kwenye mjadala kwani wananchi waliwaona wabunge wanawasemea. Wakawapigia ngoma za furaha, wanawatetea. Juhudi zote za kupinga nyongeza zisizo halali za malipo ya wabunge zikasinyaa. Utawapinga mashujaa wanaopinga ufisadi?
for more 
click here  

Zitto na Demokrasia

No comments:

Post a Comment