Mlinda lango wa Cape Verde, Guy
Ramos amesema ana matumaini makubwa kuwa taifa lake ambalo linashiriki
katika fainali hizo kwa mara ya kwanza litafuzu kwa raundi ya pili kwa
fainali.
Cape Verde inachuana na wenyeji wa mashindano hayo Afrika Kusini katika mechi ya ufunguzi siku ya Jumamosi.Ramos amesema ''ikiwa tutacheza mechi hiyo vyema bila shaka watafuzu kwa raundi ijayo''.
Ramos, ambaye anaichezea klabu ya RKC Waalwijk, ya Uholansi, alisema ''kama timu ya nchi ndogo zaidi barani Afrika, hakuna anayetarajia kuwa watashinda mechi yoyote, lakini tulishinda Cameroon 4-0, ambayo ni nchi kubwa na kinyume na matarajio ya wengi tulishinda. Kwa hivyo mbona sisi tusiwashinde Bafana Bafana?''
Ushindi utakuwa chachu ya matokeo mema
Kocha wa Cape Verde, Lucio Antunes, aliamua kuwaacha wachezaji wenye uzoezi na badala yake kuchagua kikosi kipya.
Aliyekuwa naodha wa timu hiyo Lito na mshambulizo Dady ambao wamekuwa nguzo ya timu hiyo ya Cape Verde, wameachwa nje.
Antunes pia atakosa huduma za mlinda lango Ricardo ambaye aliamua kusalia na klabu yake ya Pacos de Ferreira ya Ureno.
Kocha huyo amesema, itakuwa jambo ya kutia moyo ikiwa wachezaji wake watafanikiwa kuandikisha ushindi dhidi ya Afrika Kusini wakati wa mechi hiyo ya ufunguzi.
No comments:
Post a Comment