Saturday, November 17, 2012

Zungu akana kuishitaki TAKUKURU,ni katika hali ya kutaka kujisafisha

MBUNGE wa Jimbo la Ilala, Mussa Zungu (CCM), ameibuka na kusema hajawahi kutamka wala kufikiria kuifikisha mahakamani Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hivi karibuni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo habari jana, Zungu alisema kuwa anaamini TAKUKURU ni chombo kinachofanyakazi zake kwa taratibu na umakini mkubwa.
Zungu ambaye ni Mwenyekiti wa Bunge na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, alisema kuwa chombo hicho kifanya kazi yake kwa umakini ndiyo maana kilimhoji kutokana na tuhuma za kutoa rushwa wakati wa mchakato wa kugombea nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), kupitia Jumuiya ya Wazazi.
“Inasikitisha sana kuona jambo hili linakuzwa kwa kiwango cha juu kupitia vyombo vya habari, Tukukuru naiamini, ni chombo ambacho kinatenda haki, wala hakitumiki kisiasa, ndio maana nilitoa ushirikiano wakati wa mahojiano, japo mimi nina haki za kibunge ambazo zinanilinda,” alisema.
Alisema kwa kutambua umuhimu wa kazi za TAKUKURU na hana mashaka na uadilifi wake, ndiyo maana aliwaruhusu watu hao kupekua gari lake ambamo hawakukuta kitu chochote, jambo ambalo liliwafanya waongozane naye hadi katika ofisi za taasisi hiyo kwa mahojiano.
Alisema msingi wa tuhuma hizo nzito kwake ni siasa alizoziita za Dar es Salaam, ambazo zimepandikizwa na kuwa zilianza kipindi kirefu.
chanzo-Tanzania daima

No comments:

Post a Comment