Wednesday, November 14, 2012

kutoka kijiji cha MAISHA PLUS: Justin, Mama Kevi warejea kijijini

JUSTIN Bayo kutoka Morogoro na Berenik Kimiro ‘Mama Kevi’ wa Dar es Salaam, juzi usiku walirejea katika Kijiji cha Maisha Plus na kusababisha wanakijiji kulipuka kwa shangwe baada ya kuwaona.
Washiriki hao waliingia kijijini wakitokea ‘kula bata’ na kuwakuta wenzao wakiwa wamekaa kwenye kikao cha usiku, wakijadili mipango ya maendeleo.
Justin na Benerik walikumbatiwa kwa furaha na wenzao.
Awali, washiriki hao walipata kufurahia maisha kwa siku moja ndani ya Hoteli ya City Style ya jijini Dar es Salaam, huku wenzao wakidhani kwamba wametolewa kijijini moja kwa moja.
Wanakijiji kutozwa kodi bidhaa
HALI ya mambo ndani ya Kijiji cha Maisha Plus imeanza kubadilika, baada ya uongozi mpya ulio chini ya uenyekiti wa Venance Mushi wa Dodoma, kuwatangazia wanakijiji kulipa kodi ya bidhaa ya sh 500 kwa siku.
Utaratibu huo mpya wa kodi ya bidhaa, umekuja baada ya wanakijiji hao kutengeneza bidhaa nyingi na kununuliwa na watazamaji.
Venance, aliwatangazia wanakijiji hao alipokuwa ameitisha mkutano mbele ya Babu.
Aidha, kwa mara ya kwanza uongozi huo uliwanunulia chai wanakijiji huku vitafunwa wakijitegemea, kabla ya kuwatangazia suala la kodi.
Mbali na kiasi hicho cha sh 500, wanakijiji hao hutozwa sh 100, kama malipo ya pango kijiji hapo kwa kila siku.
Kumi waingia kikaangoni
WASHIRIKI kumi wameingizwa kikaangoni wiki hii, ambapo watatu kati yao wataondolewa kijijini endapo watapata kura chache.
Washiriki waliokikaangoni ni Rashid Ndunduke (MP 03), Bahati Kisula (MP 05), Dora Mhando (MP 06), Swaumu Shabani (MP 10).
Wengine ni Magreth Msedhu (MP 11), Tatu Masoud (MP 13), Saad Mohamed (MP 16), Gabriel Lwinga (MP 18), Hidaya Abdallah (MP 20), na Jonathan Joachim (MP 22).
Ili kuweza kumuokoa mshiriki umpendae, andika MP na namba yake, kisha tuma kwenda 15584.
Mashabiki watembelea kijijini
JUMAPILI iliyopita, mashabiki wa Maisha Plus, kupitia mtandao wa kijamii (facebook), Regina na Mary, walipata fursa ya kutembelea Kijiji cha Maisha Plus na kushuhudia mambo mbalimbali ndani ya kijiji hicho.

No comments:

Post a Comment