WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA HASEMI UKWELI, ANASIMAMIA UJANJA.
Mradi wa kujenga bomba la kusafirishia gesi MTWARA DSM utalipotezea
taifa shs. Trilioni 1 (bilioni 1000) , na fedha hizi zitarudi mikononi
mwa mafisadi na baadaye zitakuwa silaha nzito ya wezi hao katika
kuhujumu demokrasia na haki za wananchi.
Kuleta GESI kwa bomba
DSM ni sawa na ufisadi mwingine wowote ule, wizi ni wizi tu na lazima
tuutamke, hata kama wizi huu wa sasa unatetewa na anayejiita "mtoto wa
mkulima anayewagharimu wakulima".
Kama suala ni kuwa umeme unapaswa kufikishwa DSM ili kulinufaisha
taidlfa zima tujenge mitambo ya umeme Mtwara na tusafirishe umeme wa
waya angani ambao ni nafuu na utatumia nusu ya gharama zinazohitajika
kutandika bombabla gesi.
Kama hoja ya serikali ni kuileta gesi
ya matumizi ya majumbani nchi nzima na kwqmba lazima ifikishwe DSM kuna
njia rahisi, bandari ya mtwara imekaa bila kazi yoyote miaka nenda miaka
rudi, tunashindwa kuikarabati na kuipanua kwa gharama zisizozidi
bilioni 100 kisha tukaanza kusafirisha gesi safi MTWARA hadi DSM kwa
njia ya bandari hadi bandari? Nani ameturoga? Nani ametufumba macho
tunaoneshwa na hatuoni? Nani ametuziba masikio tunasikilizishwa na
hatusikii?
Bomba hili limekuwa bomba, nzi yuko tayari kufia
kwenye kidonda. Hawaoni aibu kabisa CCM, hata wizi huu wa wazi wa bomba
wanaung'ang'ania kwa nguvu ilimradi tu lengo lao la kupiga "mahela" ya
kujipanga na uchaguzi wa 2015.
Watanzania masikini, tunaibiwa
hivi hivi na hivi sasa ni kama tuko msibani, vyombo vya habari vimeanza
kucheza muziki wa Pinda na kusifia huku vikijua taifa linaliwa na
kwamba kuna kila harufu ya rushwa na ufisadi na wizi wa wazi kwenye
mradi wa ujenzi wa bomba.....lol...
Yesu wala Mtume Mohhamad
hawatashuka kuja kutusaidia katika wizi huu, mungu ametupatia akili na
utashi, lazima tuvitumie kudai haki zetu, kupigania maslahi ya nchi
yetu, kukataa kuonewa, kukandamizwa na kukubali kutawaliwa bila huruma
na "wakoloni weusi".
No comments:
Post a Comment