Robin van Persie akisherehekea bao lake
Manchester United, imeendeleza
uongozi wake katika msururu wa ligi kuu ya Premier ya England baada ya
kuilaza Liverpool kwa magoli mawili kwa moja, katika mechi iliyochezwa
katika uwanja wa Old Trafford.
Nyota wa Manchester United, Robbin Van Persie, ndiye aliyeifungia United bao lake la Kwanza.Mchezaji wa ziada wa Liverpool, Daniel Sturridge ambaye alisajili hivi majuzi kutoka kwa klabu ya Chelsea alifufua matumaini ya Liverpool kwa kufunga bao moja.
Licha ya Liverpool kuimarika katika kipindi hicho cha pili mechi hiyo ilimalizika Manchester United 2 Liverpool 1.
Kufuatia ushindi huo, Manchester United ingali kileleni mwa ligi hiyo na alama 55, alama saba nyuma ya mahasimu wao wa karibu Manchester City.
No comments:
Post a Comment