MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa Philip
Mangula jana alionja machungu aliyowahi kupata Waziri Mkuu Mizengo Pinda
baada ya msafara wake kuzomewa jijini Mwanza.
Msafara huo wa Mangula ulizomewa jana muda mfupi baada ya kumaliza mkutano wake katika uwanja wa michezo Nyamagana.
Katika msafara huo mbali na Mangula pia walikuwapo Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, Naibu Waziri wa Ujenzi, Grayson Lwenge na Katibu Itikati na Uenezi, Nape Nnauye.
Katika msafara huo mbali na Mangula pia walikuwapo Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, Naibu Waziri wa Ujenzi, Grayson Lwenge na Katibu Itikati na Uenezi, Nape Nnauye.
Mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo, baadhi
ya wananchi waliokuwa katika mkutano huo ambao hawakuwa wamevalia sare
za CCM, walijipanga kando ya barabara ya Posta na wakati viongozi hao
wakipita waliwazomea huku wakionyesha ishara ya vidole viwili.
Kutokana na hali hiyo, vijana wa CCM maarufu kama
Green Guard walianza kuvamia wazomeaji hao na kuanza kutembeza kipigo
ambapo vijana wawili ambao majina yao hayakufahamika walijeruhiwa sehemu
mbalimbali za mwili.
Septemba 17, mwaka jana, ndani ya uwanja wa
Sahara, Pinda alizomewa na wananchi wakati akihitimisha ziara yake
jijini Mwanza, kutokana na kero nyingi zinazowakabili wakazi wa jiji
hilo, huku kiongozi huyo akiwataka waachane na ushabiki wa kisiasa.
Awali, akihutubia mkutano huo, Mangula alisema
pamoja na kwamba wapinzani wamekuwa wakibeza mafanikio ya ya CCM lakini
ukweli utabaki palepale kwamba katika kipindi cha miaka 50 ya utawala
huo nchi imepiga hatua za maendeleo.
Mangula alitoa mfano kuwa wakati wa miaka ya nyuma
kulikuwa na ghorofa moja la hospitali ya Bugando na sasa yapo
‘mabugando’ mengi.
Mbali na kuelezea mafanikio hayo pia aliwataka
wanachama wa CCM kutumia vikao katika mashina kuzungumza na wanachama
kubainisha matatizo yanayowakabili badala ya kuzungumza nje ya vikao,
jambo ambalo limekuwa likikigawa chama.
Hata hivyo, Mangula ambaye alikuwa akisubiriwa kwa
hamu katika mkutano huo, tofauti na matarajio ya wengi hakuzungumza
zaidi ya dakika tano.
Wakati akiondoka baadhi ya wananchi hao walisikika walilalamika kuwa walitarajia kusikia mengi lakini hakuna walichosikia.
Wakati akiondoka baadhi ya wananchi hao walisikika walilalamika kuwa walitarajia kusikia mengi lakini hakuna walichosikia.
Kutokana na hali hiyo wananchi hao waliamua kukaa
kando ya barabara ya Posta, nje ya uwanja huo na kuanza kuwazomea
viongozi waliokuwa wakipita.
No comments:
Post a Comment