Wednesday, November 28, 2012

SHARO MILIONEA ALIMPENDA MAMA YAKE KUPITA MAELEZO …ILIKUWA AMFUNGULIE DUKA

MAJRANI wa familia ya marehemu Sharo Milionea kijijini Jibandeni, Lusanga, wanasema hawajawahi kuona mtu aliyekuwa anampenda mama yake kama Hussein (Sharo Milionea).
Mzee mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mzee Saidi akiwa na kundi la majirani wenzake, aliiambia Saluti5 kijijini hapo kwamba haujawahi kupita mwezi mmoja bila Sharo kuja kumtembelea mama yake.
“Alijua vilivyo majukumu yake, alijua kuwa yeye ndio mhimili wa familia yao, alihakikisha kila mwezi lazima aje mara moja au zaidi kumsalimia mama yeke” alisema mzee huyo na kuongeza kuwa msanii huyo alikuwa mtu wa watu kijijini hapo “Hakulewa sifa, aliendelea kuwa Hussein yule yule tuliyemlea hapa”.
Inaaminika Sharo Milionea alikuwa na mipango ya kumfungulia duka mama yake ili kujikimu kwa shida ndogo ndogo na inasemekena hata miongoni mwa vitu vilivyoibiwa kwenye gari lake ikiwa ni pamoja na pesa milioni sita kulikuwepo pia bidhaa kibao mahususi kwa ajili ya duka alililotaka kumfungulia mama yake.
Mama yake ambaye ana ulemavu wa mguu inaaminika atakuwa amepata pigo kubwa sana kwa vile Sharo alikuwa ndio kichwa cha familia.
Kwa kulewa hilo, Msanii mkongwe, Mzee Majuto aliiambia Saluti5 kuwa atapambana kadri awezavyo kuhakikisha kuwa mama huyo anapata matunda ya kazi za mwanae.
Sharo alifariki kwa ajali ya gari akiwa njiani kwenda kumsalimia mama yake ambapo alitaka akae nae kwa usiku mmoja kisha kesho yake arejee Dar kwa ajili ya mazishi ya msanii mwenzake John Stephano Maganga.

No comments:

Post a Comment