WABUNGE waliochomewa nyumba na mali zao katika vurugu
zilizotokea Mtwara juzi; Anna Abdallah na Mariam Kasembe, jana
waliangulia vilio walipotakiwa na gazeti hili kuzungumzia tukio hilo.
moja ya nyumba ya mbunge iliyochomwa juzi huko mtwara |
Nyumba za wabunge hao wa Viti Maalumu na mali
zingine kadhaa za taasisi mbalimbali, ni miongoni mwa vitu
vilivyoharibiwa katika vurugu hizo ambazo pia zilisababisha vifo vya
watu wanne wilayani Masasi.
Akizungumza kwa huzuni, Anna alisema hajui sababu
za uharibifu huo, hasa ikizingatiwa mwenyewe amekuwa huko kwa karibu
siku tatu na hakuona dalili za uhasama wowote dhidi yake.
Anna ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho
alisema: “Nina siku ya tatu hapa Masasi na nimeshiriki mkutano wa
halmashauri kwa mwaliko na wakati wote, sikuhisi chochote hivyo siwezi
kujua sababu ya chuki iliyofanya nyumba yangu ichomwe moto,” alisema.
Alipotakiwa aeleze hali ilivyokuwa, alisema,
“Wavamizi hao walipora kila kitu nyumbani kwangu yakiwamo mapazia, kabla
ya kumwaga petroli kila chumba na kuwasha moto.”
Aliendelea kueleza,” Kila kitu kiliteketea. Inatia
uchungu kwani nyumba hiyo niliijenga kwa kudunduliza fedha kidogo
kidogo nikiwa mkuu wa mkoa.”
Anna alisema, kundi hilo la vijana lilivamia nyumbani kwake saa 4:00 asubuhi na kuanza kupora mali kwa kupita chumba kimoja baada ya kingine.
Anna alisema, kundi hilo la vijana lilivamia nyumbani kwake saa 4:00 asubuhi na kuanza kupora mali kwa kupita chumba kimoja baada ya kingine.
“Hali si nzuri. Kila kitu kimeibwa na nyumba
imechomwa moto, hakuna kilichobaki. Walichukua kila kitu na itanichukua
muda mwingi kujua thamani halisi ya hasara iliyopatikana,” alisema.
Kauli ya Kasembe
Naye Kasembe alipokea simu ya mwandishi wa habari hii kwa kilio na kuikata huku akisema, “Jamani niacheni… Mwenzenu naumia…!”
Alipopigiwa tena baadaye, alisema anashangazwa na tukio hilo ambalo limemfika bila kutarajia na kumtia hasara kubwa.

“Wamepora kila kitu katika nyumba na kuichoma
moto, sijui atakuwa nani huyu, kwani sina tatizo na wapiga kura wangu na
sina mgogoro na mtu yeyote. Nashindwa hata kuhisi nani kafanya
uchochezi,” alisema Kasembe.
Alisema wakati wa vurugu hizo, ndugu zake akiwamo
mama yake, walikimbia na kwenda kujihifadhi hotelini, lakini mpaka sasa
hawajui wataishi vipi baada ya nyumba hiyo kuteketezwa kwa moto.
“Jana wanafamilia walilala hotelini na leo tupo
nje ya gofu la nyumba yangu ambayo imeteketea kabisa kwa moto,
tunasubiri majaaliwa mengine, lakini nimechanganyikiwa kwa kweli na
sijui ni kitu gani hiki, siamini,”alisema.
Polisi waeleza uharibifu
Watu 44 wanashikiliwa na polisi wilayani Masasi kufuatia vurugu hizo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Maria Mzuki alisema watu hao wamekamatwa kwa wakituhumiwa kujihusisha na vurugu hizo zilizosababisha uhalibifu mkubwa mali.

No comments:
Post a Comment