Thursday, January 17, 2013

Jimbo Katoliki la Bukoba Lapata Askofu Mpya


KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani baba Mtakatifu Benedict wa 16 amefanya mabadiliko kidogo katika safu ya uongozi wa Kijimbo , kanisa Katoliki Tanzania.

Kwa Francisco Padilla mhashamu Baba Askofu Desiderius Rwoma wa Singida amehamishwa na kuwa Askofu mpya wa Jimbo la Bukoba.

Askofu Rwoma anarejea jimbo la Bukoba alipoanzia Uaskofu kama askofu msaidizi kabla ya kuteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Singida mwaka 1999.

Kuteuliwa huko kunatokana na Baba Mtakatifu kuridhia kustaafu kwa Mhashamu Baba Askofu, Nestor Timanywa wa Jimbo la Bukoba.

Akizungumza, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania(TEC), Padri Anthony Makunde alisema kuwa mbali na kuteuliwa huko, pia Askofu Rwoma atakuwa Msimamizi wa Kitume wa Jimbo la Singida.

Askofu Rwoma ambae kwa TEC anasimamia idara ya Utume wa Walei, alizaliwa mwaka 1947 katika parokia ya Rutabo, Kamachumu jimbo Katoliki la Bukoba akitokea Parokia moja na Mwadhama Laurean Kardinali Rugambwa na alipata upadrisho kwa mikono ya Baba Askofu Timanywa, mwaka 1974 Rutabo.

Akiwa jimboni Bukoba aliwahi kuwa gombera wa seminari ya Rubya kwa miaka mingi na Mapadre wengi vijana jimboni Bukoba walipitia mikono yake hivyo anawajua vizuri na wanampenda.

Aidha alikuwa mlezi wa kiroho wa shirika la Masista wa Mtakatifu Terezia wa Mtoto Yesu, shirika la jimbo na hivyo analifahamu vizuri na kila mara amekuwa karibu.mujibu wa balozi wa Baba Mtakatifu nchini Tanzania, Askofu Mkuu

No comments:

Post a Comment