Friday, November 30, 2012

Bunge la USA kujadili vikwazo dhidi ya Iran

Bunge la Senate nchini Marekani litajadili vikwazo vipya vilivyowekewa Iran kwa lengo la kuikomesha nchi hiyo kuendelea kuzalisha madini ya uranium ili itengeneze silaha za kinyuklia.
Vikwazo hivyo vipya, vilivyowasilishwa katika bunge la Senate la Marekani hapo jana, ni pigo kwa sekta ya kawi nchini Iran.
Vikwazo vya awali vilipunguza kwa kiasi kikubwa mauzo ya mafuta nje ya Iran na kuathiri uchumi wake. Tehran inasisitiza kuwa mpango wake wa kinyuklia ni kwa manufaa ya wananchi wa Iran.

No comments:

Post a Comment