January 30 2013 ndio nimefahamu
kwamba kumbe timu za taifa za Congo Brazzaville, Equatorial Guinea,
Rwanda na Swaziland ziliomba mechi ya kirefiki na timu ya taifa Taifa
stars lakini zikatoswa.
Baada ya hizo timu za taifa
kutoswa, iliyochaguliwa kucheza na Stars ni Cameroon katika mechi ambayo
iko kwenye kalenda ya (FIFA) ya mechi za kirafiki zitakazochezwa kote
duniani Februari 6 mwaka huu.
Hizo timu zote zilizotoswa
kasoro Swaziland, zilikua zinataka hiyo mechi na Taifa stars ichezwe
kwenye viwanja vya nyumbani kwao na sio hapa bongo lakini hii mechi ya
Tanzania na Cameroon itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia
saa 11 kamili jioni.
Kikosi cha Cameroon
kilichokamilishwa na wachezaji wengi wa kulipwa wanaocheza katika nchi
mbalimbali duniani kitaanza kuwasili bongo Februari 3 mwaka huu ambapo
pia TFF imesema Kocha wa Stars Kim Poulsen mwenyewe ndio alichagua stars
ichezwe na Cameroon ambayocaptain wake ni staa Samuel Etoo.
No comments:
Post a Comment