WAZIRI wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard
Membe ametangaza kuwa hatogomea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.
Membe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mtama, mkoani
Lindi, alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwenye sherehe za Mwaka
Mpya nyumbani kwake.
“Unajua nimekuwa mbunge wenu kwa kipindi cha tatu.
Hivi leo ninawaaga rasmi kuwa sitagombea tena nafsi hii ya ubunge,”
alisema Membe.
, ambapo pia aliwataka wananchi wa mikoa ya
kusini, kuwa na subira katika kipindi hiki ambapo Serikali
inashughulikia mchakato wa kuvuna gesi asilia.
Alisema kuwa ni muhimu kwa wakazi wa mikoa
iliyopatikana gesi kutambua kuwa rasilimali zilinazopatikana nchini ni
mali ya Watanzania wote na siyo ya mikoa iliyogundulika pekee.
Waziri Membe aliwataka madiwani wa Halmashauri ya
Wilaya ya Lindi, kuacha kutumia vikao vya halmashauri kujadili malumbano
yasiyokuwa na msingi akisema kwamba kufanya hivyo ni kipoteza
rasilimali za wananchi bila faida.
“Salamu zangu za mwaka mpya ni kuwaomba madiwani
kuacha kutumia vikao kuwajadili madiwani wenzenu kwa hoja zisizokuwa na
maana, badala yake tujenge umoja na mshikamano ili kufanya kazi za
kusimamia miradi ya maendeleo,” alisema Membe.
Waziri Membe alitumia muda huo pia kuwataka madiwani kujipanga katika kusimamia matumizi ya fedha za miradi ya Halmashauri.
Baadhi ya wakazi na viongozi mbalimbali wa CCM na
Serikali mikoa ya Lindi na Mtwara walikusanyika jimboni kwa Membe
kusherekea kuadhimisha mwaka mpya.
Viongozi walioshiriki katika sherehe hiyo ni
pamoja Mbunge wa Mtwara mjini, Hasnain Murji, Godless Kweka ambaye ni
Mjumbe wa Nec, wajumbe wa Kamati ya Ulinzi Mkoa wa Lindi ikiongozwa na
Mkuu wa Mkoa, Ludovick Mwananzila na madiwani pamoja na viongozi wa dini
wa mikoa hiyo
No comments:
Post a Comment