Tuesday, January 15, 2013

Shirika la ndege la BA lilimbagua mkristo


Nadia Eweida alilazimishwa kukoma kuvalia mkufu wake wenye msalaba
Mfanyakazi mmoja wa shirika la ndege la Uingereza , British Airways, alibaguliwa kazini kwa sababu ya imani yake ya kikristo.
Huu ndio uamuzi uliotolewa na mahakama ya haki za binadamu ya Ulaya.
Jaji wa mahakama hiyo aliamua kuwa haki ya mfanyakazi huyo Nadia Eweida zilikiukwa kuambatana na sheria ya haki za binadamu ya Ulaya.
Alifikisha kesi yake katika mahakama hiyo baada ya shirika la BA, kumlazimisha kukoma kuvalia mkufu wake uliokuwa na msalaba.
Majaji wa mahakama hiyo waliamua kuwa haki za wakristo wengine watatu pia zilikiukwa.
Baadhi wa wakristo wanavalia msalaba kama ishara ya imani yao
wakristo hao ni pamoja na Shirley Chaplin mwenye umri wa miaka , 57, ambaye mwajiri wake alimuamuru kukoma kuvalia mkufu wake wenye msalaba,mshauri nasaha Gary McFarlane, mwenye umri wa miaka 51 aliyeachishwa kazi kwa kusema kuwa hayuko tayari kutoa ushauri nasaha kwa wapenzi wa jisnia moja na msajili wa watu, Lillian Ladele, ambaye aliadhibiwa kwa kukataa kufungisha ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Wanne hao walifutwa kazi kwa sababu ya imani zao na kisha wakawasilisha kesi zao katika mahakama hiyo, lakini kesi zao zinasikilizwa kwa pamoja.
Kwa upande wake Nadia Eweida alipigwa marufuku kuvalia mkufu wake akiwa kazini.
Wakristo hao wanne wanadai kuwa hatua ya waajiri wao inakiuka haki zao za kibinadamu zinazowapa uhuru wa kidini.

No comments:

Post a Comment