Saturday, November 17, 2012

Watu wengi wamejitokeza mapema nchini Sierra Leone kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu.hapo jana


Rais Ernest bai Koroma wa Sierra Leone
Mwandishi wa BBC anasema watu wengi wanaifikiria Sierra Leone kuwa nchi ya fujo tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka ya 1990.
Lakini sasa sivyo ilivyo.
Uchaguzi unafanywa katika hali tulivu na ya kidemokrasi.
Uchumi unakuwa kwa haraka ingawa ulikuwa umeanguka sana wakati wa vita.
Na bado Sierra Leone ni nchi maskini.
Rais Ernest bai Koroma anapingwa na wengine kadha katika kuania urais.
Uchaguzi unasimamiwa na maelfu ya wachunguzi wa Sierra Leone wanaolipiwa na serikali ya Uingereza.
Jeshi la Uingereza lilingilia kati nchini Sierra Leone mwaka wa 2000 kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Kwa hivo ni sawa kwa serikali ya Uingereza sasa kugharimia usimamizi wa uchaguzi ili kuhakikisha kuwa serikali mpya imechaguliwa kwa njia za kidemokrasi na halali.
chanzo-bbc.com

No comments:

Post a Comment